Kufanyia mazungumzo ya amani Uarabuni

Kufanyia mazungumzo ya amani Uarabuni

Umkonto

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2018
Posts
3,117
Reaction score
5,372
Baadhi ya nchi za Uarabuni zimekuwa zikihusika katika mazungumzo ya amani katika migogoro mbalimbali ya kimataifa mfano Qatar.

Kwa mfano, Tshisekedi na Kagame walikuwa wanakimbiana kuanzia Dar, Angola, lakini wamekubali kukutana huko Qatar na kukubali kusitisha mapigano bila masharti. Si hiyo tu, mazungumzo ya amani ya nchi mbalimbali yameishawahi kufanyika Qatar mfa Palestina, Lebanon, nk.

Pia, katika mgogoro wa Ukraini, mazungumzo kati ya maafisa wa USA na Urusi, na Ukrain na USA yalifanyika uarabuni-Saudi Arabia.

Soma Pia: Hatimaye Tshisekedi na Kagame wakutana Qatar kujadili mzozo wa M23, wakubaliana kumaliza Vita DRC

Mchambuzi mmoja katika BBC Swahili kasema Qatar imekuwa ni nchi ambayo inajiweka kati, yaani haiegemei upande wowote, hivyo wagombanao wakiitwa Qatar chapu wanaenda mana wanajua wote watasikilizwa.

Heshima wanayoipata Qatar, na sisi TZ tuirudishe kama enzi zile za nchi zisizofungamana na upande wowote (Non-aligned movement) mpaka mazungumzo ya amani ya Burundi yakafanikiwa hapa Dar es Salaam.
 
Sawa Sawa
Tuitoe CCM
Lakini hawa CCM walikuwepo enzi zile Tanzania ikiitwa kisiwa cha amani duniani mpaka kuwa kimbilio la usuluhishi mfano Burundi huko Arusha!

Nakumbuka Arusha ilikuwa inaitwa a.k.a Geneva ya Afrika! Aisee!
 
Wakati Nchi nyingi za Kiafrika zinachukua Uhuru Qatar ilikuwa ni Kijiji cha wazamia lulu.
Na leo ndio matajiri duniani
Yaani historia za Waarabu ukiangalia mpaka makasia walikua wanapiga kwenda kuomba nyama Somalia.
Hii nimehadithiwa sana na waarabu nilipokuwa naishi huko FACT
 
Unajua kwanini Qatar na Saudia walipigana vita vya baridi?
Kwa sababu Qatar alikuwa anasapoti Somalia, turkey, Hamas, Muslim brotherhood, na brotherhood wa Egypt

Saudia akawa na msimamo tofauti ndio wakawa mahasimu mpaka kufungiana mipaka na kufunga biashara

Qatar alikuwa anategemea sana Saudia hata maziwa na cheese na nyama akafunga
Unakumbuka yule tajiri wa Qatar aliebeba ng'ombe kwa ndege?

Ili wafugwe kwa ajili ya maziwa?
 
Back
Top Bottom