Kubomoa Naura Spring Hotel ni komoakomoa sio bomoabomoa

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,479
Heshima yenu wakuu,

Mimi nimeanzisha hii thread kulaani kitendo cha Watanzania kushindwa kujiongeza na kurudishana nyuma. Mimi sioni kama kuna haja ya kukomoana kwa kutumia nafasi tulizonazo kisiasa au kiuchumi.

Naura Spring Hotel ndani ya Arusha, yapewa siku tisini kujiangusha yenyewe au bulldozer la Magufuli lifanye kazi

Nianze kwa kusema kwamba Tanzania ni Nchi ya Vyama vingi, na Mtanzania yupo huru kuunga Mkono chama chochote anachopenda.

Usitegemee kwamba utagombea nchi ya vyama vingi wote wakuunge mkono. Huu ni wakati wa kutibu majeraha ya Uchaguzi na Kujenga Nchi yetu iwe na Umoja amani na Maandeleo sio Muda wa Kukomoana.

Nitoe tahadhari katika hili, siku zote unaweza ukamkimbiza mjusi akakimbia, lakini akiona amezidiwa anageuka nyoka na kuanza kukukimbiza wewe.

Mimi kuna Maswali yananitatiza;

1.Hili Jengo hadi linajengwa Serikali haikuwepo?

2.Je, alipewa Vibali vya kujenga na wakaguzi walilikagua?

4.Aliyeruhusu kujengwa kwa jengo hili kachukuliwa hatua gani?.

5.Kwanini Serikali isiingie garama ya hili jengo?

6.Imekuaje Kuanzia Msingi jengo mnaliona hadi lifike hatua hii ndo ulibomoe? Huu ni uzalendo?

7.Hakuna njia mbadala ya kufanya ili hili jengo lisibomolewe?

Hili jengo Mahakama ndiyo ilimruhusu ajenge baada ya kushinda kesi dhidi ya Manispaa ya Arusha kumzuia Kujenga.

Eti inavunjwa kisa ipo bondeni. Mbona maji hayaingii ndani? Mto Sanawari Miaka yote upo na hili jengo halijawahi kusitisha shughuli kisa maji yameigia wala hapajawahi kutuwama maji.

Hii itakuwa Hotel yake ya pili kuwekewa X baada ya moja ya Mwanzo kuwekewa alama ya X.Impala Hotel, Leopard Tours Offices kuvunjwa.

Kama ndivyo, Basi tufanye hii Nchi iwe ya chama Kimoja. Nchi hii ni yetu sote. Nchi kwanza Vyama baadae. Roho za kukomoana zishindwe kwa jina la Yesu.

Arusha Wamechagua Mabadiliko, Wapigwe mabomu, wapigwe risasi, wabomolewe, wanyimwe huduma za kijamii, vyovyote vile mtakavyo fanya haisadii.

IMG-20160108-WA0008.jpg
IMG-20160108-WA0009.jpg
 
Last edited:
Mkuu figganigga this is too much. Hawa watendaji wa Magufuli naona wanaacha kufanya kazi kwa weledi na wanaanza kufanya kazi kwa kulipiza kisasi na kukomoana. Kama hilo jengo liko bondeni na jengo la CCM pembeni yake liko angani? Na nyumba za serikali ambazo ziko pembeni je? na ofisi za CEDHA nyuma yake je? Kama hizo zote hazijapigwa X basi na hili jengo lisipigwe X wala lisivunjwe.
 
Last edited:
Nyie wenyewe ndio mnahusisha hili zoezi na siasa! Kama watu wamejenga sehemu ambazo haziruhusiwi sheria ifate mkondo! Hata watu wa mkwajuni na bonde la msimbazi wamebomolewa ..wala si Naura pekee!

Hata wamkwajuni nao wanasema walipata vibali!
 
Mkuu issue ya Naura Spring ni zaidi ya unavyojua, kumbukumbu zangu zinaonyesha waliopinga ujenzi wake kwa sababu sheria inakataza ujenzi wa nyumba ndani ya mita 60 kutoka mtoni walihamishwa kufuatia kubishana na wakuu wao.

Kama itavunjwa Mrema avumilie maumivu yake kama ambavyo wale viongozi walivyovumilia baada ya kuhamishwa.
 
