Kuelekea Ujamaa Mamboleo - Toward Neo-Socialism | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuelekea Ujamaa Mamboleo - Toward Neo-Socialism

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Companero, Jun 16, 2009.

 1. Companero

  Companero Platinum Member

  #1
  Jun 16, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  A specter is haunting Tanzania. The Specter of African Socialism. Workers and Peasants of Tanzania Unite.

  Mzuka unaindama Tanzania. Ni Mzuka wa Usoshalisti wa Kiafrika. Wafanyakazi na Wakulima wa Tanzania Unganeni.

  It is now a fact of life that Neoliberal Capitalism has committed suicide. JK's Stimulus Package attest to this. There is an ideological vacuum.

  Ni jambo la uhakika katika maisha yetu kuwa Ubebari wa Kinioliberali umejiuwa wenyewe. Mpango wa JK wa Kuzindua Uchumi unadhihirisha hilo. Sasa kuna Ombwe la Kiitikadi.

  But Nature abhors Vacuum. So, what will fill this Vacuum? In fact what is filling this Vacuum?

  Lakini Asili huchukia Ombwe. Hivyo, ni nini kitaliziba Ombwe hili? Kiusahihi zaidi, ni nini kinaliziba Ombwe hili?


  It is Neo-Socialism!


  Ni Ujamaa Mamboleo!
   
  Last edited: Jun 20, 2009
 2. Companero

  Companero Platinum Member

  #2
  Jun 16, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hatimaye makabrasha muhimu ya Itikadi ya Ujamaa yamepatikana. Makabrasha haya yaliyochapishwa Mwaka 1973 yanaelezea kwa kina Msingi wa Ujamaa Mkongwe ambao unaweza kutumika Kujenga Ujamaa Mamboleo.

  Mkusanyiko wa makabrasha haya upo katika Kijitabu cha UJAMAA NI IMANI: MOYO KABLA YA SILAHA kilochotungwa na Muasisisi wa Ujamaa Mkongwe, Mwalimu Julius K. Nyerere, na kuchapishwa na EAPH. Kauli Mbiu ya Kijitabu hicho ni dondoo hii kutoka katika AZIMIO LA ARUSHA:

  Lakini Ujamaa hauwezi Kujijenga wenyewe; kwani Ujamaa ni Imani hauna budi kujengwa na watu wanaoamini na kufuata kanuni zake.

  Imani hii ni nini hasa na inakuzwaje katika muktadha wa Ujamaa Mamboleo?
   
 3. Companero

  Companero Platinum Member

  #3
  Jun 16, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  NGUZO TANO ZA UJAMAA - KWA MUJIBU WA MHUBIRI MKUU WA IMANI HIYO

  1. WATU WOTE NI SAWA
  "...Kama hukubali hilo, yaani kama unadhani watu wengine ni miungu wengine, malaika, wengine nusu-nyani, basi hukubali ujamaa. Ujamaa kwako hauna maana, kwa sababu ujamaa unahusu usawa wa watu: hapo ndipo unapoanza...Sisemi usawa wa urefu wala ufupi; kwa urefu namzidi Kawawa, sana tena. Sisemi maguvu, hata; nasema utu, watu, na ubinadamu wao. Kuna binadamu zaidi ya mwenziwe? Kama huliamini hilo, utakuwa mjamaa? Hilo la kwanza...mkaliulize-ulize, mlielewe maana yake. Na mtu anayepinga ujamaa naye ajiulize kama anapinga hilo nalo. Mtu mpingaji ujamaa aseme, 'Hilo nalo, usawa wa watu, napinga; kwamba binadamu wote hivi si sawa'" - Mwalimu Julius K. Nyerere

  2. LAZIMA MTU AFANYE KAZI
  "...Binadamu hao unaotuona hapa, na hao waliosambaa dunia nzima wanaishi kwa kazi. Hawana namna nyingine ya kuishi. Wakiacha kufanya kazi watakufa; hawana namna nyingine; kuishi kwao, na kuendelea kuishi, lazima wafanye kazi...Lakini binadamu haishi kama farasi. Binadamu haridhiki kuishi kama farasi au punda; binadamu ana kitu anakiita maendeleo; lazima aendelee...Wakati mwingine ili kusudi maendeleo haya yaje wana shughuli za kupigana misasa akili, wanapanuana mawazo tu, nayo ni kazi...nendeni mkaulizane...kama kazi si kitu cha lazima, kama binadamu anaweza kujikalia tu hafanyi kazi, akaishi, na maendeleo yakaja bila kazi. Na huyo anayepinga ujamaa naye ajiulize kama hilo analipinga? Na hilo la kufanya kazi analipinga au kuna jingine analopinga?" - Julius K. Nyerere

  3. HAKUNA MTU KUMNYONYA MTU
  "...Kama binadamu ni sawa, tunalikubali hilo...Pili tunasema kitu kazi ni jambo la lazima kwa kila mtu, hakuna aliyesamehewa kazi. Basi siwezi kukufanyia kazi. Kukufanyia kazi maana yake ni kwamba wewe unasamehewa kazi! Siwezi kukufanyia kazi. Wewe utafanya kazi, na mimi nitafanya. Sio mimi nifanye, wewe hufanyi; lazima ufanye kazi. Kwa hiyo wewe utafanya kazi, na mimi nitafanya kazi; kila mtu atafanya kazi. Yaani namna ya kulitamka hilo ni kwamba kunyonyana hakuna. Hakuna mtu kumnyonya mtu; sasa tena msingi wa kumnyonya unatoka wapi? Tumesema watu sawa; na mtu ili aishi hana budi afanya kazi, na kazi ndio msingi wa maendeleo. Sasa mwanachama...ajiulize kama anaweza kuwa mjamaa na huku ananyonya! Unamnyonya mkeo; mkeo anakwenda kufanya kazi wewe unakwenda kupiga chibuku; hivi kweli mjamaa wewe? Tunasema kazi jambo la lazima, lakini wewe hufanyi kazi, unamnyonya mkeo. Wewe mjamaa? Nasema na hilo mjiulize...Unaweza kuwa mjamaa na huku unanyonya? Na anayepinga ujamaa ajiulize hilo nalo analipinga, kwamba yeye anaona kunyonya ni sawa tu! Sawa yeye kunyonya mwingine au wengine kumnyonya yeye, huyu anayesema kunyonya ni sawa. Kama kunyonya ni sawa baba, sasa tuanze kunyonya, au mkuki kwa nguruwe?" - Julius K. Nyerere

  4. VYOMBO MUHIMU VIMILIKIWE PAMOJA
  "...Kama watu ni sawa; binadamu wote ni sawa; kazi ni jambo la lazima kabisa; kunyonya ni haramu; la nne linafuata: Vyombo vyote vya lazima, vinavyohitajika kwa maisha ya binadamu kwa kufanyia kazi lazima vimilikiwe kwa jumla. Ardhi lazima imilikiwe kwa jumla maana tusipoimiliki ardhi kwa jumla tutamwachia Rashidi Kawawa na Sheikh Karume wao wawe ndio wenye ardhi, na ardhi ni kitu cha lazima kwa maisha, hebu tuone kwanza usawa utakuwaje. Itakuwa lazima twende kwa Rashidi na kwa Karume, 'tafadhali bwana nataka ardhi'. Umekwishamwita 'Bwana' huyu; usawa umekwisha. Lakini vilevile kama Sheikh Kawawa ana ardhi, na Sheikh Karume ana ardhi, hawa hawalazimiki kufanya kazi. Kwa nini wafanye kazi? Hawawezi kufanya kazi. Tumesema kazi ni kitu cha lazima kwa kila mtu, lakini hawa hawawezi kufanya kazi, watakaa tu wanatutoza kodi kwa ardhi yao. Ndiyo wanatunyonya hivyo tena. Mimi nafanya kazi; mimi nalima. Halafu Rashidi anasema, 'Ukishalima mahindi ukapata magunia matano, moja langu'. Ndio ananyonya hivyo. Anavunja kanuni ya usawa; anavunja kanuni ya kazi; anavunja kanuni ya kutonyonya. Kwa nini? Kwa sababu tumemruhusu amiliki yeye vitu ambavyo vinastahili viwe vya wote. Mtu ambaye yeye ana ardhi; umemkabidhi viwanda, ukishakuwa umemkabidhi majambo mengine haya, umemwongezea nguvu zake, yeye utu wake umeongezeka-ongezeka na wangu mimi umeupunguza-punguza. Kwa hiyo vitu vilivyo vya lazima kwa kila mtu, kama ardhi ambayo ni ya lazima kwa kila mtu, lazima vimilikiwe na wote. Sasa...mjiulize kama unaweza kuwa mjamaa kweli huku unajidai ardhi yangu? Na wanaopinga wanatakaje? Hao wanaosema ujamaa mbaya. 'Eti vitu vyote viwe vya ujumla'; wengine waongo, 'Eti wanasema hata wakina mama wawe wa jumla'. Tunasema ardhi, hatusemi kina mama, tunasema ardhi viwanda, madini: kwa nini mtu mmoja anakwenda kuvinyakua vikawa vyake hivi!" - Julius K. Nyerere

