Kufanya shopping na mwanamke

mr vata

JF-Expert Member
Jan 30, 2017
462
605
Hakuna kitu nakipenda katika kunogesha uhusiano kama kufanya shopping na mpenzi wangu, iwe kumfanyia shopping yeye binafsi, au shopping ya vitu vya nyumbani...
Hapa siongelei zile shopping za kushinikizwa bali zile shopping zinazotokana na mfuko kuruhusu.
Nimekumbuka na kuiongelea hapa kwa sbb ni miezi kadhaa sijafanya sasa, kuna kipindi ilikua ni sehemu ya maisha yetu lkn kwa sasa ninaona kama anasa. Kweli hali ni ngumu.
 
Duh kwa hii topic ni tamu sana. Mimi huwa nakomaa kwenda hizo shopping lakini inataka moyo. Kwa masela wengi wetu ukienda shopping unajua kabisa unataka jeans moja na t shirt labda unachukua biashara imeisha. Sasa huu ubavu wa kushoto bwana mkifika anataka sidiria mbili,atachagua arobaini,ajaribishe kumi na tatu,ili achukue mbili. Hapo inabidi mlume inabidi ukomae tu,hapo bado hamjaingia maduka kadhaa ambayo hanunui kitu,na akifika kwenye yale maduka ya vitu vya kinamama ndo nahisi yaani tumakaa humo masaa zaidi ya matatu. Sidhani hata kama huwa anahisi njaa wakati wa shopping,mbaya zaidi una mahesabu ya gemu la man united na liverpool linaloanza saa saba unusu ( kwa saa za nilipo). Hapo inabidi ukomae na kumuharakisha huwezi wala hutaki na wala huna ubavu maan usiku unakuja,utanuniwa mpaka ushangae. Kweli utu uzima dawa.
 
Kiukweli mi huwa na enjoy na niseme tu nime miss zile nyakati...
Kawaida huwa tunapanga vitu muhimu vya kununua huko tuendako hivyo tunatenga kabisa pesa ya vitu muhimu kwa makisio ya bei, na kunakua na ziada kidg.
Kuepuka usumbufu pesa huwa anabeba mama kwa hiyo yeye huwa ndio kiongozi wa msafara na anajua kwenye mfuko wangu hakuna kitu zaidi. Japo usumbufu upo lkn huwa nachukulia ni sehemu ya ukamilifu wao so sijawahi kuchukia kwenda shopping na mwanamke.
 
Duh kwa hii topic ni tamu sana. Mimi huwa nakomaa kwenda hizo shopping lakini inataka moyo. Kwa masela wengi wetu ukienda shopping unajua kabisa unataka jeans moja na t shirt labda unachukua biashara imeisha. Sasa huu ubavu wa kushoto bwana mkifika anataka sidiria mbili,atachagua arobaini,ajaribishe kumi na tatu,ili achukue mbili. Hapo inabidi mlume inabidi ukomae tu,hapo bado hamjaingia maduka kadhaa ambayo hanunui kitu,na akifika kwenye yale maduka ya vitu vya kinamama ndo nahisi yaani tumakaa humo masaa zaidi ya matatu. Sidhani hata kama huwa anahisi njaa wakati wa shopping,mbaya zaidi una mahesabu ya gemu la man united na liverpool linaloanza saa saba unusu ( kwa saa za nilipo). Hapo inabidi ukomae na kumuharakisha huwezi wala hutaki na wala huna ubavu maan usiku unakuja,utanuniwa mpaka ushangae. Kweli utu uzima dawa.
Unapaswa uwe na muda wa kutosha, lkn kama una ratiba nyingine za muhimu ni bora usiende shopping siku hiyo
 
Back
Top Bottom