Kuelekea AU Summit,Tanzania Iongoze Afrika kutaka Mageuzi ICC na Sio Kujitoa

Ben Saanane

JF-Expert Member
Jan 18, 2007
14,581
18,124
Mageuzi yanahitajika Mahakama ya Kimataifa
http://www.raiamwema.co.tz/mwandishi/mwandishi-wetu
Na Ben Saanane

Toleo la 454

RAIS wa Kenya ametangaza rasmi kuwa nchi yake haitashirikiana na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) baada ya Makamu wake, William Ruto, kunusurika, na mahakama hiyo kudai kuwa mashahahidi walitishwa. Waltet Barasa na Mwanasheria Paul Gicheru na Philip Kipkoech Bett wanatuhumiwa na ICC kuwa walihonga na kuwatisha mashahidi wa kesi ya Ruto, hivyo wanaitaka Kenya iwakabidhi kwa mahakama hiyo.

Binafsi naipongeza Serikali ya Tanzania kuweka msimamo wa kutojitoa ICC. Mwaka jana nilionya kuhusu uwezekano wa Umoja wa Afrika (AU) kujitoa katika Mkataba wa Roma ulioanzisha mahakama hiyo ya kimataifa inayoshughulikia uhalifu wa kivita, jinai dhidi ya binadamu na mauaji ya kimbari (genocide). Mahakama hii kwa sasa ni adui mkubwa mbele ya macho ya viongozi wahalifu, sio wa Afrika pekee bali hata kwingineko.
Hoja kuu ni kuwa mahakama hii inawalenga viongozi kutoka mataifa ya Afrika tu. Hii ni hoja yenye ukweli kwa kiasi fulani. Hata hivyo, viongozi wa Afrika nao wana ajenda yao juu ya mpango wao wa kutaka kujitoa ICC.

Nchi 34 kati ya 54 za Umoja wa Afrika zimesaini Mkataba wa Roma wa kukubali kuanzishwa kwa Mahakama hii. Wakati viongozi wa nchi hizo waliposaini haraka haraka mkataba wa ICC na kuziingiza nchi zao walidhani wanazuia mapinduzi dhidi yao kutoka kwa waasi, na walikwenda hatua mbele zaidi ya kujifanya kuwa hawatatambua matumizi ya mtutu katika kubadilisha utawala kwa njia ya kupindua serikali.

Hawakufikiria wala kutilia maanani kuwa ili kukomesha mapinduzi ya kijeshi ni lazima kuimarisha utawala bora wa sheria bila kuminya demokrasia, ili sauti huru zisikike na pia kujali zaidi maslahi ya wananchi wa nchi hizo. Mapinduzi ya kijeshi Afrika yanachochewa kwa kiwango kikubwa na tawala kandamizi zilizominya uhuru wa maoni na kuzuia sauti za wananchi wenye mawazo kinzani pamoja na wanaharakati.

Jambo la kufurahisha ni kuwa wapo viongozi zaidi ya 12 wa nchi za Afrika waliopo madarakani na ambao ni wanachama wa AU walioingia madarakani kwa mtutu wa bunduki na wengine wakibaki madarakani kwa kupora chaguzi. Kipindi wanapitisha azimio la kutotambua mapinduzi ya kijeshi, idadi hii ilikua kubwa zaidi na hao hao walioingia madarakani kijeshi au kwa wizi wa kura ndiyo waliotangaza kutotambua mapinduzi hayo ya kijeshi.

Kwa mujibu wa maandishi ya vitabu vya kitafiti kuhusu Mapinduzi ya Kijeshi katika nchi za Kiafrika kama Coup D'Etat' cha mwandishi Edward Luttwak na Political Order In Changing' kilichoandikwa na Samuel P. Huntngton, ilionekana kuwa pamoja na ushawishi kutoka mataifa ya nje lakini upendeleo, ufisadi na hali ngumu ya kiuchumi na kijamii ni mojawapo ya vichocheo vikubwa kwa mapinduzi ya kijeshi yaliyoikumba Afrika.

