Kuelekea mechi ya VPL: Simba SC na Mtibwa Sugar. Itakuwa mechi kali kuwahi kutokea VPL

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Kuelekea mechi ya VPL' Kikosi cha Simba SC, leo Jumapili ya February 9, 2020 kimewasili salama mkoani Morogoro kikitokea jijini Dar es salaam wakiwa tayari kuwakabili Mtibwa Sugar, Jumanne ya February 11, 2020 kwenye uwanja wa Jamhuri Stadium katika mfululizo wa ligi kuu Tanzania, Vodacom Premier League (VPL).

Achilia mbali Dar Derby, Simba SC, na Mtibwa Sugar, mchezo huu unatarajiwa kuwa mkali sana kuliko michezo mingine iliyocheza kwenye VPL kwa msimu huu, kwasababu kusaka alama tatu muhimu ili kuweza kujiimarisha kwenye msimamo na kurudisha furaha kwa Viongozi, mashabiki pamoja na,wanachama wa timu hizi hasa baada ya kupoteza michezo yao ya mwisho ya VPL, ambapo Simba SC alikubali kipigo cha 1-0 dhidi ya JKT Tanzania huku Mtibwa Sugar Akicharagwa 1-0 dhidi ya Lipuli FC.

Kocha Sven Vanderbroeck ameanza kuonja joto la mashabiki na wanachama huku mabosi wake wakimwambia kuwa hawataki kuona timu yao inapata matokeo mabaya zaidi, huku Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingiza akipenyeza kuwa hatma ya kocha Vanderbroeck ipo chini ya Bodi ya Wakurugenzi chini ya Mwenyekiti Mohammed Dewji Mo huku akiongeza kwa kuwataka mashabiki na wanachama kutulia kwani viongozi wanafanyia kazi kuona timu inafikia mafanikio yenye furaha.

Mashabiki Mtibwa Sugar wamelitaka bechi la ufundi na wachezaji kujiuliza kulikoni? kwa mwenendo mbaya wa kupoteza mechi tatu mfululizo kwenye VPL, wakipoteza dhidi ya Yanga, Ruvu Shooting, na Lipuli FC, hivyo kuwataka kujitathimini upya na kukusanya nguvu kuanzia mchezo dhidi ya Simba na michezo mingine, vinginevyo klabu yao itakuwa na wakati mgumu kujinasua kwenye mstari wa kushuka daraja kutokana na matokeo mabaya yanayoendelea kuyapata.

Itakuwa mechi kali kuwahi kutokea VPL, usikose ukaambiwa!

IMG_20200209_171234_913.jpeg
IMG_20200209_171253_827.jpeg
 
Chagizo lingine la kuifanya hii mechi iwe kali ni Simba kutaka kulipa kisasi cha kufungwa na Mtibwa Mapinduzi Cup. Simba hawatokubali kufungwa mara ya pili huku Mtibwa Sugar walitaka kuonyesha kua hawakubahatisha kuifunga Simba mara ya kwanza.
 
Amecheza Simba, Azam wakaona hana jipya wakapiga chini, sasa anataka asajiliwe na hao ni wale wale akina Ally Ally
Nami namuona. Mara avae jezi za yanga mara hiki....
Simba palimshindwa. Na azam pia! Acha abahatishe kwa yanga maana siku hizi simba ndio kama recruitment assessment ya yanga. Mtu alikaza dhidi ya simba wanataka mchukua!
 
Nami namuona. Mara avae jezi za yanga mara hiki....
Simba palimshindwa. Na azam pia! Acha abahatishe kwa yanga maana siku hizi simba ndio kama recruitment assessment ya yanga. Mtu alikaza dhidi ya simba wanataka mchukua!
Exactly mkuu..!
 
Hakuna sababu iwe ni hali ya uwanja, mvua, jua au waamuzi wa mchezo kesho haipaswi kuwa sababu. Ni ushindi pekee ndio tunahitaji na tuna kazi ya kuhakikisha tunafanikisha hilo.”.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simba Vs Mtibwa iwe hivi
1. Manula
Kakolanya ana mkosi wa kufungwa kila mechi.
2.Kapombe
3.M.Hussein (tshabalala)
4.Mlipili
5.Wawa
6.Mkude
7.Dilunga
8.Fraga
9.Kagere
10.Chama
11. Kanda



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom