Kufanya kazi dar ama mkoani/ mtazamo wako ukoje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kufanya kazi dar ama mkoani/ mtazamo wako ukoje?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by toyoyobig, Sep 2, 2010.

 1. t

  toyoyobig Member

  #1
  Sep 2, 2010
  Joined: Jan 16, 2009
  Messages: 22
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Katika kuishi kwangu, kuzaliwa kukulia nakusoma NA KUFANYA KAZI katika jiji la DAR,nnaweza kusema ilikuwa jambo la bahati sana, manake kuna watanzania wengi hawajawahi kufika DSM. Lakini mtazamo wangu wa kuishi, kufanya kazi na kujiendeleza katika jiji la DSM ulibadilika ghafla pale nilipo pata kazi mkoani. Niligundua kuwa, mkoani, kwa mfanya kazi kunaweza kukawa better (KIUCHUMI NA KIMAISHA) kuliko DAR.

  Kwa wale waliopo mikoani sasa na ambaowalifanya kazi dar, MTAZAMO WENU UKOJE?
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,334
  Likes Received: 22,186
  Trophy Points: 280
  Njoo Mbeya, ukifanya kazi huku wala huto tamani kurudi DSM,
  hamna foleni, hamna misongamano, vyakula na matunda fresh.
  Hali nzuri ya hewa, yaani raha mtindo mmoja
   
 3. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Maisha popote tu ndugu yangu.
   
 4. t

  toyoyobig Member

  #4
  Sep 2, 2010
  Joined: Jan 16, 2009
  Messages: 22
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kweli maisha popote, lakini maisha gani ? ndio maana kila mtu anamipangilio ya maisha, sio kweli kwama maisha popote, ama maisha ni maisha tu.
   
 5. t

  toyoyobig Member

  #5
  Sep 2, 2010
  Joined: Jan 16, 2009
  Messages: 22
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nahicho ndicho ninacho kiexperiance mimi pia, hakuna taabu nying kama za DAR, FOLENI, MICHANGO, CHAKULA NA MIKANDAMIZO MINGINE MIINGI.
   
 6. K

  Kabengwe JF-Expert Member

  #6
  Sep 2, 2010
  Joined: Oct 20, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Maisha ya mikoani ni "cheap" compared to Dar.
  Ila Dar mzunguko wa pesa ni mkubwa sana kuliko mkoa wowote.

  Kama ni mfanyakazi wa level ya kati, maisha ya mkoani ni mazuri zaidi kuliko ukiwa Dar. Ila kama wewe ni mfanyabiashara na akili zako zinafanya kazi haraka kwenye kuona opportunities na kuexplore, then Dar inakufaa. Kama bongo lala, lazma ufunge biashara

  Kwa kifupi naweza sema Dar inawafaa Opportunists na mikoani watu wasio penda "ku-take risks"
   
 7. Papa Mopao

  Papa Mopao JF-Expert Member

  #7
  Sep 2, 2010
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 3,355
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Mahala popote penye crowd huwa kunakuwa na mazuri na mabaya yake, kwa mtazamo wangu Dar sasa hivi naweza sema nje ya nyumbani kwako kumeharibika sana yaani mambo mengi yanaivuruga sana kichwa na maisha ya kila siku, yaani kero zimejaa kupita kiasi! Mikoani hakuna mambo kama hayo tatizo ni mzunguko wa pesa ni mdogo basi! Ukitaka kutuliza kichwa chako na mambo mengine nenda mikoani!
   
 8. M

  MAKOLA Member

  #8
  Sep 2, 2010
  Joined: Jun 5, 2010
  Messages: 46
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  kwa kweli kwa mfanyabiashara dar kupo bomba ili mradi uwe unafikiri kwa kina kwani hakina kisichouzika dar mzunguko wa pesa upo bomba. lakini kwa mfanyakazi wa kawaida mwenye mshahara wa laki 4 , 5,6,7 na hana malupulupu dar sio kwema kwake. mimi nipo mkoani. nasema kwamba mkoani kunalipa kuliko dar, nina nyumba.
   
 9. Papa Mopao

  Papa Mopao JF-Expert Member

  #9
  Sep 2, 2010
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 3,355
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  (Kwenye red) Big up sana mkuu!

  Foleni inanyonya sana hela sababu mafuta zinaishia njiani!
  Vocha inakula sana hela!
  Michango ya harusi na mengineyo zinakula sana hela!
  Muda wa kupumzika ni kiduchu mno!
  Huwezi kufanya mambo mengi kwa siku moja Dar!
  dar kumeja pollution za kila aina!
  Dah niishie hapa!
   
 10. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #10
  Sep 2, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  binafsi ningependa ifanyike
  kampeni ya kuwahamasisha watu wapungue hapa dar....
  ukweli dar hapafai kama unapenda maisha ya utulivu.......
  binafsi ningependa kuishi mbali na kero za foleni,misongamano,kelele n.k

  tatizo ni kuwa huko mikoani kuna vitu vinakosekana..
  mwisho watu wanaamua kubanana hapahapa.......
   
