Kufanya mazoezi barabarani hasa kukimbia sio hatari kiafya?

Ila watanzania hua hatujifunzi sijui kwann barabara hio hio bodaboda, baiskeli, maguta, magari Madogo kwa malori na hatujui madereva wamevuta au kunywa kitu gani na bdo unalikuta lijitu linakimbia Huku lina ma earphones ushamba tu wanawaiga wazungu wakat huko nchi zilizoendelea watembea kwa miguu magari baiskeli hawatumii barabara moja me Naona ushamba tu
 
Mimi nimejiamulia kukimbia kwenye njia ya hizi nyaya kubwa za umeme huku kimara kuelekea mbezi maana chini Kuna eneo pana ambalo Barbara zimewekwa. Huku hakuna Magari na kuna pikipiki moja moja Sana. It is safe kwa kweli
 
Mimi nakimbia huu mwaka wa 5 mfululizo. Mazoezi ya kukimbia barabarani (Road runner's) yapo dunia nzima watu wanakimbia. Ili kuimarisha usalama wako UCHAGUZI wa route ya kukimbilia ni muhimu sana, umakini barabarani, nguo na vifaa vya kukimbilia ni vitu vya kuzingatia sana na kumuomba Mungu.
Barabara nyingi kubwa kwa mfano kutoka Tegeta hadi posta mjini etc zina space iliyojitenga mbali kabisa na main road kwa waenda kwa miguu tumia hizo space vizuri..pia kuna barabara nyingine zina mstari unaotenganisha eneo la waenda kwa miguu hizi uwe nazo makini hasa uyaface magari upande yanapotoka ( keep right). Pia pendelea barabara ambazo hazina movement sana ya magari..hapo utakuwa safe sana.Zingatia sheria za barabarani kwa kuvuka kwenye zebra etc.

Kama unapenda kuvaa
headphones,vaa ambazo zitakufanya usikie kila kinachoendelea around.

Always focus mbele kuangalia kinachoendelea usipende kukimbia unaangalia chini.

Usipende kukimbia speed kali,hiyo speed kali nenda uwanjani

Pendelea kuvaa nguo za rangi rangi kama njano, ,orange ,nyeupe, pink, red etc au usiku zenye reflector au taa kabisa ili uweze kuonekana vizuri.

Hili la kusema kukimbia barabarani na utavuta harufu ya moshi na utakuathiri ni propaganda za madaktari.ziko kufikirika zaidi kuliko ukweli

Kikubwa muombe Mungu akupe ulinzi kama vile unavotaka kwenda kwenye shughuli zako unavoomba

Faida za mazoezi ya kukimbia ni nyingi sana ..inatibu magonjwa yote ya mtindo wa maisha, inasaidia kukata weight ,inakupa relaxation of body and mind (afya ya akili) , inaimarisha ulinzi wa mwili , nguvu za kiume inarejesha , magonjwa yote ya mfumo wa kike Tiba ni kukimbia, inakufanya uonekane kijana na mtu imara na nadhifu, magonjwa yote haya madogo madogo ya homa , mmengenyo wa chakula etc utayasikia tu kwa wengine, inasaidia kikubwa pia inasafisha damu kwa kuondoka sumu kwenye damu etc..inaimarisha mifupa na misuli, .Faida za mazoezi ya kukimbia ziko nyingi sanaaaa..naona wabongo wengi wanakimbia kupunguza vitambi tu.
USIOGOPE KUKIMBIA BARABARANI
"WE KIMBIA TU"
 
Ni kweli barabarani ni hatari kwasababu ya magari. Mwanariadha Simon Robert akiwa kwenye kiwango chake cha juu alipoteza maisha mwanzoni mwa miaka ya 90 kwa kugongwa na gari huko Arusha wakati akifanya mazoezi. Pia mazoezi ya kwenye lami yanaleta injuries kirahisi sana kwenye miguu. Kwa mlioko mijini ninawashauri nendeni viwanjani muwe mnazunguka uwanja. Wale wa Dar mnaweza kwenda beach pia. Mazoezi ya uwanjani ni mazuri kwasababu pia mnakutana wengi hivyo kunakuwa na mambo ya networking. Mimi nilikuwa naendaga Gym fulani maeneo ya Ilala ila nikaacha baada ya kuchukizwa na kitendo cha kina dada fulani kuja gym wamevaa mavazi ya kujifunika badala ya yale yaliyozoeleka.
Wee jamaa bangi sana ujue. Sasa wewe ulifata mazoezi au hao kina dada? Na ulitaka hao kina dada waje uchi? Mbona wewe hukwenda uchi? Unampangia mtu mavazi ya kuvaa?
 
Mwaka huu early July i think kama kumbukumbu zangu ziko sawa Mwanza walikufa watu 3+ kwa kugongwa na gari wakati wakifanya mazoezi barabarani.

Huwa naona ni kama watu kutafuta sifa tu maana nchi yetu barabara mbovu zipo kila mahali kwanini wasiende kukimbia huko wanaenda kupishana na magari barabarani kwenye lami kuwaonyesha wanaopita na magari yao kwamba hata wao wana magari yao ila wameamua kuyapaki ili kupunguza mafuta.
Umewaona wadada wanavyovaa hivyo vichupi Sasa pembeni ya barabara?Kuna njia ya mikwambe-kijichi Hadi unajiulizaa Hawa watu Wana mission gani?
 
Umewaona wadada wanavyovaa hivyo vichupi Sasa pembeni ya barabara?Kuna njia ya mikwambe-kijichi Hadi unajiulizaa Hawa watu Wana mission gani?
Hao mbona wanajulikana siku nyingi kwamba wanafanya biashara?kila jumamosi utawaona wakikimbia barabarani mixer wanaume,ninamfahamu jamaa anaishi Magomeni yeye hujiunga nao kila baada ya wiki mbili na akijiunga anaondoka na namba ya simu ya mmoja jumapili biashara imeisha anarudia tena hivyo hivyo.

Zile crews unazoona zinapigiwa chapuo sana na radio stations hao kina usafi na ile nyengine inayomilikiwa na mume wa yule binti aliyemuuwa kanumba wote wale hakuna anayefanya mazoezi ni biashara wanatangaza kupitia mgongo wa mazoezi.

Wanasema usimruhusu mumeo au mkeo kujiunga kwenye hivi vikundi,hao kuvuana nguo ni kama kugusa tu.
 
Hao mbona wanajulikana siku nyingi kwamba wanafanya biashara?kila jumamosi utawaona wakikimbia barabarani mixer wanaume,ninamfahamu jamaa anaishi Magomeni yeye hujiunga nao kila baada ya wiki mbili na akijiunga anaondoka na namba ya simu ya mmoja jumapili biashara imeisha anarudia tena hivyo hivyo.

Zile crews unazoona zinapigiwa chapuo sana na radio stations hao kina usafi na ile nyengine inayomilikiwa na mume wa yule binti aliyemuuwa kanumba wote wale hakuna anayefanya mazoezi ni biashara wanatangaza kupitia mgongo wa mazoezi.

Wanasema usimruhusu mumeo au mkeo kujiunga kwenye hivi vikundi,hao kuvuana nguo ni kama kugusa tu.
Kumbe wapo kazini...sijui Kwa Nini nimetamani kumjua huyo mtu wa magomeni🤦🤦
 
Back
Top Bottom