Kuendeleza mali za baba, kikwazo ni msimamizi wa mirathi

davie123

Member
Mar 28, 2015
32
4
Wana JF habari za majukumu.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 29, Kwa mara ya kwanza naweka uzi huu humu jamvini!

Miaka 17 iliyopita baba yangu alifariki na kutuacha mimi na mdogo wangu wa kike ambaye tunachangia baba ingawa mama wa mdogo wangu ni mama yangu pia kwani alinilea kwa upendo na malezi yote kama mama kwa kuwa mama yangu mzazi alishatangulia nikiwa mdogo kati ya umri wa miaka 4~5.

Nikiwa mimi na mdogo wangu wa kike pamoja na mama yetu palitokea changamoto kubwa ya kimaisha hasa baada ya baba yetu kufariki. Mama yangu mlezi ni mfanyakazi ktk taasisi moja hapo DSM mpaka leo na alikuwa tayari anilee ingawa ndugu waliingilia kati kwa kuwa hakunizaa...basi mama hakuwa na jinsi.

Baada ya kumaliza msiba mama aliwasilisha wosia ulioachwa na baba na aliainisha mali zake alizoacha ingawa ndugu wa baba hawakuwa tayari kukubaliana na wosia.

Mahakama ilimteua baba mkubwa kusimamia mirathi na tangia hapo nyumba aliyojenga baba tulitoka nikawa naishi kwa baba mkubwa msimamiz wa mirathi ingawa nilikuwa mdogo darasa la 5 nafsi yangu ilipenda kuishi kwa mama...pesa za mirathi zilizotoka zilisaidia na kwa kuwa niliamini urithi pekee ni elimu nilikaza buti na nilifaulu azania.

ingawa nilipata shule nyingine private japo ada ilikuwa kubwa bb mkubwa kwa wakati huo hakuwa na kazi kwani shirika lao lilitaifishwa hivyo kiasi cha pesa za mirathi kilinisogeza na kufikia form 3 pesa ziliisha na kilichonisaidia ni kufanya vzr darasani na mpaka namaliza form 4 sikulipa ada.

Nyumba yetu ipo eneo abalo limepimwa lakini hati ilikuwa bado baba hakuipata ilikuwa ktk process na kilichokuwepo ni offer peke yake. Tulipokuwa tunajitambua na kujitegemea nikaomba baba atupe ridhaa ua kusimamia mali kwa maana ya nyumba na shamba lililopo Kigamboni eneo la mradi wa mji mpya.

Kiukweli ktk maisha yangu yote mzee (msimamizi) hakuwahi kunihusisha chochote mpaka mwisho nikawa mwenyewe naenda shamba kwa kuibia ili nisipasahau...uzuri eneo la shamba wananifahamu na ilikuwa rahisi kutembea.

Nikiwa form 5 NILISTAAJABU KUONA MTU AMEJENGA NDANI YA ENEO LETU...niliporudi kumuuliza bb akikuwa mkali kiasi akanitamkia maneno ambayo sipendi kuyaandika humu. All in all najua aliuza seheni ya shamba na hapo ndipo Msaada wa kisheria napouhitaji nina BARUA ya mauziano ya shamva ingawa baba hajui ila mama na mdogo wngu ndio wanajua.

Nianzie wapi maana nahitaji kuendeleza sehemu hii kwasasa niko nje ya dsm niba kazi serikalini na uzuri nyumba ipo mikononi mwetu tumepangisha. Nahitaji kupata Umiliki wa kimaandishi yaani hati miliki Ila kikwanzo msimamizi HATAKI. Msaada wa kisheria je tunaweza kupewa Mamlaka kamili ya mali zetu kutoka mahakamani kwani sisi mahakama haitutambui na yeye bado ameshikilia mali.

Binafsi nina mali zangu kwa ajili ya watoto wangu na naimani baba yetu hakuwa mjinga kuandika wosia ndio maana alituandika watoto wake...nafuatilia mali hii isipotee.

:confused::confused:
Wadau msaada wa mawazo Poleni kwa uzi mrefu.
 
nijuavo msimamizi wa mirathi ni mwangalizi was Mali ya marehemu na sio mmiliki,sheria inamlazimu kutenda kulingana na wosia,huyo bamkubwa aliteuliwa kusimamia hizo Mali kutokana na nyie kuwa wadogo,alihitajika kuzikabidhikwenu baada ya kuwa wakubwa,cha kufanya kachunguze kama aliweza Kurile inventory na final accounts kuhusiana na hiyo mirathi kama sheria inavomtaka,pia kama kuna matumizi yoyote ya Mali iloachwa kwa manufaa yake,ikiwa hakutimiza jukumu la kwanza au alifanya hilo la pili nenda ukaombe utenguzi wa uteuzi wa babayako mkubwa(application for revocation of grant of probate) katika mahakama ilomteua huku mkiomba uteuzi mpya ambapo mtagawana vizuri huku mkizingatia kurudisha mrejesho ktk hiyo mahakama kwa kudisplay inventory na final accounts,baada ya hapo mwaweza kwenda kwa msajili wa ardhi na nyumba kufanya maombi ya kubadilisha hizo title ukiambatanisha uthibitisho wa mahakama kama warithi halali mliopewa Mali kupitia wosia. soma hapa patakusaidia.
http://www.saflii.org/tz/cases/TZHC/2006/37.html
 
Back
Top Bottom