Kwa kipindi cha karibia miaka 60 tangu nchi za Kiafrika zipate Uhuru, Afrika imeshudia mapinduzi ya kijeshi zaidi ya 40 huku nchi ya Nigeria ikiongoza kwa kukumbwa na mapinduzi 10 ya kijeshi kati ya mwaka 1966-1999 ikifuatiwa na Ghana iliyokumbwa na zaidi ya mapinduzi tisa ya kijeshi.

Kwa hiyo, badala ya kufikiria namna ya kuondoa sababu na vichocheo vya uwezekano wa mapinduzi ya kijeshi huko baadae, viongozi wetu hawa wa Afrika waliamua kufumba macho na kuchagua njia waliyoiona ni rahisi zaidi kwa wakati huo bila kutazama athari zake kwao pia, yaani Mkataba wa Roma wenye kuasisi Mahakama ya ICC.

Kwa mfano suala la uchaguzi kwa nchi za Afrika ni kichocheo kikubwa cha uvunjifu wa amani na mapinduzi kwa njia ya mtutu. Viongozi wa Afrika wanaogopana kuambiana ukweli au hawaheshimiani kwa kuwa tabia zao za ukiukaji wa sheria na kutowajali raia wao zinafanana.

Burundi inaangamia kwa sababu ya Pierre Nkuruzinza kupindua katiba na kung'ang'ania madaraka. Umoja wa Afrika unambembeleza. Hapa kwetu Zanzibar uchaguzi ulichafuliwa ukaitishwa uchafuzi. Busara za viongozi wa CUF chini ya Maalim Seif ndizo zilizoishikilia amani ya Zanzibar hadi sasa.

Nchini Kenya kwa mfano, wakati Mwai Kibaki, Uhuru Kenyatta na wanasiasa wengine wa kilichokuwa chama tawala cha Kenya cha PNU walipofanya udanganyifu kwenye uchaguzi wa Rais na wabunge mwaka 2007, hali iliyosababisha wapinzani kutoka chama cha ODM wakiongozwa na William Ruto na Raila Odinga kwa upande mwingine kuingia barabarani kupinga kuporwa uchaguzi huo na kusababisha mauaji ya watu zaidi ya 1,000 na wengine zaidi ya 600,000 ya wasiokuwa na hatia kukosa makazi, Umoja wa Afrika, AU haukutangaza moja kwa moja kumchukulia hatua Mwai Kibaki na watawala wengine.

Umoja huu haukutangaza kumtenga Mwai Kibaki na serikali yake na hata Rais Benjamin Mkapa wa Tanzania na Dk. Koffi Annan walipopelekwa kusuluhisha mgogoro huo walipata wakati mgumu kutoka kwa Kibaki, wakati wote huo wa vurugu za Kenya waliokuwa wanapoteza maisha ni raia wanyonge tu kutoka maeneo mbalimbali wa nchi hiyo.

Sasa swali la kujiulia ni kuwa kuna haja gani ya kufanya uchaguzi ikiwa aliyeshinda uchaguzi anaporwa ushindi? Kuna tofauti gani kati ya mapinduzi ya kijeshi (Coup d'tat) na wizi wa kura?

Unapopora haki ya raiakuchagua, unapopora haki ya raia kutoa sauti. Hayo ni mapinduzi ya matakwa ya umma (coup d'civillien). Hayo ni mapinduzi mapya baada ya coup d'tat. Viongozi wa Afrika wamelibariki hilo. Unafiki ulioje?

Mara zote mapinduzi ya aina hii yasipofanikiwa kwa asilimia kubwa husababisha vita ya wenyewe kwa wenyewe. Tulishuhudia jaribio hili kule Cot de'Ivore, Laurent Gbagbo alishindwa uchaguzi na mpinzani wake Allasaine Outtara, akaamua kufanya ‘coup de' civillien'. Afrika haikufua dafu, walitoa sauti za kinafiki kukemea na hali ilizidi kuwa mbaya na kuhatarisha amani kiasi cha kusababisha uwezekano wa kuzuka vita ya wenyewe kwa wenyewe hadi jumuiya ya kimataifa ikiongozwa na mkoloni wa zamani wa nchi hiyo, Ufaransa walipoingilia kati na hatimaye Gbagbo akakamatwa akiwa amejificha kwa aibu.
Leo anashtakiwa mbele ya Mahakama ya ICC, Mahakama hii ndiyo ambayo viongozi hawa wanataka kujitoa ili kujiepusha na haya yanayomkuta Gbagbo. Kwa hiyo, tunaona kwamba mjadala wa akina Kenyatta na viongozi wa AU na nia yao ya kujadili suala la kujiondoa ICC inalenga pia kuwalinda viongozi hawa ambao wengi wao wamekiuka haki za binadamu na pia kuua na kutesa wapinzani wao. Ni ufedhuli mtupu.