  5. KUUNDA NCHI BILA MATABAKA
  "..Kama tunakubali kuwa watu wote ni sawa; na watu wote ni lazima wafanye kazi, mtu asimnyonye mtu; na mali, mali kubwa, sikusema shati langu liwe la Rashidi: misingi ya uchumi kama mabasi yale yanapita iwe kwamba tunasema mabasi yetu, asiweko mheshimiwa mmoja pale anasema 'Basi langu lile!' Basi lako! Yupo dereva mle anaendesha, anasema dereva wake! 'Dereva wangu' - dereva wako, wewe unaweza kuwa na dereva? Dereva anaweza kuwa dereva wa umma, sio dereva wako. Dereva ni sawa sawa na mwalimu; mwalimu wa umma, daktari wa umma, dereva wa umma. Huyu anakuwaje 'wako'? Hata askari siku moja utasema wako. Kama tunakubali watu wote ni sawa; watu wote lazima wafanye kazi, hakuna kunyonyana; mali,vitu vyote vile vya jumla lazima viwe vya umma; maana yake ndio kusema tunataka kuunda nchi ambayo haina tabaka: hakuna mabwana na watwana." - Julius K. Nyerere

  NUKUU ZOTE ZIMETOKA KWENYE UJAMAA NI IMANI: MOYO KABLA YA SILAHA (1973)
   
 4. Offish

  Offish Senior Member

  #4
  Jun 16, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 172
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Respect Mkuu, global economic meltdown in ishara tosha kuwa upepari umeshindwa na kulegea kabisa na kwamba unahitajika mfumo mpya uibuliwe ukiwa umejikita katika nguzo hizo. Ni juu ya miamba hiyo tu dunia yenye neema ya kweli yawezekana...
   
 5. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #5
  Jun 16, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180

  Mkuu. Nyerere alikuwa mlalaheri na wewe mlalahai. Afu mnatufundisha walalahoi kuhusu usawa.
   
 6. Companero

  Companero Platinum Member

  #6
  Jun 16, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Naam huo mfumo 'mpya' ndio huo wa Ujamaa Mamboleo ambao utaifanyia marekebisho kidogo hiyo nguzo ya nne na ya tano ili ile rasilimali kuu tu kama ardhi, misitu na madini ndio zimilikiwe kwa umoja/ujumla na zile za kawaida kama viwanda na kadhalika ziweze kumilikiwa na sekta binafsi katika soko linalodhibitiwa kwa wastani na wananchi wenyewe kupitia vyombo vya kidemokrasia. Wengine wanauiita mfumo huu 'uchumi mchanganyiko'. Hilo ndilo lilokuwa wazo la mwanzo la Mwalimu Nyerere kabla hajachanganya madesa ya ubepari wa dola na usoshalisti wa chama kushika hatamu.
   
 7. SYLLOGIST!

  SYLLOGIST! JF-Expert Member

  #7
  Jun 16, 2009
  Joined: Dec 28, 2007
  Messages: 306
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45
  Hako ka "Rabbit" sasa!

  Tembo bado anakula nyasi yake...
   
 8. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #8
  Jun 16, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Hivi kwanini Nyerere alihamua kuchukua usoshalisti au ubepari wa dola?
   
