Kubet ni dhambi?

Kubet ni dhambi?

Kubet ni dhambi??

Hellow hellow nakusalimu Tena na Tena

Kuna jambo limenitafakarisha kidogo nimeona nikumegee japo Kwa sehemu halafu nawewe utoe unachokijua kuhusu hilo

Kimsingi Maisha siku hizi yamekuwa na ugumu kidogo kwenye swala Zima la utafutaji iwe ni biashara n.k ushindani umekuwa mkubwa na ndio maana wanaofanikiwa sana siku hizi ni watu wenye talents eg wachezaji mpira , wanamuziki n.k

Tunamwona misso misondo katoka kusini kaja dar kirahis sana Kwa kile alichokua akifanya yawezekana hakuwa anajua kma angefanya kazi Efm siku moja

Na hili limepelekea kugunduliwa Kwa njia nyingi za utafutaji wa pesa Leo hii mchezo wa kubet umekuwa unashika nafasi ya juu sana kama ingekuwa ni hits za YouTube basi ingeshika 01 trends

kwasababu wanaoshiriki huo mchezo wamekuwa wengi na ndio maana Kila kukicha kampuni nyingi za kubet zinaanzishwa ni Kwasababu hata watumiaji pia wapo wengi hivyo watu wenye mitaji wameona ni biashara inayolipa Kwa haraka

Sambamba na Hilo hao wenye mitaji wameona ni biashara inayolipa lakini pia wanaobet nao wameona fursa ya kujipatia pesa za haraka na wakati mwingine ni pesa nyingi ambayo mtu anaweza akatengeneza akiwa ndani na simu yake,

Na kiukweli wapo wengi wanaendesha Maisha mjini Kwa betting tu hakuna kingine mtu ana mtaji wake wa million moja tu anatafuta odds 1.2 ambayo akiamua kuweka kiasi Cha 250,000/= anaweza kuapata 300,000/= hiyo elf 50 ni faida ndani ya muda mfupi kuliko akafungua duka kariakoo Kisha kusubiri wateja na kuanza kulogana Ili kuleta mvuto katika biashara Ili iende n.k

Sasa swala linakuja kwenye dini mbili ambazo ndio zinafahamika sana yaani (Ukristo& Uislam) hili swala la kupata faida ya Namna hiyo inaonekana kama ni kosa na dhambi japo Kwa utashi wa kawaida tu hii ni biashara kama biashara nyingne ambayo mtu angefanya

Yaani anayebet hatofautiani na mwenye duka la simu kwasb wote wanaweka mtaji na lengo ni kupata faida. Na Kwa upande mwingine wote hawa Huwa wanakumbana na hasara pia

Ni kwanini huu uwekezaji ambao mtu ameamua kuufanya uonekane ni dhambi au halamu kama wengine wanavyouita.

Lakini pia nikipita kwenye maandiko labda nizungumzie Kwa upande wa Biblia Kuna andiko linazungumza jambo Fulani ni gumu kidgo kulielewa

Muhibiri 9:11
Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote.

Huyu anayeongea hapa ni Suleiman ambaye alikuwa tajiri mkubwa sana lakini pia ni mtu wa hekima sana.
Sasa jambo ambalo ameongea hapo ambalo naona ni kama code Fulani imefichwa,

Yaani aliwaza nini hadi kusema bahati ni muhimu katika mafanikio ya mtu.

Kumbe unaweza ukapambana sana kwenye Maisha na usifanikiwe ila kwenye Maisha pia Kuna swala Zima la bahati linaweza likamfanikisha mtu.

Na ni kweli Kuna watu wanapambana sana kwenye utafutaji ila matokeo ni madogo sana halafu Kuna watu ni kama wakigusa button kidgo mambo yao yanatiki na huyu mwandishi anasema bahati humkuta Kila mtu,

Ikumbukwe huu mchezo ni bahati nasibu. Na kiukwel sio tu huu mchezo ndio bahati nasibu ila ukikaa na kufikir Kwa akili vizr utagundua Kila jambo linalofanyika duniani ni almost betting kwasababu hakuna unachoweza kufanya ukawa unauhakika wa 100% kwamba hiki lazma kitakuwa hvi

Kuna watu wamesoma coarse Fulani vyuoni wakiwa na matarajio makubwa lakini mwisho wake ni kinyume,

Kuna walioingia kwenye ndoa wakiwa na matarajio makubwa lakini mwisho wake pia ni kinyume

kuna wanaokwenda hospital na magonjwa ambayo wengine wamepona lakini wao hayohayo hawaponi na wanaweza wakafariki kabisa,

kwahyo unaweza ona mambo mengi sana hayo ni mfano tu ni kama kubet tu hayana uhakika sana na ndio maana yamkini hata Atheists wanaona kama kuwepo Kwa Mungu ni kubet pia Kwa upande wao kwasababu hawaamini kama yupo kweli au lah.

Sasa wewe unazungumziaje swala Zima la kubet especially sports betting maana ndio ambayo imekuwa habari ya mjini Leo hii ni Halali au si Halali Kwa misingi ya dini?

Unaruhusiwa pia kutoka nje box View attachment 2838822
Katika Ulimwengu hakuna dhambi hizo ni porojo za Wazungu na Waarabu tu. na Imani zao za sungura na fisi . Tunachokaza Waafrika ni kwamba Watu hawatakiwi kuishi kwa kubahatisha tufanye kazi.Wazee wa Kiafrika wanasema Michezo ya kubahatisha ni burudani tu wale usiwekeze akili huko maana mwanya wa kufanikiwa ni mdogo sana
 
Mkuu unasema kwenye riba hakuna hasara upo serious kweli ??

Waulize wanaofanya biashara ya kukopesha kama hawapatagi hasara
Kunakuwa na collateral security (Bond/Rehani) ku- secure huo mkopo, mdaiwa akishindwa asset inauzwa ku-cover loss.
 
Kumbukumbu la Torati 18:10
[10]Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,
 
Kumbukumbu la Torati 18:10
[10]Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,
Ushawahi kusoma Hilo andiko katika Biblia ya kiingereza ????? Ukaona neno lililotumika kubashiri ni neno gan?

Deuteronomy 18:10
There shall not be found among you any one that maketh his son or his daughter to pass through the fire, or that useth divination, or an observer of times, or an enchanter, or a witch,

Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,

Sasa unajua maana an enchanter?

enchanter from oxford dictionary
noun
a person who uses magic or sorcery, especially to put someone or something under a spell.

Yapo maneno mengi kwenye kiswahili huwezi pata tafsiri halisi iliyokusudiwa jizoeze kusoma maandiko Kwa lugha tofaut hasa zile ambazo ndio zilitumika kuandika Kwa matoleo ya kwanza.

Maneno mengi sana kwenye Bible ya kiswahili yanaleta shida sana watu wakiyasoma.

Kwa kumaliza tu hiyo bashiri iliyotumika hapo sio betting ni bashiri za wapiga ramli

Ramli ni neno la kiarabu ambalo Huwa matumizi yake ni watu hutumia kumwangalia mtu ana matatizo au shida Gani. Ndio kilikatazwa hiko .
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom