KUFELI KWA WANAFUNZI DAR

mlogolaje

JF-Expert Member
Nov 10, 2016
1,509
813
Wakuu habari za asubuhi kufeli kwa wanafunzi wengi shule za dar wakiwemo wavulana ambao ndo nataka niwazungumzie kutatengeneza tofauti kubwa baadae kati ya wanaume wa mkoani na wa dar

Tofauti itakayo kuwepo mbeleni kwanza wanawake wengi watawapenda wanaume wa mkoani kwa elimu yao pili wanaume wa dar watakuwa vibarua wakiwatumikia wa mikoani

Nawatakia jumapili njema
 
Mkuu ulitafakari kabla ya kuandika?dunia mzunguko wewe km ukikuwa hujui.....bila shaka hata wewe umemalizia shule mkoani na sasa unaishi dar.....
 
Hapa naona umeandika kwa kufikiria ila ukweli ni kuwa hata mikoani wamefeli sana na ukumbukuke watu walio peleka watoto wao kusoma nje ya dar ni wengi na ndo walio faulu huko mikoani
 
Mkuu ulitafakari kabla ya kuandika?dunia mzunguko wewe km ukikuwa hujui.....bila shaka hata wewe umemalizia shule mkoani na sasa unaishi dar.....
Mkuu nimezaliwa ocean road,nimekulia mtaa wa urambo kinondoni,nimesoma kinondoni shule ya msingi ikiongozwa na mwl mkuu mama makweta,,mmezama kwenye unga mnasahau na elimu
 
Mkuu nimezaliwa ocean road,nimekulia mtaa wa urambo kinondoni,nimesoma kinondoni shule ya msingi ikiongozwa na mwl mkuu mama makweta,,mmezama kwenye unga mnasahau na elimu
Nimekuelewa concern yangu ni kwamba sio wote waliofeli wataishi dar maisha yao yote na si wote waliofaulu mikoani wataishi huko.....elewa unaweza kusoma mkoani lakini family base yote iko dar..vice versa...! Ndo maana nikakwambia maisha ni mzunguko ndg......ingawa umezaliwa ocean road lakini inawezekana ukawa mgunya.....sasa je unapozungumzia wanaume wa dar ni akina nani sasa......huo mji wa wazaramo.
 
Kelele nyingi dar utandawazi maisha ya kwenye tv.sengeli, mdundiko,vigodoro.shida ya usafir,maisha yasio na maadili kwani wana ona mama na dada zao wakijiuza dar
Sasa hapo mtoto asipo wekwa sehem salama kwel anaweza kua na mda wakujisomea na kufaulu...hapana
 
Back
Top Bottom