Kwa nini hawajitoi kwenye Shirika la Fedha Duniani (IMF), Benki ya Dunia (WB) na kwenye Shirika la Biashara Duniani (WTO)? Inatambulika kuwa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani ni nyenzo kuu za mabeberu zinazotumika kuzinyonya nchi zinazoendelea na hasa zile nchi zenye viongozi wasiofikiria mbele. Heri yao wananchi wa Venezuela waliojiondoa kutokana na ushupavu wa Rais wao, Kamaradi Hugo Chavez. Vyombo hivi vya mabeberu (IMF, WB na WTO) ni hatari kwa Afrika na ustawi wa wananchi wa Afrika kuliko Al-Qaeda na Al-Shaabab ambayo ni makundi hatari kwa mabeberu, vibaraka na maslahi yao popote pale duniani.

Jambo kubwa la kinafiki kutoka kwa viongozi wetu hawa ni kuwa wengi wao wa Afrika walioshitakiwa ICC walipelekwa huko na serikali za nchi zao ambazo viongozi wake walikusanyika huko mjini Addis Ababa kulalama kuwa ICC inawashtaki wao tu.

Serikali zilizopeleka kesi na watuhumiwa wenye asili ya kiafrika huko The Hague ni pamoja serikali za nchi za Jamhuri ya Afrika ya Kati, Cote d'Ivoire, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Uganda. Kesi nyingine mbili za Darfur na ile ya Libya zilipelekwa mbele ya Mahakama hiyo na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mamlaka yake zikiungwa mkono na wanachama wa baraza hilo kutoka barani Afrika.

Viongozi wa Afrika ni wabinafsi na hawawezi kuona mbele hadi hatari iwaguse wao binafsi. Si wale viongozi wa kaliba ya kina Kwame Nkrumah, Julius Nyerere, Nelson Mandela, Ahmed Sekou Toure, Thomas Sankara, Gamal Abdel Nasser, Patrice Lumumba. Viongozi tunaowaheshimu katika ujengaji wa hoja kwa maslahi ya nchi na Bara la Afrika kwa vitendo tofauti na hawa madikteta waoga.

Viongozi wa sasa wa Afrika walipotia saini Mkataba wa Roma walikuwa na akili zao timamu, waliona namna Marekani, China na Urusi ambao ni wajumbe watatu muhimu wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa walipokacha kusaini mkataba wote au hata kujiwekea sheria zao za ndani za kuzuia matumizi ya mkataba huo wa Roma kwa raia wao. Leo wanalalamika na kuhoji uhalali wa wajumbe hao wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wasioikubali ICC?

Wakati Marekani wanaimarisha taasisi za uwajibikaji kama Mahakama huku taasisi hizo hapa kwetu ni dhaifu na haziko huru. Naipongeza Serikali ya Tanzania kupitia Waziri wa Mambo ya Nje, Dk. Augustine Mahiga kwa kukubali kuwa ICC inahitajika lakini ni sharti kufanyiwa mageuzi (reforms).

Sasa natoa rai kwa Serikali ya Tanzania ipeleke mpango maalumu wa kutaka ‘reform’ ya ICC kama mbadala wa mpango maalumu wa kujitoa ulioandaliwa na Rais Uhuru Kenyatta. Kwa kufanya hivyo, tutakua tumelinda tunu tuliyoachiwa na Mwalimu Nyerere ya kujali utu, haki na wajibu wetu.

