Fixed Point
JF-Expert Member
- Sep 30, 2009
- 11,304
- 12,753
Asante sana Kongosho, kumbe sipo peke yangu.Mie nawaongoza kwa kiasi.
Ila lazima nipige asubuhi na jioni
Na lazima nikumbushe usafi as if naondoka na mifagio
Ila lazima nikumbushe watoto walale mapema ili wasisumbue kuamka asubuhi kwenda shule
Kuhusu wamepika nini huwa siulizi, sijui kwa nini.
wadada wenyewe na siku hizi si unawajua? hata uwawekee ratiba nini cha kufanya siku hiyo bado watataka uwakumbushe, na usipofanya hivyo utakoma na roho yakoFP, inaonekana hupendi ku-delegate sana.
wakati mwingine ni vizuri kuledegate ili upate muda wako
Asante MAMMAMIA. hayo ya kumtunza baba vizuri sitaki kuyajua. Nadhani kiuhalisia, ninaposafiri nyumba huwa namwachia baba, dada wa kazi atabaki kuwa msaidizi tu. sasa nilikuwa nawaza labda akina baba watatuambia, wanadhani tunapofanya hivi ni kwamba hatuamini kama wanaweza kuendesha nyumba kama sisi?Hii ni dalili ya kuwa unajali sana nyumba yako, hasa ikiwa una watoto. Pia inaonesha nyumbani unaye msaidizi. Ikiwa anatekeleza majukumu yake na unaridhika, hupati malalamiko toka kwa watoto na mume wako/mwenzako, sioni kama kuna tatizo kwa upande mmoja. Kwa upande wa pili, tatizo linaweza kuwepo kwa kwa huyo unayemkabidhi majukumu - Ni dada wa kukusaida kazi tu au ni jamaa yako? Ikiwa ni dada wa kukusaidia kazi, je, pia "Anamtunza" baba vizuri?
In red unafanya vizuri, ukichunguza ni sawa na kutafuta na atafutaye hupata, hata ikiwa halipo atalibuni. Kuhusu kuachiwa majukumu siwezi kusema mengi kwani nimepata fursa chache, lakini ninapoachiwa huwa ninapokea maagizo kwa kila jambo na silalamiki kwa kuelekezwa au kukumbushwa. Pengine katika 10, japo moja atakuwa amefanya vyema kunikumbusha.Asante MAMMAMIA. hayo ya kumtunza baba vizuri sitaki kuyajua. Nadhani kiuhalisia, ninaposafiri nyumba huwa namwachia baba, dada wa kazi atabaki kuwa msaidizi tu. sasa nilikuwa nawaza labda akina baba watatuambia, wanadhani tunapofanya hivi ni kwamba hatuamini kama wanaweza kuendesha nyumba kama sisi?
safi sana kama haiwakeri, maana mimi nilidhani sijui anajisikiaje? ni kama naona yeye hawezi kufanya ninavyotaka mimi!In red unafanya vizuri, ukichunguza ni sawa na kutafuta na atafutaye hupata, hata ikiwa halipo atalibuni. Kuhusu kuachiwa majukumu siwezi kusema mengi kwani nimepata fursa chache, lakini ninapoachiwa huwa ninapokea maagizo kwa kila jambo na silalamiki kwa kuelekezwa au kukumbushwa. Pengine katika 10, japo moja atakuwa amefanya vyema kunikumbusha.
Nahisi wamama wengi wako kama wewe - wanatumia remort ili kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa.
Dena Amsi kumbe haya mambo yapo kila nyumba! mara nyingi watoto afya zina-shake sana mama akisafiri, wadada wengi hawajali milo ya watoto, na ukizingatia watoto wetu wa siku hizi kula mpaka umuimbie, nani atafanya kazi hiyo mara 5 kwa siku!Kumbe tuko wengi eeehhhh........
Mie naona yangu ni mengi kuliko yako maana huwa nauliza
watoto anekula chakula chote ulichomuwekea, kashiba, kanywa
maji, kaoga, mpeleke akalale..............Na mengine meeengii
@
Kongosho sio kudeligate hatuwezi nafikiri unajua wasichana
wetu usipowasukuma aahhh mtoto atalala bila kula na akimuamsha
mara moja mbili haamki yeye anampeleka kitandani kulala hajali kivile......
Cha muhimu ni kuwa ikiwa kila kitu kinafanywa "in a good faith", bila gubu wala malalamiko yasiyo ya lazima, kuelekezana na kuelewana, kila kitu kinakwenda smooth.safi sana kama haiwakeri, maana mimi nilidhani sijui anajisikiaje? ni kama naona yeye hawezi kufanya ninavyotaka mimi!
na ndo hivyo, tunafanya in a good faith, si vinginevyoCha muhimu ni kuwa ikiwa kila kitu kinafanywa "in a good faith", bila gubu wala malalamiko yasiyo ya lazima, kuelekezana na kuelewana, kila kitu kinakwenda smooth.
dah,jf inatufunza mengi. nimepata mwanga hata mie ambaye cjaingia ndoani. AM PROUD TO BE JF MEMBER
Kongosho, huyo dada basi ujue na yeye alikuwa anapenda msosi. sasa wadada wetu wa siku hizi, wenyewe wanasema wanafanya diet, kwa hiyo msosi haupikwi nyumbani, watoto ni mwendo wa viporo tu mchana kutwaDena Amsi, wakati bado wadogo nilibahatisha dada mzuri kwa kulisha watoto.
Alikuwa anajua kiasi chao ila ratiba ndo ilikuwa inampiga chenga hadi kukumbusha wape sasa hivi.
Ila sasa vitu vingine alikuwa mmmh, saidia siku ziende
Nitakufundisha mwenyewe sitaki kungwi........tena makungwi wenyewe akina Kongosho..sitaki