Kufanya kosa huku ukijua ni kosa

Kufanya kosa huku ukijua ni kosa

Tarime one

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2013
Posts
2,246
Reaction score
1,742
Kama siku mbili hivi nilikua nchi jirani kumwona rafiki yangu wa karibu sana ambae ni dr, katika maongezi yetu aliniambia jambo la kusikitisha sana na linamtesa sana kiakili na kihisia. Dr ana rafiki yake mkikuyu yuko well kiuchumi na ni muathirika wa virus vya ukimwi na dozi humtumia huyu jamaa yangu kumchukulia mara kwa mara kama utaratibu wa zile dawa ulivyo, kinachomtesa jamaa ni kwamba huyu bwana alitaka kuoa na akawa amempata binti mzuri tu ambae ni mwl.

Katika urafiki wao binti akamwambia yule bwana kwamba ni vyema wakapima kwanza kujua afya zao na mambo mengine yaendelee.Jamaa kakubari kupima na sababu anajijua akamfata rafiki yangu ambae ni dr na kumwomba asimamie zoezi na asimuumbue na akumtangulizia kiasi cha pesa kizuri tu na dr akakubali, wakapima na majibu dr kasimamia na yakatoka kwamba wote hawajaathirika, but ukweli ni kwamba binti alikua safi,wakawa wapenzi rasmi na hivi karibuni wanafunga ndoa.

Sasa dr hili jambo linamuumiza sana na ameshindwa atafanyaje coz ni kinyume cha maadili ya kidaktari na pia nafsi inamsuta kwa kufanya hilo jambo, actually nilishindwa nitamjibu nini au nimshauri lipi, zaidi nilimwambia afanye toba tu ndilo suluhisho,but ukweli yuko very stressed.

Naomba mnisaidie mawazo kwa hilo
 
Ingekuwa vizuri ungemshauri huyo Dr. Mapema asifanye hivyo au ungetafuta namba ya huyo binti na kumwambia ukweli tu.
 
Daaah kitu hii kitu huwa inanifikirisha sana aisee ni hatari kuwa na watumishi wanaoendekeza njaa kama hawa na wasiozingatia maadili ya kazi yao
 
Aisee binti wa watu ndo kafanyiwa hivyo, aisee dhambi sana
 
Ingekuwa vizuri ungemshauri huyo Dr. Mapema asifanye hivyo au ungetafuta namba ya huyo binti na kumwambia ukweli tu.

Tayari hili tukio limeishatendeka,na hao watu tayari wana mahusiano pia mwezi wa nane wanafunga ndoa,hii ataanzaje kumwambia binti?
 
Daaah kitu hii kitu huwa inanifikirisha sana aisee ni hatari kuwa na watumishi wanaoendekeza njaa kama hawa na wasiozingatia maadili ya kazi yao

Khantwe,maadili yamepotea hata sehemu zenye huduma muhimu kama hosp,naamini ni wengi wanaumizwa bila hatia kwa matendo kama haya.
 
Tayari hili tukio limeishatendeka,na hao watu tayari wana mahusiano pia mwezi wa nane wanafunga ndoa,hii ataanzaje kumwambia binti?

It was very simple, huyo daktari kama kweli angekuwa na huruma na wakati huo huo anataka kulamba hela, angelamba hela na siku hiyo hiyo angetafuta line ya simu hata iliyosajiliwa kwa jina lingine la mtaani, alafu anamtext sms binti. Na asijionyeshe kama ni yeye angejifanya tuu msamaria mwema. Then anamshauri waende sehemu nyingine kupima na binti awe ndo sterling wa kuamua wapi pa kwenda kupima ili jamaa asije akachakachua. Anyway kama ni maji yameshamwagika
 
hapo kuomba msamaha kwa Mungu haitoshi..damu ya huyo binti iko mikononi mwake ikiwa ataambikizwa ukimwi.

Mshauri amwambie huyo binti hata kwa siri..ukweli utamuweka huru na atajisikia amani.
 
Duh kuna mambo mengine unahitaji kukubali kuwa mbaya tu
 
It was very simple, huyo daktari kama kweli angekuwa na huruma na wakati huo huo anataka kulamba hela, angelamba hela na siku hiyo hiyo angetafuta line ya simu hata iliyosajiliwa kwa jina lingine la mtaani, alafu anamtext sms binti. Na asijionyeshe kama ni yeye angejifanya tuu msamaria mwema. Then anamshauri waende sehemu nyingine kupima na binti awe ndo sterling wa kuamua wapi pa kwenda kupima ili jamaa asije akachakachua. Anyway kama ni maji yameshamwagika

Na hili ndilo linamtesa sana,anajutia kweli kweli.
 
hapo kuomba msamaha kwa Mungu haitoshi..damu ya huyo binti iko mikononi mwake ikiwa ataambikizwa ukimwi.

Mshauri amwambie huyo binti hata kwa siri..ukweli utamuweka huru na atajisikia amani.

Nitamwambia ajaribu kufanya hivyo,unawezakuta hajaambukizwa ya mungu mengi.
 
Muambie rafiki yako aandike ujumbe kisha asionyeshe kuwa ni yeye,kisha amtumie yule dada akimuambia kuwa amshinikize jamaa wakapime tena ila sehemu nyingine kwa sababu amepata habar za uhakika kuwa amejihusisha kimapenzi na mwanamke mwenye kuathirika,kisha akatubu...maana toba ya kwel inaambatana na vitendo hivyo...
 
Back
Top Bottom