Mwandishi wa makala haya, Ben Saanane, anapatikana kwa simu 0768078523

Chanzo: Raia Mwema
 
Hiyo mahakama ya ICC huwa inatuingizia shilingi ngapi kwenye uchumi wetu hadi tung`ang`anie Tanzania kubaki humo?
 
Kwa tunakoelekea kisiasa hapa kwetu nchini, katuTanzania haiwezi kuthubutu kutia neno kuhusu mahakama hiyo! Nchi hii sasa inatawaliwa na mkono wa chuma kwa kisingizio cha kupambana na ufisadi na kutowajibika. Zanzibar inatawaliwa kijeshi na huku Tanganyika hakuna tena uongozi bali hofu na wasiwasi imewajaa wenye madaraka! Hawajui kesho itakuwaje na hata ubunifu katika akili zao umeyeyuka.

Kwa kuwa watawala wetu ni watuhumiwa watarajiwa kwa hali yo yote hawawezi kuunga mkono kuendelea kuwepo kwa mahakama hii hadharani au kifichoni!!!
 
100% true
 
Hayo mambo ya ICC tayari na waziri Mahiga alishaongelea hebu sikiliza hapa
 
Hiyo mahakama ya ICC huwa inatuingizia shilingi ngapi kwenye uchumi wetu hadi tung`ang`anie Tanzania kubaki humo?

Ndiyo sababu nakuambia wewe unafikiria kwa kutumia kinyesi!. HUNA KICHWA ILA UMFUNGIWA FURUSHI LA MAVI JUU YA SHINGO!.

Hupashwi kufungua domo wala hilo furushi lako kwa sababu halifai palipo binadamu. Huelewi nini??
 
TZ issue kubwa ni Ufisadi (si uhalifu wa kivita au genocide)...Focus yetu sasa ni kuwekeza kwenye mahakama ya mafisadi!
 
Kwa kweli ulichokiandika kinalogic kubwa sana. Waziri Mahiga ni chaguo bora kabisa alilolifanya Mheshimiwa Rais maana katika maswala haya anauzoefu mkubwa sana baada ya kukaa muda mrefu kwenye ubalozi wetu wa kudumu umoja wa mataifa. Sasa wataalamu tuano ni vema wakaandika ni reform ya namna gani ifanyike kuliko kupendekeza reform ifanyike na kukaa kimya itakuwa haina maana. Tuonyeshe kwa vitendo.
 
Ben Saanane Pengine nikuulize swali dogo, mageuzi yanayohitajika ICC ni katika eneo gani na ni yapi?

Nguruvi3,

Asante

ICC inapaswa ijipambanue vyema .Kwa mfano Azimio namba 1593 la UN Security Council lililopelekea Sudan kuwa Refered ICC lilionekana kama ni Selective Jurisdiction kama ambVyo Brazil ilivyo-abstain as a negative diplomatic gesture na kuituhumu Washington kwa kusapoti hilo

Sudan sio Signatory wa Rome statute but yet Omary Al-Bashir ana Arrest Warranty

Marekani sio Signatory lakini Bush hana Arrest warranty ya Uhalifu wa Kivita Afganistan na Iraq

Mambo haya yanasabababisha selective jurisdiction of ICC court and it's proceedings ndio maana katika mataifa 114 yalio-ratify ICC hakuna taifa la Mashariki ya kati kwenye Crisis na North Africa lililoridhia Rome Statute isipokua ufalme wa Ishmitite ndani ya Jordan

Nimejibu simple tu mkuu
 
Mageuzi yanahitajika Mahakama ya Kimataifa
Na Ben Saanane

Toleo la 454

RAIS wa Kenya ametangaza rasmi kuwa nchi yake haitashirikiana na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) baada ya Makamu wake, William Ruto, kunusurika, na mahakama hiyo kudai kuwa mashahahidi walitishwa. Waltet Barasa na Mwanasheria Paul Gicheru na Philip Kipkoech Bett wanatuhumiwa na ICC kuwa walihonga na kuwatisha mashahidi wa kesi ya Ruto, hivyo wanaitaka Kenya iwakabidhi kwa mahakama hiyo.

Binafsi naipongeza Serikali ya Tanzania kuweka msimamo wa kutojitoa ICC. Mwaka jana nilionya kuhusu uwezekano wa Umoja wa Afrika (AU) kujitoa katika Mkataba wa Roma ulioanzisha mahakama hiyo ya kimataifa inayoshughulikia uhalifu wa kivita, jinai dhidi ya binadamu na mauaji ya kimbari (genocide). Mahakama hii kwa sasa ni adui mkubwa mbele ya macho ya viongozi wahalifu, sio wa Afrika pekee bali hata kwingineko.
Hoja kuu ni kuwa mahakama hii inawalenga viongozi kutoka mataifa ya Afrika tu. Hii ni hoja yenye ukweli kwa kiasi fulani. Hata hivyo, viongozi wa Afrika nao wana ajenda yao juu ya mpango wao wa kutaka kujitoa ICC.

Nchi 34 kati ya 54 za Umoja wa Afrika zimesaini Mkataba wa Roma wa kukubali kuanzishwa kwa Mahakama hii. Wakati viongozi wa nchi hizo waliposaini haraka haraka mkataba wa ICC na kuziingiza nchi zao walidhani wanazuia mapinduzi dhidi yao kutoka kwa waasi, na walikwenda hatua mbele zaidi ya kujifanya kuwa hawatatambua matumizi ya mtutu katika kubadilisha utawala kwa njia ya kupindua serikali.

Hawakufikiria wala kutilia maanani kuwa ili kukomesha mapinduzi ya kijeshi ni lazima kuimarisha utawala bora wa sheria bila kuminya demokrasia, ili sauti huru zisikike na pia kujali zaidi maslahi ya wananchi wa nchi hizo. Mapinduzi ya kijeshi Afrika yanachochewa kwa kiwango kikubwa na tawala kandamizi zilizominya uhuru wa maoni na kuzuia sauti za wananchi wenye mawazo kinzani pamoja na wanaharakati.

Jambo la kufurahisha ni kuwa wapo viongozi zaidi ya 12 wa nchi za Afrika waliopo madarakani na ambao ni wanachama wa AU walioingia madarakani kwa mtutu wa bunduki na wengine wakibaki madarakani kwa kupora chaguzi. Kipindi wanapitisha azimio la kutotambua mapinduzi ya kijeshi, idadi hii ilikua kubwa zaidi na hao hao walioingia madarakani kijeshi au kwa wizi wa kura ndiyo waliotangaza kutotambua mapinduzi hayo ya kijeshi.

Kwa mujibu wa maandishi ya vitabu vya kitafiti kuhusu Mapinduzi ya Kijeshi katika nchi za Kiafrika kama Coup D'Etat' cha mwandishi Edward Luttwak na Political Order In Changing' kilichoandikwa na Samuel P. Huntngton, ilionekana kuwa pamoja na ushawishi kutoka mataifa ya nje lakini upendeleo, ufisadi na hali ngumu ya kiuchumi na kijamii ni mojawapo ya vichocheo vikubwa kwa mapinduzi ya kijeshi yaliyoikumba Afrika.

Kwa kipindi cha karibia miaka 60 tangu nchi za Kiafrika zipate Uhuru, Afrika imeshudia mapinduzi ya kijeshi zaidi ya 40 huku nchi ya Nigeria ikiongoza kwa kukumbwa na mapinduzi 10 ya kijeshi kati ya mwaka 1966-1999 ikifuatiwa na Ghana iliyokumbwa na zaidi ya mapinduzi tisa ya kijeshi.

Kwa hiyo, badala ya kufikiria namna ya kuondoa sababu na vichocheo vya uwezekano wa mapinduzi ya kijeshi huko baadae, viongozi wetu hawa wa Afrika waliamua kufumba macho na kuchagua njia waliyoiona ni rahisi zaidi kwa wakati huo bila kutazama athari zake kwao pia, yaani Mkataba wa Roma wenye kuasisi Mahakama ya ICC.

Kwa mfano suala la uchaguzi kwa nchi za Afrika ni kichocheo kikubwa cha uvunjifu wa amani na mapinduzi kwa njia ya mtutu. Viongozi wa Afrika wanaogopana kuambiana ukweli au hawaheshimiani kwa kuwa tabia zao za ukiukaji wa sheria na kutowajali raia wao zinafanana.

