Kuelekea hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, AS Vita Club dhidi ya Simba SC, Injinia Ngapi?

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Kuelekea hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika, baada ya kuwakwaruza vilivyo JS Saoura ya Algeria, kwa mikwaruzo mitatu bila majibu, DOZI Kimataifa kuendelea.

..Mwana Kulitaka Mwana Kulipewa

Mabingwa wa Nchi ya Tanzania, Simba SC, Kesho Jumamosi Januari 19' 2019 watakuwa ugenini Kinshasa DRC kukipiga na AS Vita Club katika mechi ya kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika, mchezo ambao unatarajiwa kuwa ni mkali na wakusisimua katika dakika zote 90 za mchezo.

Mkuu wa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, De la boss amesema timu imejipanga na wanakwenda kuhahikisha wanapata matokeo mazuri kwa ajili ya Nchi na maslahi ya Simba SC.

..Mfumba Jicho MK 14 Meddie Kagere

Akiwa amecheka na vyavu mara 5 Ligi ya Mabingwa Afrika, na kuwa kinara kwa ufungaji, Meddie Kagere MK 14, Mfumba Jicho ataongoza safu ya ushambuliaji ya Simba SC kuhakikisha mabeki wa AS Vita Club wanakuwa na Tandabelua kwa muda wote wa mchezo.

..Nahodha wa Simba SC John Bocco!

Simba itamkosa nahodha wake John Rafael Bocco kutokana na kusumbuliwa na majeraha aliyoyapata katika mchezo dhidi ya JS Saoura

Kumbuka mchezo huu utashuhudia LIVE na ZBC 2 kuanzia saa moja kamili usiku..!

Kutoka Kiembesamaki, Zanzibar kwa niaba ya JFSimba..ni Ghazwat nakuambia Usikose Ukaambiwa.
FB_IMG_15477940913714458.jpeg
IMG_20190118_095431_066.jpeg


Kikosi cha Simba kikifanya mazoezi ya mwisho Jana jioni, tayari kuwakabili AS Vita Club katika uwanja wa Stade des Martyrs DRC

IMG_20190118_100323_197.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom