Kuelekea mechi ya VPL: Simba SC na Mtibwa Sugar. Itakuwa mechi kali kuwahi kutokea VPL

huyo mlipili sahau, atapangwa yule tall mbrazil anaekimbia kama anasukumwa kisa umri, Simba tumefeli sana!

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakumbuka Mechi na Pilisi Moshi.

Huyo Babu alipigwa chenga ya kuzunguka akadondoka na hakuamka tena Hadi Goli ninafungwa. Straika akampenyezea mfungaji kulia kuna beki Mzee Kennedi, kushoto kuna beki Mzee Shamte, forward akaipress katikati wakawa wanamsindikiza tu kwa macho miguu inagoma, mfungaji akaweka kambani.

Ukingalia lile Goli hakika utagundua tofauti ya kuwa na wachezaji vijana na wazee.

Tatizo la Simba Sports Club ni kujaza

"WACHEZAJI WENGI WAZEE"

(Julio)



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo Vitoroli FC Leo mnapigwa, mark my word. Tukutane jioni SAA 12.30
 
Kuelekea mechi ya VPL' Kikosi cha Simba SC, leo Jumapili ya February 9, 2020 kimewasili salama mkoani Morogoro kikitokea jijini Dar es salaam wakiwa tayari kuwakabili Mtibwa Sugar, Jumanne ya February 11, 2020 kwenye uwanja wa Jamhuri Stadium katika mfululizo wa ligi kuu Tanzania, Vodacom Premier League (VPL).

Achilia mbali Dar Derby, Simba SC, na Mtibwa Sugar, mchezo huu unatarajiwa kuwa mkali sana kuliko michezo mingine iliyocheza kwenye VPL kwa msimu huu, kwasababu kusaka alama tatu muhimu ili kuweza kujiimarisha kwenye msimamo na kurudisha furaha kwa Viongozi, mashabiki pamoja na,wanachama wa timu hizi hasa baada ya kupoteza michezo yao ya mwisho ya VPL, ambapo Simba SC alikubali kipigo cha 1-0 dhidi ya JKT Tanzania huku Mtibwa Sugar Akicharagwa 1-0 dhidi ya Lipuli FC.

Kocha Sven Vanderbroeck ameanza kuonja joto la mashabiki na wanachama huku mabosi wake wakimwambia kuwa hawataki kuona timu yao inapata matokeo mabaya zaidi, huku Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingiza akipenyeza kuwa hatma ya kocha Vanderbroeck ipo chini ya Bodi ya Wakurugenzi chini ya Mwenyekiti Mohammed Dewji Mo huku akiongeza kwa kuwataka mashabiki na wanachama kutulia kwani viongozi wanafanyia kazi kuona timu inafikia mafanikio yenye furaha.

Mashabiki Mtibwa Sugar wamelitaka bechi la ufundi na wachezaji kujiuliza kulikoni? kwa mwenendo mbaya wa kupoteza mechi tatu mfululizo kwenye VPL, wakipoteza dhidi ya Yanga, Ruvu Shooting, na Lipuli FC, hivyo kuwataka kujitathimini upya na kukusanya nguvu kuanzia mchezo dhidi ya Simba na michezo mingine, vinginevyo klabu yao itakuwa na wakati mgumu kujinasua kwenye mstari wa kushuka daraja kutokana na matokeo mabaya yanayoendelea kuyapata.

Itakuwa mechi kali kuwahi kutokea VPL, usikose ukaambiwa!

leo wanacheza dada mtu na shangazi yake--tutarajie mauno ya kufa mtu.
 
Hii ndio First 11 ya Simba ninayoijua Mimi hata tukifungwa nitaamini ni matokeo ya mpira Kishingo bana Bocco na Kagera wanatakiwa kuanza pamoja siku zote Boya wewe.
 
Back
Top Bottom