Burundi inaangamia kwa sababu ya Pierre Nkuruzinza kupindua katiba na kung'ang'ania madaraka. Umoja wa Afrika unambembeleza. Hapa kwetu Zanzibar uchaguzi ulichafuliwa ukaitishwa uchafuzi. Busara za viongozi wa CUF chini ya Maalim Seif ndizo zilizoishikilia amani ya Zanzibar hadi sasa.

Nchini Kenya kwa mfano, wakati Mwai Kibaki, Uhuru Kenyatta na wanasiasa wengine wa kilichokuwa chama tawala cha Kenya cha PNU walipofanya udanganyifu kwenye uchaguzi wa Rais na wabunge mwaka 2007, hali iliyosababisha wapinzani kutoka chama cha ODM wakiongozwa na William Ruto na Raila Odinga kwa upande mwingine kuingia barabarani kupinga kuporwa uchaguzi huo na kusababisha mauaji ya watu zaidi ya 1,000 na wengine zaidi ya 600,000 ya wasiokuwa na hatia kukosa makazi, Umoja wa Afrika, AU haukutangaza moja kwa moja kumchukulia hatua Mwai Kibaki na watawala wengine.

Umoja huu haukutangaza kumtenga Mwai Kibaki na serikali yake na hata Rais Benjamin Mkapa wa Tanzania na Dk. Koffi Annan walipopelekwa kusuluhisha mgogoro huo walipata wakati mgumu kutoka kwa Kibaki, wakati wote huo wa vurugu za Kenya waliokuwa wanapoteza maisha ni raia wanyonge tu kutoka maeneo mbalimbali wa nchi hiyo.

Sasa swali la kujiulia ni kuwa kuna haja gani ya kufanya uchaguzi ikiwa aliyeshinda uchaguzi anaporwa ushindi? Kuna tofauti gani kati ya mapinduzi ya kijeshi (Coup d'tat) na wizi wa kura?

Unapopora haki ya raiakuchagua, unapopora haki ya raia kutoa sauti. Hayo ni mapinduzi ya matakwa ya umma (coup d'civillien). Hayo ni mapinduzi mapya baada ya coup d'tat. Viongozi wa Afrika wamelibariki hilo. Unafiki ulioje?

Mara zote mapinduzi ya aina hii yasipofanikiwa kwa asilimia kubwa husababisha vita ya wenyewe kwa wenyewe. Tulishuhudia jaribio hili kule Cot de'Ivore, Laurent Gbagbo alishindwa uchaguzi na mpinzani wake Allasaine Outtara, akaamua kufanya ‘coup de' civillien'. Afrika haikufua dafu, walitoa sauti za kinafiki kukemea na hali ilizidi kuwa mbaya na kuhatarisha amani kiasi cha kusababisha uwezekano wa kuzuka vita ya wenyewe kwa wenyewe hadi jumuiya ya kimataifa ikiongozwa na mkoloni wa zamani wa nchi hiyo, Ufaransa walipoingilia kati na hatimaye Gbagbo akakamatwa akiwa amejificha kwa aibu.
Leo anashtakiwa mbele ya Mahakama ya ICC, Mahakama hii ndiyo ambayo viongozi hawa wanataka kujitoa ili kujiepusha na haya yanayomkuta Gbagbo. Kwa hiyo, tunaona kwamba mjadala wa akina Kenyatta na viongozi wa AU na nia yao ya kujadili suala la kujiondoa ICC inalenga pia kuwalinda viongozi hawa ambao wengi wao wamekiuka haki za binadamu na pia kuua na kutesa wapinzani wao. Ni ufedhuli mtupu.

