Kuchonga Funguo za Gari

Kuchonga Funguo za Gari

Raimundo

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2009
Posts
13,415
Reaction score
12,627
Nimepotelewa na funguo ya gari na haikuwa na copy, vipi kuna uwezekano wowote wa kutengeneza funguo bila copy ya kuangalizia?

Kama kuna mtu anao utaalamu tusaidiane au tupeane contacts kwa anayemfahamu mtaalam.
 
Pole sana Mimi niliwahi kupata tatizo kama lako na nilikuwa sina copy nikaenda pale mtaa wa Lumumba jamaa akanitengenezea tatizo nilishapoteza namba zao ila ofisi yao naijua maana inaangalia barabarani.ni jirani na makao makuu ya ccm dsm
 
Nimepotelewa na funguo ya gari na haikuwa na copy, vipi kuna uwezekano wowote wa kutengeneza funguo bila copy ya kuangalizia?

Kama kuna mtu anao utaalamu tusaidiane au tupeane contacts kwa anayemfahamu mtaalam.
Funguo ya gari gani? kwasababu kuna magari yenye immobilizer system, unaweza kuchonga funguo vizuri lakini isiwashe gari mpaka ufunguo uwe programmed kuwasha gari hilo. Gari lako Make, Model, Year gani?
 
Haswa yanayotoka Europe. Nenda manji pale kisutu wanaprogram ya computer
 
Hapa si unaweza kuchonga funguo ukaiba gari ya mtu???
magari mengi ya siku hizi yanakuja na immobilizer system, ili kuwasha yanahitaji uweke Master Key au Transponder Keys zilizokuwa programmed na ECU ya gari. Ndani ya funguo kunakuwa na chip inayofanya mawasiliano na ECU ya gari. Bila huo ufunguo Anti Theft System inakata Fuel Flow kwenye Engine kwahiyo gari haliweza kuwaka,,mfano mzuri kwenye magari ya Toyota kunakuwa na taa nyekundu inaBlink either ndani ya speedometer au kwenye dashboard, inakuwa na shape ya gari + ufunguo. Unapochomeka ufunguo unaotambulika ile taa inazima..
2i8uf14.jpg
 
Mrejesho: Baada ya kuomba ushauri wa wadau mbali mbali nimeenda kwa fundi wa funguo pale Ubungo, nimeenda naye mahali lilipo gari kanirekebishia.

Hawa jamaa si mchezo funguo inawasha gari kama vile ni original.

Gari ni Suzuki Swift, madhani haiko programmed kama mdau Brakelyn alivyosema hapo juu.

Asanteni sana wadau.
 
Last edited by a moderator:
magari mengi ya siku hizi yanakuja na immobilizer system, ili kuwasha yanahitaji uweke Master Key au Transponder Keys zilizokuwa programmed na ECU ya gari. Ndani ya funguo kunakuwa na chip inayofanya mawasiliano na ECU ya gari. Bila huo ufunguo Anti Theft System inakata Fuel Flow kwenye Engine kwahiyo gari haliweza kuwaka,,mfano mzuri kwenye magari ya Toyota kunakuwa na taa nyekundu inaBlink either ndani ya speedometer au kwenye dashboard, inakuwa na shape ya gari + ufunguo. Unapochomeka ufunguo unaotambulika ile taa inazima..
2i8uf14.jpg

Nimekupata mkuu
 
Mimi Nina sefu funguo zilipotea miaka kumi iliyopita naweza pata mtu wa kuchonga funguo!
 
Back
Top Bottom