 11. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #11
  Sep 3, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Ulimbukeni ndo unawafanya watu wakimbilie na kung'ang'ania Dar. Nakuhakikishia nimeishi mkoa mmoja wa wa nyanda za juu kwa miaka 3 nimefurahia maisha ile mbaya. Kwa ujumla maisha ni rahisi na ni stress free kind of life ambayo nimekuwa nikiishi. Dar ya leo hata ukiwa na gari tabu mtindo mmoja ili uwahi kazini kila siku unaamka saa 11 alfajori na kulala saa 5 usiku katika harakati za kupambana na foleni. Mikoani ni tofauti kabisa, hakuna misongamano hivyo kila utakapo kwenda ni ndani ya dakika chache umefika. Tabu ni kuwa siku wakija Twanga Pepeta ni balaa tupu maana mji wote unahamia ukumbini na hivyo kuwa kero. Ukipata nafasi ya kwenda mkoani nenda unaweza ku make maisha ile mbaya
   
 12. Erick_Otieno

  Erick_Otieno JF-Expert Member

  #12
  Sep 3, 2010
  Joined: Mar 28, 2010
  Messages: 630
  Likes Received: 944
  Trophy Points: 180
  Mkoani kiwanja chenye hati sh.600,000/-. mzunguko wa mjini radius yake yake haifiki kilomita moja kwa hiyo gharama za usafiri zinakua chini, vyakula fresh, ukiwa mfanyakazi wa kati network ni kubwa unafahamika na akina RPC, RC, wafanyabiashra wakubwa na wadogo n.k. unafahamika, siyo! Space kubwa nyumbani, na garden zinakubali vizuri tu kwenye mikoa mingi!!! Gharama za matibabu ni safi.....nafasi ya kulima na kufuga pia ni kubwa..biashara ndio zinachupukia!
   
 13. senator

  senator JF-Expert Member

  #13
  Sep 4, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Kwa tanzania Huduma muhimu zote zinapatikana dar..i mean elimu nzuri..ukitaka hata kusafiri lazima utie timu dar..DAr ni JIJI na mikoani kuna miji..Kufanya kazi dar hata kama kipato kipo cha kati unaweza kuwa na miradi midogomidogo maisha yakaenda.Kwa kifupi kufanya kazi Dar ni akili kichwani mkoani tegemea tarehe ya mshahara..kuna tofauti kubwa sana ya kufanya kazi mkoani na Bongo ..i mean Dar...kuna sehemu mikoani habari(magazeti) yanafika after two days ! ila maisha yanakwenda vyema tu..
   
 14. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #14
  Sep 4, 2010
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Ni kweli mkuu.
  Kwa kifupi mikoani kunawafaa watu walioridhika na hali walizonazo aidha kielimu au kimapato. Ukiwa na malengo ya kujiendeleza zaidi na kuujuwa vizuri ulimwengu ni lazima uwe Dar maana ndo kiini cha nchi yetu.
  Kuna watu wako mikoani na wanaonekana kuwa ni watu maarufu na matajiri wakija Dar hujiona wako nyuma sana hasa wakikutana na wenzao waliosoma pamoja jinsi walivyopiga hatua kubwa kimaendeleo.

  Ila naunga mkono hoja ya kwamba kwa mtu mwenye mshahara mdogo na asiyekuwa na marupurupu mengine na asiyekuwa na mpango wa kujiendeleza zaidi mikoani kunamfaa zaidi
   
 15. faithful

  faithful JF-Expert Member

  #15
  Sep 4, 2010
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 375
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mkoani kumefanya maisha yangu yamekuwa bomba sana.........na hadi leo marafiki zangu wengi niliosoma nao vyuoni wapo tu mitaani dar wanatafuta kazi hawataki kuishi mikoani.....ni mizinga tu kila wakipiga simu au ukikutana nao dar hadi nawakwepa...kazi nzuri kibao mikoani tena zinalipa ile mbaya.....tatizo la watu wa dar wanawaona wenzao wanaofanyia mikoani washamba......kumbe maisha ni popote.
   
 16. faithful

  faithful JF-Expert Member

  #16
  Sep 4, 2010
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 375
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mimi sitanii wala sibishani na wewe inategemea hao unaowajua ila mimi nikija dar marafiki zangu wote wananitafuta na mizinga kibao.
   
 17. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #17
  Sep 4, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Sikubaliani na sipendi picha baadhai ya watu humu ndani wanayo taka kupaka kuwa mtu mwenye akili tu ndiye anayeishi Dar na wote ambao wameridhika kimaisha ndiyo wanaoishi mikoani. Kuna watu wengi tu wana kaa mikoani na wana maisha mazuri na kuna wengi tu wanaoishi Dar na maisha yao hayana maendeleo yoyote. Ni ulimbukeni huu huu ambao mwanzo watu walikua nao wa kuassume kwamba mtu anayeishi nje ya nchi (haswa nchi za Marekani na Ulaya) kwamba ndiyo wana maendeleo zaidi.

