Kufika Loliondo kwa babu jamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kufika Loliondo kwa babu jamani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by One and Only, May 30, 2011.

 1. One and Only

  One and Only Senior Member

  #1
  May 30, 2011
  Joined: Mar 7, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Habari zenu great thinkers, naomba msaada wa mawazo mwenzenu, nina bibi yangu amegoma kula na hataki kuongea na mtu yoyote hapa nyumbani kisa kijijini kwao wazee wenzake wote wameenda kupata kikombe cha babu kasoro yeye kwa hiyo anataka kupelekwa loliondo. Mtu mwenyewe anamatatizo makubwa ya miguu, je kuna ndege za kwenda loliondo na kama zipo tutapata wapi? Apelekwe yaishe maana imekuwa taabu na hawezi kusafiri mwendo mrefu na gari anaumwa sana miguu. Nawasilisha janvini, msaada wenu jamani
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  mjomba tuingie PM mara moja, nitakusolvia shida hii right away!...
  If you are serious be serious!
   
 3. One and Only

  One and Only Senior Member

  #3
  May 30, 2011
  Joined: Mar 7, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Niko serious Paka very serious
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Atapata ndege, na atarudi anatembea kwa miguu yake...Nadhani hadi anapokomalia hivyo ujue ana imani ya kutosha kuhamisha milima!
  Nitakupa options kadha za kufika huko kwa ndege au helikopta, just at your convinience.
   
 5. One and Only

  One and Only Senior Member

  #5
  May 30, 2011
  Joined: Mar 7, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  I will appreciate that kiukweli
   
 6. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #6
  May 31, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  nikiwa samunge alikuja pilot mmoja na ndege ndogo nadhani inachukua watu watano ile anaitwa babu sambeke akatua na ile ndege barabarani dah raia tuliburudika saana maana 2 days tuko pale kwenye foleni ni sisi na wasonjo tuu na mbuzi choma zao. uwanja wa ndege upo nyuma ya mlima sehemu inaitwa wasso. baada ya hapo unachukua gari sijui ni bei gani.
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  May 31, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Kama utakuwa makini magari yale yako chini ya babu, na yana namba za serikali (SM)...Kinachofanywa pale ni kuchangia mafuta ambapo inabidi ipatikane 20K kwa kila abiria!
   
 8. r

  rachel kusia Member

  #8
  May 31, 2011
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole sana kwa matatizo ya bibi. Usafiri uje hadi Arusha, ufike arusha airport Kisongo, kuna Helicopta utapewa gharama ya kama dola elfu moja hadi mia saba hivi ila sina hakika ya gharama kwani kila mara inabadilika. Mtafute Kapten Barasa. Hiyo inatua nje kwa babu hakuna gharama zaingine za gari.
   
 9. N

  Nguto JF-Expert Member

  #9
  May 31, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,653
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Panda precision mpaka KIA na kutoka hapo si ipo ile helikopta ya ndesa!!!
   
 10. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #10
  May 31, 2011
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Hujasema uko wapi? Kama uko Mwanza kuna ndege ndogo za AURIC AIR zinaruka mara mbili kwa wiki kwenda kwa Babu. Unafanya booking kabla na namba ikitimia mnaenda na ndege inawangoja mnapata kikombe halafu mnarudi. Sina uhakika wa gharama kwa mtu mmoja.
   
 11. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #11
  May 31, 2011
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Mkuu sio wanatua pembeni ya barabara pale karibu na bonde la mto! Duh! nilitembelea huko na Wasonjo ameniput off! wanapenda sana pesa wale ahh! ugali mbichi na babu akisitisha shughuli kule watakufa na njaa maana wamesahau hata kulima na mbuzi zote zitakuwa zimeisha lol! Mkuu huyo bibi inabidi apande helicopter tu! milima na mavumbi yale vitamuua!
   
 12. terabojo

  terabojo JF-Expert Member

  #12
  May 31, 2011
  Joined: Aug 3, 2010
  Messages: 215
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Auric Air wanasafari za kibiashara kati ya Dar na Loliondo; na Mwanza Loliondo. Niliambiwa Mwanza/Loliondo/Mwanza ni laki tano na thelathini elfu - nadhani. Wapigie utapata unafuu kuliko kwenda arusha na kulipia helikopta
   
 13. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #13
  May 31, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Wakati PJ unaendelea kumpatia msaada Once and Only nimejifunza jambo na mimi pia kuwa at the moment kila njia inaelekea Samunge!

  1.. AURIC Air
  2.. Precision Air (in collaboration with Capt Barasa)
  3.. Babu Sambeke Air !
   
 14. One and Only

  One and Only Senior Member

  #14
  May 31, 2011
  Joined: Mar 7, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Asante sana mkuu, ntayafanyia kazi maelezo yako
   
 15. One and Only

  One and Only Senior Member

  #15
  May 31, 2011
  Joined: Mar 7, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Asante sana mkuu T, niko Dar so ntawasiliana nao kesho
   
 16. One and Only

  One and Only Senior Member

  #16
  May 31, 2011
  Joined: Mar 7, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Niko Dar, asante sana mkuu
   
 17. One and Only

  One and Only Senior Member

  #17
  May 31, 2011
  Joined: Mar 7, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Thanks every one, ngoja nikafanyie kazi msaada yenu, maana anatukosesha usingizi , she is 80 yrs lakini dah! hataki chochote mpaka apelekwe loliondo ndio kitaeleweka
   
Loading...