Kuchukuliwa mke inauma

Kuchukuliwa mke inauma

Big Lion

Member
Joined
Jan 5, 2015
Posts
46
Reaction score
15
Jana jioni nimepigiwa simu na jamaa mmoja inaonekana ni mtu mzima hivi kutokana na sauti. Tukasalimiana kistaarabu tu akaniambia wewe si Bakari nimjibu sio utakua umekosea namba,but kang'ang'ania mim ni Bakari.

Akaniambia nimekupigia simu naomba uachane na mke wangu. "Nikastuka mke wako" anasema ndio. Namba kaipata kwa mke wake.Kumuuliza yuko wapi anasema wao wanaishi Bukoba.

Mzee anatia huruma maskini. Sasa kijana mimi Bukoba hata sikujui me nipo Dar es salaam wala sina mahusiano na mke wa mtu nasikitika mzee kapewa namba ya uongo so anayetembea na mke wake ataendelea huku mzee akiamini ashamkanya.
 
Bulldog

Kuna mmoja alimfuata anayemuibia mke kutoka dar mpaka dodoma usiku sa nane usiku nakumpiga vibaya mno... NIKAAMINI MKE WA MTU SUMU KALI
 
Last edited by a moderator:
Mtanjiwa wengi nakutupwa vichakani
Bulldog
Kuna mmoja alimfuata anayemuibia mke kutoka dar mpaka dodoma usiku sa nane usiku nakumpiga vibaya mno... NIKAAMINI MKE WA MTU SUMU KALI

Kuna siku nlikuwa narudi kutoka Mombasa, all the way nachat na mamsap!

Kufika SEGERA, ghafla ikaingia sms, si tu ni love sms, sms imekaaa ki mchepuko mchepuko!

Worse than all, sms haina uhusiano na kile tulichokuwa tunajadili wakati huo, mf miss chagga tunajadili Mahindi yanaliwa na Ngedere shambani, ktkt inaingia love sms!

Guess what happened?
 
Last edited by a moderator:
Kiukweli ni moja kati ya matukio yenye kuumiza moyo na kuleta huzuni isiyomithirika hebu vuta picha ni maumivu makali kiasi gani utayapata pale unapogundua kuwa yule uliyeamini kuwa ni malikia wa moyo wako yule ambaye kila siku anakuimbia nyimbo nzuri za mapenzi huku mkiwa watupu kitandani yule ambaye kila siku analalama kuwa maisha yake hayawezi kukamilika bila ya uwepo wako hapa duniani.

Yule ambaye mlikula nae viapo kuwa ni kifo tu ndio chenye haki ya kuwatenganisha kwani muunganiko wenu MUNGU pekee ndiye aliyeuunganisha yule ambaye ulijitoa na kumpigania kwa kila hali kwa ajili yake ili ajae tabasamu usoni mwake,yule ambaye ulimkuta hana mbele wala nyuma na ukaamua kumuinua ili na yeye aonekane mtu kati ya watu, hadi ukafikia hatua ukagombana na ndugu zako au watu wa karibu kwa ajili yake alafu unakuja kugundua kuwa kumbe yale yoote uliyokuwa ukiyapigania kwake hayana maana tena.

Hayana thamani hata chembe ndani ya moyo wake, yale yote uliyokuwa ukiyafanya juu yake ni kama ulikuwa unajipendekeza tu kwake kumbe kuna mtu mwingine anamthamini kuliko wewe uliyekuwa unajitoa kwa ajili yake ukiangalia nyuma umbali uliotoka, muda uliopoteza na hasara ulizopata juu yake unajawa na hasira ambayo inaweza ikakufanya ufanye jambo lolote baya ukifikiria magumu.

Uliyopitia kwa ajili yake unatamani umkate kichwa kwa hasira,ukitazama jinsi alivyokutenganisha na ndugu na marafiki katika kumfanya yeye afuarahi.. unabaki ukimuangalia anavyokucheki kwa dharau huku wewe ukibubujikwa na machozi mengi ya hasira kali, kabla hujaamua adhabu umpe inamfaa ambayo itamfanya na yeye ayapitie maumivu makali unayohisi wewe kwa ajili yake.Ni matukio ambayo usiombe yakukute maishani mwaka.kwani yanaweza yakabadilisha kabisa maisha yako na kuonekana kituko kama sio mwendawazimu mbele ya jamii.LOVE HURTS
 
Nyie ndo mlotufundisha kuchepuka mn kila cku cc ndo watu wa kuwasamehe tu km vile hatuna mioyo
 
Mke / Mume wa mtu ni mtamu, acheni lakini usiombe ya kukute
 
Hivi kumbe huwa mnaelewa kuwa mapenzi yanaumiza eeh... Sasa mnavyojihalalishia michepuko mnadhani wanawake wana mioyo ya mawe??!!!
Pole sana...unaonekana bado una makovu ya huba...maana kwa jinsi ulivyopanic.......mungu atakujaalia utapona tu.........
 
nyie ndo mlotufundisha kuchepuka mn kila cku cc ndo watu wa kuwasamehe tu km vile hatuna mioyo

nyinyi kuwa na wanaume wengi ni janga kwenye familia,kijamii na kithamani pia kwakuwa mwili wako unatumiwa na kila mtu unakuwa hufai
 
KikulachoChako

Hahahahahahahaha kumbe huwa inauma kiasi hicho na nyie?poyeeeeee!
wenzenu tushazoea kujiuliza hayo maswali kiasi mpk sa hiz hatujiulizi tena!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom