Kuelekea Uchaguzi wa 2015, Amina Chifupa atimiza miaka nane tangu afariki 26/06/2007

DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,837
1,674

AMINA CHIFUPA ATIMIZA MIAKA NANE 26/06/2007

Nyerere alinipiga POINT OF ORDER kwenye kikao cha NEC Halmashauri Kuu Ya Taifa Kilichofanyika WHITE HOUSE DODOMA tukiwa kwenye mjadala wa NEC kama huu ulofanyika kati ya tarehe 6/07/2015 na tarehe 11/07/2015.

Napenda kuyaeleza haya kwa kuwa ni muhimu sana katika kipindi hiki ambapo Nchi yote ipo mikononi mwa Halmashauri Kuu Ya Taifa.Nina maana kuvunjika kwa Nchi kuko mikononi mwa maadili ya CCM Taifa,Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa, Halmashauri Kuu ya Taifa na Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM.
Mazungumzo yalikuwa kama ifuatvyo:-
Mwenyekiti wa kikao kipindi hicho mwaka 1995 alikuwa ni Rais wa awamu ya Pili Alhaji Alli Hassan Mwinyi baada ya kujieleza wagombea wote 17 waliowania Urais mwaka 1995 na mjadala ukaanza .Niliinua mkono na kuanza kuzungumza.

CHIFUPA:

''Mheshimiwa, mimi naomba kutoa mapendekezo, napendekeza majina yote 17 ya waombaji wa Urais tuletewe yote tuyapigie kura kuyachuja sisi wajumbe wa NEC.''

MWALIMU NYERERE:

Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwa kikaoni kwa haraka akasimam. ''Mwenyekiti POINT OF ORDER huyu Katibu anatupotosha yeye anawajuaje wagombea wote 17 undani wao na kila mtu, Kamati kuu ndio inayojua wagombea wote na undani wao,ningependekeza majina yote yaende Kamati Kuu kasha wao ndio watuletee majina Sita [6 ] tuu kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa''.

CHIFUPA

Mimi nilipigwa na butwaa na kukaa kimya ,baadae niligundua kuwa ni kweli kumjua kila mtu na undani wake sisi wajumbe wa NEC ni vigumu sana kumjua mtu undani wake,Sasa ningependa nieleze kuwa Wananchi ni vigumu kujua undani wa mtu.Unaweza kumuona mtu anatembea amevaa tai,mwingine kanzu, mwingine suruali na mwingine kaptura lakini kujua undani wake ni kazi ya vyombo vya Dola.

CHAKUWAMA:
Leo nimekuja Chakuwama kuleta nguo za Duka la Amina Chifupa ambalo tumekaa nalo miaka nane [8] iliyopita.

Foundation ya Amina Chifupa ilitegemea kupata mafanikio bega kwa bega na mama mlezi wa kikundi hiki.Nachukua nafasi hii kumpongeza mama mlezi kwa kazi ngumu anayoipata ya kuwalea watoto yatima walioko katika nyumba hii.
Alinisimulia jinsi Amina Chifupa alivyokuwa akisomesha watoto 30 kwa kuwalipia shilingi 30,000/= kwa mwezi jumla y ash 900,00/= kwa mwezi, na jinsi Amina alivyomletea Shs milioni 3 kwa ajili ya kusaidia malezi ya watoto hao, na baada ya kufa Amina Chifupa yote ya kusomesha watoto yalisitishwa.

Mimi niliposimuliwa wote tulitokwa na machozi kwa kuwa kufa kwake shujaa wetu AMINA CHIFUPA watoto hao wapatwa na msiba mara mbili, wa kukatishwa masomo na pia kufa kwake.
Ningependa mama wa Chakuwama kwa moyo wake wa kuendeleza kuwahudumia watoto hawa na hatuna cha kumlipa Mungu mwenyewe ndio anayejua na ndiye ataye kulipa.Ningetoa mwito kwa wenye moyo kuanzisha kikundi kama hiki cha Chakuwama na kuvisaidia vingine vilivyopo Nchini Foundation ya Amina Chifupa Ikianza kazi itahirikiana na kikundi hiki na vingnevyo vilivyopo nchini kwa kuwa Katiba ya Foundation ina eleza hivyo.
JINA LA MAJI YA AMINA CHIFUPA SPRING WATER
Jina la maji ya Amina Chifupa Spring Water lina badilishwa na kuwa hii ni taarifa rasmi kama kuna wenye mapendekezo ya jina pia tutawaomba wafanye hivyo tumebadilisha jina kwa kuliita Lyanjo Spring Water Lupembe Kwa kuwa Amina mwenywewe akiwa motto wa miaka 5 alimuomba Babu yake Chifupa Solomon Mkalimoto Mpagama Mbanga kuwa Babu mimi nikifa uje unizike hapa akionyesha mahali tulipomzika kwa wosia wake hapa kijijini IYANJO LUPEMBE NJOMBE.
Na ndio maana kuanzia sasa tunabadilisha jina na kukipa kinywaji hicho jina la Kijiji hicho ambacho ni makao makuu ya Chief Solomon.

AMINA CHIFUPA FOUNDATION:
Foundation ya Amina imepitia misukosuko mingi sana katika jisni ya kupata fedha kwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania MHE.JAKAYA MSRISHO KIKWETE alituahidi kutuchangia Foundation yetu hiyo ya AMINA CHIFUPA FOUNDATION tunachukua nafasi hii kumuomba kukumbusha Rais wetu ahadi aliyotupatia kuwa atatusaidia ili FOUNDATION iweze kutekeleza majukumu yake ya kusaidia wale wanaoishi katika mazingira magumu, yatima n.k

Tunaomba Rais aaikumbe ahadi yake atusaidie ikiwa itashindikana sasa kwa sababu ya majukumu mazito aliyonayo Kitaifa basi msaada huo wa maombi yetu hayo atusaidie kuufikisha kwa Rias ajaye. Lakini ingependeza zaidi Rais akasikia ombi hilo nasi AMINA FOUNDATION tukapata nguvu ya machango wake huo ili kuweza kutimiza ndoto na maonoa ya Mwanaccm na Shujaa wa vijana Marehemu Amina Chifupa.
Tunamomba Rais wetu mwenye moyo wa huruma aweke roho yake hiyo ya huruma kwa jicho la karibu kwenye Foundation hiyo.

Source :
LT H.G. CHIFUPA
Katibu Mkuu AMINA CHIFUPA FOUNDATION
04/07/2015
Phone:+255 754 004 884/ +255 784 785 506

 
Back
Top Bottom