 9. Companero

  Companero Platinum Member

  #9
  Jun 16, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Syllo safari ya maili elfu moja inaanzia na maili moja na umoja ni nguvu - visungura vitamwangusha tembo tu mbona kashaanza kuweweseka au huoni hivyo vifurushi vya kuchochea uchumi vinavyotupwa kiholela?

  Zaku Mwalimu aliamua kukumbatia Ubepari wa Dola na Uhodhi wa Chama kutokana na kuchanganya madesa kwa kudhani Dola/Chama = Umma/Wananchi ndio maana baadaye alikiri kuwa alifanya makosa - Rejea tena na tena ukubali wake wa kosa hilo hapa chini na ushauri wake kuhusu mfumo mbadala:

  There are things that I would have done more firmly or not at all. For example, I would not nationalize the sisal plantations. This was a mistake. I did not realize how difficult it would be for the state to manage agriculture. Agriculture is difficult to socialize. I tried to tell my government that what was traditionally the family's in the village social organization should be left with the family, while what was new could be communalized at the village level.

  Ndugu uzoefu huu ndio tunauhitaji sisi walalahai na ndugu zetu walalahoi dhidi ya wanyonyaji walalaheri ili turekebishe makosa hayo na kuleta Ujamaa Mamboleo wenye mchanganyiko wa umiliki wa umma na umiliki binafsi wenye uwiano/mizania unaoleta usawa na kuzuia matabaka ya mabwana na watwana.
   
 10. SYLLOGIST!

  SYLLOGIST! JF-Expert Member

  #10
  Jun 16, 2009
  Joined: Dec 28, 2007
  Messages: 306
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45
  Siasa za itikadi zaishia ukingoni hazina mpenyo kwenye siasa mbadala na jamii za sasa. Hata siku moja ikitokea kukiwa na Usawa basi-Kuna Usawa.
  Hatungeweza kushabikia dini kama hakuna maovu-au hakungekuwepo na dini bila ya maovu kuwepo...vilevile inavyoeleweka hakuna itikadi hapa duniani ambayo imeweza kupunguza hayo manung'uniko hapo juu-'uwiano' 'usawa' na matabaka ya mabwana na watwana. Only in Heaven na huko nasikia Mkuu wake yupo!:(

  Huu Ujamaa wa mambo ya leo ndio hayo hayo...shika lwako au ujiunge na Chama Cha Mwenyewe mwenyewe tu.
   
 11. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #11
  Jun 16, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Companero:

  Kuna mchumi mmoja Marekani alitoa nadharia yake kuhusu kukua kwa uchumi. Katika nadharia hii anasema kuwa ongezeko la machinery liko direct proportion na ongezeko la uchumi. Hivyo nchi ikiweza kuongeza idadi za machines, basi itaongeza idadi ya industrial output ambayo in turn itaongeza kukua kwa uchumi.

  Coincidently WaRusi (Soviet Union) walifanya mageuzi ya kiuchumi kwa kutumia nadharia ya ongezeko la machines.

  Tukirudi kwa mchumi wa Marekani, nadharia yake aliitoa kipindi cha great depression kwa kuzingatia kwamba wananchi wengi walikuwa idle. Na yeye hakuangalia nchi za dunia ya tatu. Na application ya nadharia yake ilikuwa kwa nchi zilizoendelea. Miaka 10 baadaye alikubali mapungufu ya nadharia hii.

  Pamoja na mapungufu ya nadharia, World Bank ilitumia kama nadharia za mwanzo za kuleta maendeleo katika nchi masikini. Na kwa sababu nchi hizi zilikuwa na walalahoi wengi, iliaminika kuwa ni serikali ndio yenye uwezo wa kuleta maendeleo ya uchumi kama vile Urusi ilivyofanya.

  Kwa mfano: katika miaka ya 70, inaonyesha kuwa kulikuwa na ongezeko la machinery nchi Tanzania. Lakini wakati huo huo industrial productivity per worker ili-decrease kwa zaidi ya mara tatu kwa mwaka.