Ila naanza kuingiwa mashaka na akili za Magufuli,you simply can't do this in the name of environment preservation. Only mad man can do this,not sane man!
Kwa hiyo unataka watu waachwe tuu kuendelea kuvunja sheria kwakuwa kuna watu walivunja huko nyuma na kuwapa vibali kujenga pasipo stahili? Hata watu wa bonde la msimbazi wamekubwa na hii bomoa bomoa si Naura pekee....
 
Nakumbuka miaka mingi hili jengo lilikaa bila kufanyiwa finishing (likiwa skeleton), kuna anayejua ilikuwa ni kwa nini!?
Kuna msemo wa Wajerumani kuwa 'perfection doesn't exist...' bali sis binadamu tunajitahidi kadri tunavyoweza na kamwe hatuwezi kufikia ukamilifu. Kama basi serikali ya JPM imekusudia kuwa in perfection kwenye nchi ambayo kila kitu ni imperfect kwa 95% basi badala ya bomoabomoa waanze na ukamilifu katika elimu maana ndio engine kuu ya uwepo wa binadamu duniani!
 
Mkuu @figanniga this is too much. Hawa watendaji wa Magufuli naona wanaacha kufanya kwa weledi na wanaanza kufanya kazi kwa kulipiza kisasi na kukomoana. Kama hilo jengo liko bondeni na jengo la CCM pembeni yake liko angani? Na nyumba zaa serikali ambazo ziko pembeni je? na ofisi za CEDHA nyuma yake je? Kama hizo zote hazijapigwa X basi na hili jengo lisipigwe X wala lisivunjwe.

Bomoa tu tunataka Arusha uwe mji wa Kimataifa, na hauwezi kufikia hiyo hadhi kama kila mtu anajenga anavyotaka, nasema Bomoa yote tuanze upya kesho utambue kwamba fedha siyo kila kitu bali kuna sheria za nchi ambazo ni lazima zifwatwe!
 
Nyie wenyewe ndio mnahusisha hili zoezi na siasa! Kama watu wamejenga sehemu ambazo haziruhusiwi sheria ifate mkondo! Hata watu wa mkwajuni na bonde la msimbazi wamebomolewa ..wala si Naura pekee!

Hata wamkwajuni nao wanasema walipata vibali!
Ndo maana Mahakama imesitisha baada ya kuona haki haitendeki. Hiyo mkwajuni Mlioboa Nyie hamna hata Mwenyekiti wa Mtaa. Keko mnapotaka kubomoa hamna hata mwenyekiti wa Mtaa.
 
Nakumbuka miaka mingi hili jengo lilikaa bila kufanyiwa finishing (likiwa skeleton), kuna anayejua ilikuwa ni kwa nini!?
Kuna msemo wa Wajerumani kuwa 'perfection doesn't exist...' bali sis binadamu tunajitahidi kadri tunavyoweza na kamwe hatuwezi kufikia ukamilifu. Kama basi serikali ya JPM imekusudia kuwa in perfection kwenye nchi ambayo kila kitu ni imperfect kwa 95% basi badala ya bomoabomoa waanze na ukamilifu katika elimu maana ndio engine kuu ya uwepo wa binadamu duniani!

Huko kwenye Elimu mbona walishaanza tayari? Wewe hauko Bongo nini? Sasa hivi Shule zote wanaingiziwa fedha kwenye akaunti zao kwa ajili ya Elimu!
 
Mkuu @figanniga this is too much. Hawa watendaji wa Magufuli naona wanaacha kufanya kwa weledi na wanaanza kufanya kazi kwa kulipiza kisasi na kukomoana. Kama hilo jengo liko bondeni na jengo la CCM pembeni yake liko angani? Na nyumba zaa serikali ambazo ziko pembeni je? na ofisi za CEDHA nyuma yake je? Kama hizo zote hazijapigwa X basi na hili jengo lisipigwe X wala lisivunjwe.
Kama Naura imeingilia kwenye uelekeo wa mto au sehemu hisiyo stahili itabomolewa kama wanavyo bomolewa wengine na Kama jengo la Ccm limejengwa sehemu isiyo stahili basi itabomolewa...! Msihusishe hili jambo na siasa..! Watendaji wanafanya kazi kwa weledi mkubwa....
 
Back
Top Bottom