  Ukweli ni kwamba watu wengi wanaoishi Dar ni ving'ang'anizi. They have nothing going on for them over there but wana hiari kusota Dar kuliko kuondoka kwa sababu wakienda vijijini kwao wanaweza kudanganya watu wana mafanikio. Dar hali ya maisha ni haili exaggerated. Mtu anaona ni bora awe masikini lakini azunguukwe na vitu vizuri ambavyo hata hivyo hana uwezo wa kivifaidi. Ni mentality ile ile ya watu wanaoo zamia Ulaya na wana hiari wawe masikini huko ila wazunguukwe na magorofa makubwa na barabara nzuri kuliko kuishi nyumbani.


  Mkuu Mazingira ukisema watu walioridhika na maisha yao una taka kusema wewe hapo ulipo unaamini kabisa kwamba una maisha mazuri na uwezo mkubwa kuliko idadi kubwa ya watu waishio mikoani? Kuhusu vijana je unajua kwamba kuna vijana wameajiriwa mikoani na makampuni makubwa na wanalipwa mamilioni kwa mwezi? Je utasema wao wameshindwa kimaendeleo na wenzao wa Dar? Na ukisema matajiri wanaoishi mikoani wakija Dar wanajiona hawana kitu je mfano mtu kama Abood wa Morogoro akija Dar una taka kusema ataonekana masikini?

  Mimi siishi mikoani ila nadhani watu wanaokaa Dar nao wana tatizo la ego na kutaka kuji choresha kuwa wanaishi maisha bora kuliko Watanzania wengi ambao wapo nje ya jiji la Dar. Mafanikio ni popote pale. Kuna watu wanaishi mikoa yenye wingi wa dhahabu na almasi na wameweza kutake advantage of it. Kuna watu wanaishi mikoa inayo pakana na maziwa na wameweza kutake advantage of it. Oppprtunities zipo kila mahari. Nawashauri tu watu wa Dar waache ulimbukeni. Dar is not that different from other parts of Tanzania. Ni kwa sababu tu serikali ipo Dar hivyo kuna influx ya hela na projects mbali mbali zinazo toa nadharia kwamba Dar ipo juu sana,. Ukweli ni kwamba wanao faidika na kutake opportunities za Dar ni wachache sana na wengi waliobaki wanashangaa tu mataa.
   
 18. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #18
  Sep 4, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Dar ina watu milioni mbili na ushee hivi. Hawajiulizi ni wangapi kati ya hao unaweza kusema wana mafanikio. Dar ni city centre tu lakini ime zunguukwa na sehemu kibao the like of Manzese, Mwananyamala, Keko etc. Ni wachache wanafaidi na wengine wote wakiona nyumba na magari za hao wanaofaidi na wao wanajiona wapo juu. Tatizo bado watu wengi wanaona Tanzania ni Dar tu. Baadhi ya watu wengine humu utakuta hawaja wahi kuishi mikoani. Binafsi sijawahi kuishi mikoani ila naona maisha ya hata baadhi ya ndugu tu ambao wapo mikoa kama Arusha etc.
   
 19. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #19
  Sep 4, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Kwanza inategemea unzungumzia mkoa gani, Kwa mfano mkoa wa Kigoma ni tofauti na Arusha, au mkoa wa Lindi ni tofauti na Mbeya. na hata kama unaishi dar es salaam inategemea unaishi Dar ipi, uwanja wa fisi ni tofauti na masaki, au Mbezi ni tofauti na mbagala. Vilevile inategemea unafanya kazi gani, kama ni mpagazi huwezi kuifeel Dar na kuienjoy kama fisadi. Kama ni mama ntilie huwezi kuifaidi Dar kama anavyoifaidi mwenye baa.

  Ni kweli Dar kuna opportunities nyingi za Kazi, lakini hii haina maana kuwa mikoani hazipo kabisa.

  Nina rafiki zangu wanaishi Arusha, Moshi, Mwanza na Mbeya kila siku wanasema walichukua uamuzi wa maana kuchagua kuishi mikoani. Kwanza uswahili na mambo ya ujinga ujinga ni chini sana ikilinganishwa na Dar, na ustaarabu(civility) mikoani ipo juu zaidi. Na wengi wamejijenga kiais kwamba hawataki kusikia kuhusu kuhamia Dar.

  Hata kiafya ukiangalia watu wa mikoa hiyo mwenyewe nakubali kuwa wanakula chakula cha maana japo wao si matajiri, tofauti na Dar kwa watu wa kawaida chakula ni mgogoro, wakila chips na bia 2 basi wanaona chakula cha maana sana. Wengine wanafurahi kusikia tu wanaishi Capital city like life yao ni worse kuliko hata ile ya mkoani, wakati miwngine ni much worse.

  Kwa hiyo kufanya kazi au kuishi mahali fulani, kuna factors nyingi sana.
   
Loading...