Kwa nini hawajitoi kwenye Shirika la Fedha Duniani (IMF), Benki ya Dunia (WB) na kwenye Shirika la Biashara Duniani (WTO)? Inatambulika kuwa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani ni nyenzo kuu za mabeberu zinazotumika kuzinyonya nchi zinazoendelea na hasa zile nchi zenye viongozi wasiofikiria mbele. Heri yao wananchi wa Venezuela waliojiondoa kutokana na ushupavu wa Rais wao, Kamaradi Hugo Chavez. Vyombo hivi vya mabeberu (IMF, WB na WTO) ni hatari kwa Afrika na ustawi wa wananchi wa Afrika kuliko Al-Qaeda na Al-Shaabab ambayo ni makundi hatari kwa mabeberu, vibaraka na maslahi yao popote pale duniani.

Jambo kubwa la kinafiki kutoka kwa viongozi wetu hawa ni kuwa wengi wao wa Afrika walioshitakiwa ICC walipelekwa huko na serikali za nchi zao ambazo viongozi wake walikusanyika huko mjini Addis Ababa kulalama kuwa ICC inawashtaki wao tu.

Serikali zilizopeleka kesi na watuhumiwa wenye asili ya kiafrika huko The Hague ni pamoja serikali za nchi za Jamhuri ya Afrika ya Kati, Cote d'Ivoire, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Uganda. Kesi nyingine mbili za Darfur na ile ya Libya zilipelekwa mbele ya Mahakama hiyo na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mamlaka yake zikiungwa mkono na wanachama wa baraza hilo kutoka barani Afrika.

Viongozi wa Afrika ni wabinafsi na hawawezi kuona mbele hadi hatari iwaguse wao binafsi. Si wale viongozi wa kaliba ya kina Kwame Nkrumah, Julius Nyerere, Nelson Mandela, Ahmed Sekou Toure, Thomas Sankara, Gamal Abdel Nasser, Patrice Lumumba. Viongozi tunaowaheshimu katika ujengaji wa hoja kwa maslahi ya nchi na Bara la Afrika kwa vitendo tofauti na hawa madikteta waoga.

Viongozi wa sasa wa Afrika walipotia saini Mkataba wa Roma walikuwa na akili zao timamu, waliona namna Marekani, China na Urusi ambao ni wajumbe watatu muhimu wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa walipokacha kusaini mkataba wote au hata kujiwekea sheria zao za ndani za kuzuia matumizi ya mkataba huo wa Roma kwa raia wao. Leo wanalalamika na kuhoji uhalali wa wajumbe hao wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wasioikubali ICC?

Wakati Marekani wanaimarisha taasisi za uwajibikaji kama Mahakama huku taasisi hizo hapa kwetu ni dhaifu na haziko huru. Naipongeza Serikali ya Tanzania kupitia Waziri wa Mambo ya Nje, Dk. Augustine Mahiga kwa kukubali kuwa ICC inahitajika lakini ni sharti kufanyiwa mageuzi (reforms).

Sasa natoa rai kwa Serikali ya Tanzania ipeleke mpango maalumu wa kutaka ‘reform’ ya ICC kama mbadala wa mpango maalumu wa kujitoa ulioandaliwa na Rais Uhuru Kenyatta. Kwa kufanya hivyo, tutakua tumelinda tunu tuliyoachiwa na Mwalimu Nyerere ya kujali utu, haki na wajibu wetu.

Mwandishi wa makala haya, Ben Saanane, anapatikana kwa simu 0768078523

Chanzo: Raia Mwema

Vipi Mbowe unamuweka hapo kwenye Viongozi wa Kiafrika? Kwa maana hata yeye hachaguliwi,haondoleki wala hafukuziki, na wala hakuna anayejua jinsi ya kumuondoa, vipi huyo naye? Ameongoza Chama chake kwenye chaguzi tatu na ameshindwa zote lkn bado ni kiongozi Mkuu wa Chama Chake naye anaangukia hapo hapo kwa viongozi wabinafsi na walafi wa Kiafrika uliowataja?
 
Hiyo mahakama ya ICC huwa inatuingizia shilingi ngapi kwenye uchumi wetu hadi tung`ang`anie Tanzania kubaki humo?
Vitu vingine kama hauvielewi soma kisha uliza mkuu sio lazima uchangie, hauwezi kujua kila kitu mkuu, haiya ni maji marefu haulewi kwa siku moja
 
Back
Top Bottom