  Sasa mkuu naomba unieleze huo Ujamaa wako mpya unashindana vipi na nadharia za wahisani wetu kama World Bank
   
 12. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #12
  Jun 16, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,586
  Likes Received: 1,953
  Trophy Points: 280
  Philosophy ya mwalimu kuhusu "Binadamu wote ni sawa" Ili base kwenye mahitaji muhimu ya mwanadamu,kuwa ni food,shelter and clothes,kwamba bottom line wanadamu wote wanahitaji pa kula,pa kulala na mavazi ya kujisetiri,mambo ambayo bado ni anasa kwa baadhi ya maeneo nchini mwetu.Nadhani ndiyo dhana halisi ya kila binadamu nisawa plae mwalimu alipoona kuwa kuna wanadamu wengine wanachukuliwa kama ni less of a human being. Kwenye kusema kila mtu ni sawa ni upotoshaji,ila wanadamu ni sawa kwenye mahitaji kuhimu ili kuweza kuwa a descent human being.
   
 13. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #13
  Jun 16, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Kwa nini unaiita falsafa yake (Mwalimu)? Kwani yeye ndiye aliyeianzisha?
   
 14. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #14
  Jun 16, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Uchokozi....kama Dilunga...
   
 15. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #15
  Jun 16, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Unalo jibu?
   
 16. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #16
  Jun 16, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,586
  Likes Received: 1,953
  Trophy Points: 280
  Dunno! Hapo chini ni basics za mjadala huu,kama una la kuongezea ama kurekebisha basi you're welcome,just go ahead...Hata hivyo hapo kwenye "Watu" nadhani ilikuwa ikisema binadam,Companero ataweza kutuelewasha. Binafsi sijui tofauti haswa ya hizo 2 terminologies "watu vs binadamu" as to whether they provide us with axcatly the same menings or not. I think mostly is where, when and how they are used.  So Nyani Nizo nguzo tau za ujamaa zi za nani huyo muhubiri mkuu?
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  Jun 16, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Dunno! Mimi nimekuuliza wewe swali na hujalijibu. Jibu swali langu Mangi
   
 18. Companero

  Companero Platinum Member

  #18
  Jun 16, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hilo ongezeko la mashine lilitokana na nadharia za uchumi za Import Substitution Industrialization (ISI) ambazo tulizivaa kichwa kichwa na sio hizo nadharia zako za Benki ya Dunia iliyokuwa ikimwaga fedha kwenye miradi mikubwa ya Kidola iliyoweka Umma pembezoni.

  Tulichotakiwa ni kuangalia uhusiano kati ya mapinduzi ya kilimo na mapinduzi ya viwanda hasa nadharia 'Lewisian Turning Point' ambayo aliiongelea Mkaribiani Arthur Lewis kuhusu namna ya kuingia kwenye sekta ya Viwanda bila kuathiri uzalishaji wa Sekta ya Kilimo.

  Mimi hapa kwenye Ujamaa Mamboleo naongelea mchanganyiko wa nadharia za Uchumi wa Kiimla na Uchumi Huria yaani 'Uchumi Mchanganyiko' unaohakikisha kuwa tunawapa uhuru Umma kuzalisha bila kuingiliwa sana na Dola ilhali Dola inasimamia 'Mali ya Taifa' kama Madini.
   
 19. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #19
  Jun 16, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,586
  Likes Received: 1,953
  Trophy Points: 280
  Elimu yetu sisi tz tuliambiwa mwalimu ndo alisema hayo,kwa binadamu wote ni sawa,sasa wewe kama kuna mtu mwingine ambaye una uhakika ndiye mwanzilishi wa filosofia hiyo,then kwanini usiseme tu badala ya kuuliza nonsense? Sasa ni swali gani hilo hujajibiwa,umeuliza kama ni mwalimu,nikasema zimeletwa nguzo tano za ujamaa hapa na Companero,sasa nini huelewi kuhusu mwalimu na ujamaa na filosofia yake ya Binadamu wote ni sawa? Ama?
   
 20. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #20
  Jun 16, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Sasa bwana Mangi baada ya kupata elimu zaidi huko ughaibuni bado unaamini kwa Mwalimu ndiye mwanzilishi wa hiyo falsafa?

  Halafu acha ghadhabu Mangi. Tunajadiliana tu hapa. Hatushindani, okay?
   
Loading...