Kuchukua Coordinates za eneo lako au unalotaka kulimiliki

mtafiti muelewa

Senior Member
Oct 16, 2013
186
98
Unajua ni kiasi gani inaumiza pale nyumba yako inapowekewa "X" na ukajua kabisa kuwa itavunjwa bila kulipwa fidia? Utajisikiaje pale mamilioni uliyotumia kujenga yanapopotea na mateso juu ya kutafuta pa kwenda? Je utajisiaje ukiwekewa zuio la kuendeleza eneo lako na kuambiwa uendelezaji unaotaka kuufanya si sahihi kwa eneo husika na ulitumia pesa nyingi kununua eneo hilo?

Mambo yamebadilika sana. Kuishi kiholela hakupo tena. Kila siku watu wanabomolewa nyumba zao. Wanapoteza pesa pia wanakosa sehemu za kuishi. Unataka kuwa mmoja wao? Naamini hutaki kuwa mmoja wao.

Na kama hutaki basi fanya yafuatayo.

1. Kabla hujanunua eneo ambalo halijapimwa tutafute wataalamu tukusaidie kutokana na matakwa yako juu ya eneo hilo (tuchukue Coordinates na tukwambie kuwa hilo eneo limetengwa kwa matumizi yapi)

2. Kama unamiliki tayari, pia tutafute turasmishe eneo hilo kwa kulipima. Ili uishi kwa amani na uhakika wa eneo lako.
Bila kusahau eneo lililopimwa linakupa fulsa mbalimbali ikiwemo kukopesheka.

PIA TUNATOA HUDUMA ZIFUATAZO
-Kufuatilia HATI (Umepimiwa ila hujapata hati)
-Kubadilisha jina kwenye HATI (Ulinunua eneo au jengo na ukafuata taratibu zote kisheria, isipokuwa kwenye Hati bado kuna jina la aliyekuuzia. Sisi tutakusaidia kufanikisha mchakato wa hiyo hati kuwa na jina ulitakalo)
-Kubadili matumizi ya Ardhi (Umenunua eneo la makazi ila unataka kuendeleza kama sehemu ya biashara. Tunatoa msaada katika kufanikisha mabadilika hayo kuwa rasmi)
-Kufuatilia kibali cha ujenzi (Building Permit).
-Tunafanya Uthaminishaji ( Property Valuation)
- Tunatoa ushauri juu ya masuala ya Ardhi.

Kwa huduma ya yeyote hapo juu tutafute kwa no 0657 317631.
Tuko Samora Avenue, Matasalamat building, floor ya tatu.

Asanteni na Karibuni sana
 
Kuna matatizo mengi sana yamekuwa yakiwakuta wamiliki wa ardhi zisizo rasmi(Hazijapimwa). Watu wanajikuta wanamiliki maeneo ambayo kisheria hawakupaswa kumiliki. Kwa mfano, maeneo ya viwanja vya michezo, maeneo ya hospital, maeneo ya shule, maeneo ya makaburi, hifadhi za barabara, mabondeni nk.
Matatizo yanakuwa makubwa zaidi pale unapogundua kuwa umiliki wako umeangukia katika eneo lisilo sahihi na umeliendeleza eneo hilo, mfano umejenga na ukaambiwa utabomolewa kwa kujenga eneo lisilo sahihi.
Tufanye nini sasa?

Kwanza tuwe na utaratibu wa kujua eneo unalonunua kwenye TP (Town Planning Drawing) liko sehemu gani. Je ni eneo la shule? Je ni viwanja za michezo? Je ni hifadhi ya barabara nk.
Kama ulishanunua pasipo kujua na hujaendeleza eneo hilo ni nafasi yako pia kujua eneo lako liko sehemu gani katika TP ya eneo husika.

Kwa huduma ya kuangaliziwa eneo lako ili kujua lipo sehemu gani katika TP niPM mimi. Tutakwenda site nitachukua coordinates kisha tutaziprocess na tutakuprintia TP ikionesha eneo lako lilipo.
Hii huwa ni hatua ya kwanza katika mchakato wa kupima ardhi yako. Kwahivyo basi kama pia unauhitaji wa kupimiwa eneo lako unaweza kuniPM pia na tutafanya hatua moja baada ya nyingine mpaka kukupimia eneo lako.
Asanteni sana.
Mimi nahitaji hiyo huduma 0713322856
 
Hivi kwann mamlaka husika wasitengeneze website na kuainisha maeneo ya kujenga makazi na yasiyofaa kwa makazi katika kila mkoa.
Inatakiwa michoro iwepo kwenye ofisi za serikali za mitaa. Lakini hata ikiwepo haitoshi kuonesha mwenye kiwanja kuwa kiwanja chake kimekaaje. Lazima awepo mtaalamu asaidie.
 
michoro ipatikane mpaka kwa watendaji wa kata na vijiji,hii itasaidia sana kwa matatizo ya ardhi yote
Mh. Lukuvi kasema michoro iende kwenye ofisi za serikali za mitaa. Hii itasaidia ile kupunguza gharama za kuuchukua mchoro wizarani tu. Ila mtu unaweza kumpa mchoro husika na GPS pia na akashindwa kujua eneo lako likoje kwenye hiyo TP. Itasaidia but cha kusaidia zaidi ni kielemisha jamii kiwa kabla hujamiliki ardhi watafute wataalamu wa mipango miji. La sivyo hata kila mtu akipewa mchoro haitatua tatizo kwa kiwango cha juu..
 
Back
Top Bottom