Kuelekea siku ya wanawake: Wajue wanawake 8 Magangwe waliobadili historia ya dunia

SONGOKA

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
1,843
1,841
Karne hii imekuwa vigumu sana kuamini kuwa dunia hii tunayoishi kwa sasa historia yake yote ni matokea ya wanawake. Wanawake wa sasa wamekuwa rahisi rahisi, ombaomba, na legelege kinyume na historia na asili ya mwanamke.

Kwa kuwa tunaelekea katika siku ya wanawake, naomba kuwakumbusha wanawake magangwee waliobadili kabisa mwenendo na historia ya dunia hii. Na hapa sizungumzii ugunduzi tu lakini nazungumzia historia, mwenendo, na mtazamo wa watu duniani kotee

1. Eve/Eva

Huyu ndo mwanamke wa shoka kuliko yeyote duniani na ndo aliyesababisha haya yanayotokea duniani yawepo. Kwanza Eve ndo sababu ya binadamu wote kuanza kuvaa nguo. Baada ya kula tunda lililokatazwa aligundua yuko uchi, na biblia haijaandika alitumia siku ngapi kutafakari kabla ya kumpa Adam, labda kila siku alikua anamshangaa Adam yuko uchi bila Adam kujua na akampa baada ya wiki, mwezi mwaka, biblia haijasema.

Lakini huyu mama wa shoka ndo mwanamke wa kwanza kuzaa mtoto, na kuanzisha uzazi katika dunia hii, lakini pia ndo binadamu wa kwanza kumuona na kuongea na shetani. Bila Eva pasingekuwa na makanisa ya kina Gwajima na wapendwa wengine wanaojikita katika kutoa mapepo. Huyu Eva ni mama gangwee na kabambee , aliposikia eti ukila tunda unakuwa kama Mungu akaona isiwe taabu akala fasta (what an opportunist)

2. Maria mama wa Yesu

Huyu ni mwanamke haswaa, mtaratibu kwelikweli na kupitia yeye dunia nzima leo inapiga goti kwa kristo. Maria akiwa binti mdogo tena bikira alipata ujauzito, ikumbukwe wakati huo kulikuwa na waganga kwelikweli tena wataalamu haswa, lakini hakuona umuhimu wa kwenda kupigiwa ramli, wala kuzunguka kwa mabesti zake kuwasimulia yale maajabu, alitulia na kujifungua Jesus.

Bila mwanamke huyu yote yanayomuhusu Yesu na Yosefu pengine yasingeandikwa. Huyu kabadili kabisa muelekeo wa dunia katika ibada kupitia kwa mwanaye Yesu kristo.
Si wewe leo ukiwa na mimba na hujui ya nani kutokana na kurukaruka kwako basi utamsingizia kila mtu na mwishowe kuishia kuitoa...whaat kuitoa, acheni kabisaaa

3. Hagar

Huyu alikua kijakazi tu lakini ndo mwanzo wa waarabu na fujo zao. Mwanamama huyu alitimuliwa na Sarah kutokana na wivu wa mapenzi na akatembea jangwani kwa siku kadhaa bila kuchoka huku akiwa amembeba mwanaye Ishmael, narudia alitembe jangwani kwa siku kadhaa. Siku hizi wadada wanatupa watoto vyooni wakati wana kila kitu kinawazunguka. Bila huyu mama waarabu tusingewajua, lakini pia uislam pengine usingekuwepo, kwasababu ni ukoo mwa Ishmael ulioendelea na kuja wakina Mohammed Mtume. Mwanamke wa shoka huyu, alivuka jangwa na kwenda kuanzisha historia katika ardhi ya ukame, Bila huyu mama Hija mngeziskia tu!

4. Delilah

Wengi mtashangaa kwa nini huyu mama nimuweke katika list. Huyu ndo mwanamke wa shoka aliyeleta dhana ya honey pot duniani, yaani kutumia wadada warembo kama spies au wapelelezi. Baada ya mataifa kwa mataifa kumshindwa Samsoni, baunsa mbabe wa Kiisraeli mwenye kila mbinu za kivita, ilibidi majemedari waumize vichwa. Hapo ndo wazo la kigori mpelelezi lilipokuja na wanawake kibao walikataa kwa hofu ya kuuawa na samsoni. Lakini kwa mara ya kwanza katika historia Agent Delilah alikubali na akaingia kazini na kuifanikisha hii kazi kwa mafanikio makubwa. Kuanzia hapo taaluma ya upelelezi wa kimapenzi ikazaliwa

5. Queen of Shebah

Huyu mwanamama alibadili kabisa historia ya dunia. Kwanza kupitia yeye mpaka sasa kuna vizazi kadhaa wanaamini Ethiopia ndo mji mtakatifu. Lakini pia malkia ndo mwanamama pekee wa kiafrica aliyefanikiwa kuiunganisha Africa na ukoo wa Daudi ambao ni ukoo wa Yesu. Inaaminika alizaa na Suleimani ambaye alikua mwana mpendwa wa Daudi. Na kimsingi Yesu kristo alizaliwa kutika ukoo wa Daudi, hivyo kupitia mwana mama huyu tuna uhakika kuwa huku Africa kuna raia wana DNA au vinasaba sawasawa na Yesu Kristo.

5. Cleopatra

Mwanamama hatarii na aliyebadili angani historia ya dunia hii kuliko hata gia za angani za siasa za bongo. Bila mwana mama huyu pengine mpaka sasa dunia ingekuwa chini ya dola la Kiroma (the great Roman empire). Wakati dola la kiroma likiwa katika peak na likitawala dunia nzima mwana mama Cleopatra alitumia mbinu za Delilah kumrubuni kaisar Julius, The great Julius Ceasar na kuwa mpenzi wake.

Kwa utamu wa penzi Julius alihamia Egypt na kuliacha dola lake kwa muda mrefu, hii ilisababisha Waroma kuchukia na kupanga mapinduzi yaliyopelekea kuuawa kwa Julius. Hata hivyo baada ya kufa Julius Mwanamama akahamishia penzi kwa mkuu wa majeshi wa Roman Empire, General Mark Antony. Akamchanganya kiasi cha kumhamishia katika jeshi lake la Egypt yeye na kikosi cha Roma na kwa pamoja wakaivamia Roma iliyokuwa chini ya bwana mdogo Octavian mpwa wa Julius.

Ingawa walishindwa vita na wote kujiua, lakini ndo ukawa mwisho wa Roman empire sababu wanajeshi watiifu wa Mark Antoni waliendelea vita ya ndani kwa ndani na octavian hivyo kusababisha dora la kirumi kuanguka na ustaarabu wao kutoweka. Ikumbukwe mataifa na wanaume kibao walishindwa kuiangusha dola hii lakini mwana mama Cleo alifanya yake

6. Queen Nzinga

Unamuachaje Nzinga katika historia ya dunia hii na mabadiliko ya kiutawala. Mwanamama huyu wa Angola katika dola la Ruanda ndo mwanamke pekee duniani kupigana vita kwa muda mrefu zaidi. Alipigana vita na wareno kwa miaka 30 mfululizo.

Wapi kina mama ambao mkipigwa na maisha kwa mwezi mmoja tu mnajiuza kweupeee. Nziga mwanamke wa shoka huyu alisimama na mzungu kwenye battle mpaka mzungu akaomba reinforcement Ulaya

Mwanamama huyu alibadilisha kabisa aina ya utawala wa Wareno kutoka katika ule wa kibabe kwenda katika ASSIMILATION. What a woman

7. Sara Breedlove

Huyu ni kibokooo, wakati mnadhani Oprah ni tajiri basi mentor wake ni Sara. Huyu ndo mwanamke wa kwanza duniani tena mwafrica kuwa self made Millionaire. Ukiacha utajiri wa kurithi wa kina malkia, Sara alijitengenezea utajiri mwenyewe kuanzia from scratch.

Alibadili kabisa historia ya dunia kwa kuwafanya kina mama kuanza kuamini kuwa kumbe utajiri si lazima usubili mmewako afe ili urithi. Wapi kina mama wajasiriamali.

8. Wanawake waliogundua bia

Kama hutaki acha, ila historia inasema kuwa bia iligunduliwa na mwanamke. Ingawa rekodi hazikufanikiwa kumtaja au kuwataja majina, lakini ni ukweli kwamba beer iligunduliwa na wanawake. Kwa wale mnaoshinda viti virefu alafu mnaenda kuwafanyia fujo wake zenu mjue mnawabugudhi wagunduzi wa kitu muhimu

Hii imebadilije historia ya dunia, kama hujui na hili basi kapange nyumba KIBITI

Natambua wapo wanawake weliofanya mambo makubwa lakini hayakubadili historia ya dunia bali yali compliment tu, Margareth Thatcher, Ellen Johnson, Terresa, Wangali, Mwanamakuka, Mary Magdalena, etc

Kina dada na kina mama naomba niishie hapo. Dunia hii ni ya kwenu acheni nyimbo za haki sawa, nyie mnazo nyingi kuliko hata wanaume. Wakati sisi tunashangaa wanyama pale Eden tayari mwakilishi wenu Eva alikua katika safari ya kutaka kuwa kama Mungu.
 
Story za kufikirika ambazo sioni kama zina uhalisia.. Story kama hzi ndiyo zinazo sababisha tushindwe kufika kwenye Tanzania ya viwanda..
 
Mwongo ww. Binadamu alimuiga nyani kunywa pombe. So mgunduzi wa bia ni nyani/sokwe/ngedere wao porini walikula matunda yaliyooza wakalewa
 
Ungetakiwa uongeze kikundi cha wanawake waitwao 'mke' hichi kikundi ni noma humu duniani
 
Hao ndo wenyewe achana na hawa wanaoshindana na sisi kuvaa surual ili tuwe sawa eti, tunaweza kuwa sawa kwa kuvaa salawili?? Hahahaha
 
Back
Top Bottom