Kuelekea 2030 Katiba iwe ni mjadala wa kitaifa

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
KUELEKEA MWAKA 2030 KATIBA UWE NI MJADALA WA KITAIFA.

Ni mara chache sisi WanaCCM kujitokeza kuandika haya hadharani hasa Kwa kuwa misingi ya Chama chetu ni kusemana ndani. Lakini nineona hili leo niliseme hadharani ili kumuunga Mhe Rais kuendelea kulijenga Taifa.

Ninatambua Makada wengi tumechagua njia rahisi ya kupongeza sana, Lakini tumesahau hawa viongozi ni binadamu. Hivyo wanapaswa kupongezwa, kushauriwa na kuwapa mapendekezo.

Hili andiko ni maalumu sana kwa makada wenzangu wa CCM. Sisi tunadhamana kubwa ya kuijenga nchi na kuibomoa kutokana na uwingi wetu. Bahati mbaya wapo wanaodhani mazuri yanawahusu CCM na Mabaya yanawahusu Wapinzani. Ukweli ni kuwa hakuna Chama Duniani ni chama Cha kudumu hasa kwenye siasa za ushindani. Kuna wakati vyama huwa vinabadilishana utawala. Kwenye kubadilishana utawala huko ndiko kunakotakiwa kutuamusha kuwa kuelekea mwaka 2030 tunapaswa kuwa na katiba ambayo itadumisha misingi ya nchi na kuboresha Sheria zingine zinazoenda na Wakati.

Katiba ambayo hata siku tukiwa nje ya utawala bado katiba haitakuwa kikwazo kwetu. Katiba iliyopo si mbaya, lakini inahitaji maboresho makubwa kutokana na wakati tulio nao Sasa. Imetuvusha ktk mengi lakini tunapaswa kuwa na katiba nyingine itakayo tuvusha kwenye Diplomasia ya uchumi Duniani.

Wakati mwingine ni ngumu sisi makada kueleweka. Ningekuwa ninatumia maneno ya dini ningesema wengi wetu si wa moto Wala wa Baridi ni wa vugu vugu. Kwa lugha ya kidiplomasia sisi HATUFUNGAMANI NA UPANDE WOWOTE.

Imekuwa kawaida kwetu kuwa kitu tulichoshangilia na kukipigia makofi jana kikija Kwa namna nyingine leo tunakishangilia hata kama ni kinyume chake.

Leo hii nimeona wengi tunampongeza Mhe Rais Kwa maamzi mazito aliyoyafanya huko bandarini. Mimi ni sehemu ya niliyepongeza na pia kumuonea huruma Mhe Rais Kwa kazi kubwa iliyopo mbele yake hasa kupambana na hawa watengeneza madili. Lakini nimejiuliza Kwa Nini haya? Wajibu wa Bunge letu kuisimamia serikali ukoje? Namna ya Bunge kutunga Sheria upoje? Kwa nini Rais agundue uozo huu kama Bunge lipo?

Pamoja na kuwa Rais ni sehemu ya Bunge Kwa mjibu wa katiba Ibara ya 62(1) lakini bado wapo Wabunge waliotakiwa kuyaona haya na kuhoji. Bunge letu ndilo taa inayotakiwa kuwaka muda wote na kumlika kila kona.

Mimi Binafsi ninaona changamoto ya haya yote ni kuwa na Katiba itayotengeneza Sheria ya kuwa na Dira ya Taifa. Dira ambayo itakuwa road Map ya kila kiuongozi. Katiba iliyopo bado inatoa nafasi kubwa ya viongozi wakubwa kuamua mambo mengi kwa niaba yetu. Ni katiba ambayo inawapa watu wengine nguvu na kuifanya mihili mingine kuwa kama ipo ipo....

Ili kulinda legacy ya Mhe Samia ninadhani katiba kuwa na Katiba mpya itakuwa ni Jambo la mhimu na Katiba itaenda kuyalinda mazuri yote atakayofanya. Hata akitokea kiongozi mwingine, Kwa kuwa yaliyofanyika yalifanyika Kwa mjibu wa Sheria, Dira ya Taifa na ushirikushwaji basi atalazimika kuyalinda. Tunatakiwa kuwa na katiba ambayo Mafisadi hawataona mwanya wowote wa kukwapua fedha za umma.

Katiba ambayo haitajenga nia njema ya viongozi wetu wakuu kuwa daraja la madalali wa kugombanisha serikali zilizopita na Iliyopo. Katiba ambayo unapokuwa Rais hutaona hiyo nafasi ni mzigo Bali ni nafasi ya utumishi.

Katiba ambayo kila baya hataangushiwa Rais bali waliofanya uzembe. Katiba ambayo watawala na watawaliwa wataishi kwenye Sheria moja. Lakini katiba ambayo vyama vya siasa havitakuwa mahasimu bali watani kama SIMBA NA YANGA.

WanaCCM tunawajibu huu!

Elius Ndabila
0768239284
 
Sasa hivi hata Sukuma gang watasema wanataka katiba mpya. Hakika muda ni mwalimu wa kila kitu
 
Back
Top Bottom