Kubomoa Naura Spring Hotel ni komoakomoa sio bomoabomoa

Mnyika aliposema JK ni dhaifu wengi mlikubaliana naye sasa hakuna mantiki ya kuhoji kwamba kwa nini ujenzi uliachwa uendelee mahali pasipofaa ilhali mkijua serikali iliyopita ilikuwa dhaifu.

Au mmesahau maana ya kuwa dhaifu?

Kama una kibali chochote ulichokipata awamu ya nne jiandae kisaikolojia maanake inawezekana anayekitambua ni huyo huyo aliyekupa.

Nchi haiendeshwi kwa mujibu wa busara bali ni kwa mujibu wa sheria hivyo basi kama kakiuka sheria asiangaliwe usoni.
 
Kushabikia mali za watu wengine kuharibiwa kwa mwanvuli wa sheria sio jambo zuri, watanzania tunaonesha jinsi gan tuna roho mbaya kwa watu waliopata na ndio sifa kuu ya ngozi nyeusi, ww kama uliandikiwa No ni No tu mpaka unarudi kaburin, hata ukishabikia wenzako kuonewa na kuharibikiwa haitakusaidia kitu, hiz sio siasa tena ni visasi na roho mbaya, msishangae vikaanza kuibuka vikundi vya mauaji kama mungiki,manake for every action there is opposite reaction which may be of greater magnitude.
 
Ni maumivu makubwa sana kubomolewa nyumba kama hii. Lakini ni bora ibomolewe tu. Tulisema sana jinsi alivyoharibu mazingira, pengine madhara yake yanafichwa na uzuri wa macho wa Jengo lenyewe.
Chemichemi ya maji ni mhimu sana kuliko hilo Jengo.
Watu, vizazi na Vizazi watatumia maji hayo. Je kuna haja ya kuharibu maji hayo Kisa Jengo?
Nchi hii iliharibiwa na huyo cheka cheka maumivu yote kuleta yeye. Poleni sana Naura spring. Jengeni sehemu sahihi.
 
Ila naanza kuingiwa mashaka na akili za Magufuli,you simply can't do this in the name of environment preservation. Only mad man can do this,not sane man!
nilianzisha thread hapa jf nikiulizia kama magufuli akili zake ana matatizo ya kisaikolojia au vp? maana jamaa anapenda sana kubomoa yaani kupita kiasi tangia akiwa waziri wa ujenzi, nikatukanwa sana na uzi ukafutwa, kama hii habari itakua sahihi basi magufuli apimwe akili
 
kama wamejenga pasipo halali
Nyie wenyewe ndio mnahusisha hili zoezi na siasa! Kama watu wamejenga sehemu ambazo haziruhusiwi sheria ifate mkondo! Hata watu wa mkwajuni na bonde la msimbazi wamebomolewa ..wala si Naura pekee!

Hata wamkwajuni nao wanasema walipata vibali!
kama wamejenga isivyo halali wabomolewe tu kwani hakuna namna nyingine
 
Mbona Lumumba ndio watetezi wa hii kitu,Hapa kuna siri nyuma ya pazia.kumbukeni hamumjengi raisi kwa kumdanganya afanye mambo yatakayozidi kumgombanisha na jamii.Embe lenyewe kaliokota chini ya Mbuyu mharibieni hivyohivyo halafu baada ya miaka mitano mtaelewa athari yake.
 
Jamaa ana HATI na kibali cha ujenzi? Je wakati wanatoa HATI hawakujua kama hapo ni bondeni?/ Je hizo gharama za ujenzi nani atazilipa?
Kweli ndugu, nashauri wafuatiliwe pia walioruhusu kujengwa hapo ila kama hakuna aliyeruhusu, ianguke ndani ya cku 9
 
nilianzisha thread hapa jf nikiulizia kama magufuli akili zake ana matatizo ya kisaikolojia au vp? maana jamaa anapenda sana kubomoa yaani kupita kiasi tangia akiwa waziri wa ujenzi, nikatukanwa sana na uzi ukafutwa, kama hii habari itakua sahihi basi magufuli apimwe akili
Kweli apimwe akili. Tunajenga au tunabomoa? Yeye angeweka misingi kuanzia sasaiv yasitokee ya nyuma
 
Kwa hiyo unataka watu waachwe tuu kuendelea kuvunja sheria kwakuwa kuna watu walivunja huko nyuma na kuwapa vibali kujenga pasipo stahili? Hata watu wa bonde la msimbazi wamekubwa na hii bomoa bomoa si Naura pekee....

Argue kwa kwa kutumia common sense na si political sense, wamabondeni wote walikuwa na vibali? mbona ni 681 tu ndio wametinga mahakamani? Kama huyo Naura hakuwa na building permit hiyo ni case nyingine lakini kama alikuwa na building permit yeye atajuaje uhalali wa kibali so long kimetolewa sehemu husika na hakinunuliwi kwenye black market?
 
Mimi nataka na hayo majengo ya serikali yabomolewe kuanzia tanesco ubungo TRA Arusha central police Arusha nssf na ofisi nyingine zilizopo kando na ofisi za serikali zipo nyingi zilizopo maeneo kama hayo azivunje sio kuvunjia watu
 
In order to be safe, make a pact with the Almighty God and follow the necessary minimum requirements for anything to last. Watanzania wenye pesa wamezoea kufikiria wana uwezo wa kuchezea sheria na kuzipinda bila kupata madhara. Open space nyingi waliovamia sio watu hohehahe...ni watu wenye nguvu zao. Kwanini tushiriki kwenye msiba walioamua kuutengeneza kwa kutojari sheria na kufuata taratibu zilizopo?
 
Nimeishi arusha ukweli hayo majengo pamoja na ccm yapo mtoni kabisa yabobolewe tu hamna namna
 
ibomolewe tu aliambiwa asijenge akawa mbishi,, hiii hotel iko mtoni kabisa na kuna taarifa alipojenge kuna tindiga uwezekano wa kudidimia na kuanguka ni mkubwa, bora wabomoe mapema kabla halijaleta madhara kwa binadamu
 
Naura Springs imejengwa kwenye mto Goliondoi na ukitaka kujua athari za ujenzi huo kaangalie flow ya maji ya mto Goliondoi ilivyopungua
Wacha kusema usichokijua
1)Ni mto Naura sio Goliondoi,miaka ya sitini ukitwa Naururu
2)Mto huo na Themi imeanza kukauka miaka yasitini wakati huo mmiliki Mrema alikuwa dobi WA Muhindi Hana kitu
3)Hospitali ya. Mt Meru,Polisi mkoa na wilaya zote ziko usawa huo huo ZIVUNJWE pamoja na TRA ?
A little knowledge is worse than no knowledge
 
Back
Top Bottom