Companero
Platinum Member
- Jul 12, 2008
- 5,604
- 1,704
- Thread starter
- #41
Mpaka sasa sijapata hard copy ya kitabu cha Dk. Malima Bundara nimesoma excerpts tu. Lakini kwa mahojiano yake na radio Butihama, inaonyesha sources alizotumia kujibu maswali yake, hazikuwa na majibu ya kutosha.
Siku zote historia inaandikwa na washindi. Hivyo ukichukua sources za washindi hili uandike historia yako, kutakuwa na mashaka na kile unachoeleza.
Katika pitapita zangu nilipata sources zilizoandikwa wakati Northen Europe ikiwa gizani. Na kwa kutumia source hizo na vilevile ancient and medieval jiografia, naweza kusema kuwa maendeleo yamo vidoleni mwetu. Kinachoshindakana mpaka sasa ni kutoitumia population yetu na vilevile kuwa na wasomi, viongozi na wahisani wanao-undermine uwezo wa mtanzania wa kawaida (mlalahoi).
Na yale uliotaja katika posti yako moja kuhusu watu kupata chakula cha kutosha hili wawe na wakati kutosha wa kufanya shughuli zingine ni moja ya vitu vya mwanzo katika kuleta maendeleo na vitu vingine vilivyobakia ni commentary tu. Hilo ndilo hitimisho langu. Na ulini-surpise kuja na hile solution.
Hicho kitabu ninacho hapa mbele yangu. Vyanzo vyake ni mchanganyiko - kuna picha alizopiga kwenye nchi tofauti, takwimu alizokusanya kutoka katika ripoti za ndani na nje ya Afrika (mf. Black Think Tank, The South Commission & Africa Events) na pia humo kuna rejea anazozijadili kutoka kwa Waafrika/Weusi kama Justinian Rweyemamu, Walter Rodney, Olesegun Obasanjo, Yoweri Museveni, Ali Mazrui, Nelson Mandela, Frantz Fanon, Frederick Douglas, Musamali Nangoli, Chinweuzu na Mwalimu Nyerere.
Dibaji ya kitabu hicho imeandikwa na Pius Msekwa na nukuu za kukitambulisha kwa wasomaji zinatoka kwa Profesa Samuel Wangwe, Prof. William Matuja na Marehemu Prof. Cuthbert Omari.
Nukuu za maneno ya Mhandisi Malima Bundara mwenyewe ambazo nilizipigia mstari wakati nakisoma ni pamoja na hizi:
"Mwandishi huyu anaamini kwamba mpaka sasa siyo historia wala elimu ya uchumi wa sayansi ya jamii inayotosheleza kuelezea kudidimia kwa maendeleo ya Afrika na Waafrika wenyewe. Pamoja na kukubaliana na mchango wa utumwa, ukoloni na mengineyo, mwandishi anaamini kwamba maendeleo ya bara la Afrika yanadidimizwa na Waafrika wenyewe kwa sababu ya kiwango cha fikra-jumuiya cha wengi wao ni cha chini mno. Imani hii inatokana na uzoefu wa mwandishi uliothibitishwa na utafiti wake kuhusu kiini cha maendeleo duni barani Afrika. Utafiti wake ulichukua zaidi ya miaka saba katika nchi 16 za bara la Afrika. Kwa maneno mengine bara la Afrika halitaweza kuendelea iwapo Waafrika hawataongeza kiwango chao cha fikra-jumuiya kufikia angalau moja."
"Inawezekana kwamba baadhi ya watu na hasa Waafrika watauona uchambuzi huu kama matusi ya ubaguzi wa rangi kwa Mwafrika. Pamoja na kuwahurumia wote wanaofikiria hivyo, mwandishi anaomba ieleweke kwamba yeye binafsi anakerwa sana na kuendelea kunyanyaswa kwa Waafrika kokote ulimwenguni na hata katika nchi zao. Kwa mawazo yake, uchambuzi huu unalenga katika kumnasua Mwafrika kutoka kwenye fikra potofu za kuendelea kulaumu historia au kuamini kwamba bara la Afrika litaendelezwa kwa misaada na watu kutoka Ulaya na kwingineko."
Huo ndio utangulizi wake sasa sijui nikusaidiaje ukipate ila nachoweza kufanya humu ni kutoka muhtasari wangu wa kitabu hicho na kukuwekea baadhi ya dondoo ambazo nadhani ndio msingi mkuu wa hoja zake.