Kubet ni dhambi?

Kubet ni dhambi?

Kuna kitu kinaitwa factors of production (Nyenzo za uzalishaji mali). Theory of distribution/Price Indices.

Kila nyezo ya uzalishaji mali ina ujira(reward)wake.

-Labour-(Salary/Wage)
-Land-(Rent)
-Capital-(Interest)
-Entrepreneur-(Profit/Loss)

Sasa kwa mtiririko huo tofauti ya riba na faida tutaibaini kwamba, huyo mjasiliamali(enterpreneur) sio mara zote anapata profit/faida, kuna muda ana incur loss/hasara, lakini kwa anaeweka Capital/mtaji ili apate interest (riba)yeye lazima apate faida yeye hanaga hasara, ila wa profit anaweza pata mara dufu ya kile alichoweka na wa interest yeye iko fixed kwa muda maalumu, kama ni 5000 kwa mwezi au kwa mwaka kiasi ni kilekile hakipungui wala kuzidi(fixed percentage over time).
Mkuu unasema kwenye riba hakuna hasara upo serious kweli ??

Waulize wanaofanya biashara ya kukopesha kama hawapatagi hasara
 
Yaani watu wa dini wanapenda kuamka na kujitungia dhambi kisa wao hawafanyi...we kama hupendezwi na kitu usifanye...Mungu ni WA kwako sio wa wote...unasema Mara riba Mara kuchuma Mara Nini...bac stock exchange speculation ni dhambi, bac forex ni dhambi, bac mikopo ni dhambi, biashara ni dhambi... kwanza hamna evidence ya bible au Quran iliyosema kubeti ni dhambi kwa sababu waliotunga hivyo vitabu hawakujua future kutakuwa na michezo hio...na hata kungekuwa na vifungu bado haiprove chochote... coz ni watu tu waliandika na kupachika " Mungu kasema" coz wamekosa sababu za msingi kujustify their claims so Wanatumia Vitisho.

I hope nimejibu swali
Well said mkuu naunga mkono
 
Kubeti ni ulevi fulani hivi, ukizoea hutaacha kirahisi, kwa hiyo wanaobeti ni walevi sawa na wa pombe tu. Makampuni ya kubeti na makampuni ya pombe yanashindana kupata nafasi ya kujitangaza kwenye jezi za wachezaji na kwenye mabango viwanja vya michizo waonekane luningani
 
hisia zangu? Walevi wa kubeti mnajua hakuna mistari ya kupinga kubeti, ipo ya kutosha
Mimi huwa sibeti na sijawahi kubeti, ila tunapoongelea dhambi, tunaongelea makatazo kutoka kwenye vitabu vitakatifu.
Bila kutoa nukuu huko, je tutaithibitishaje hiyo dhambi?
 
Kuna kitu kinaitwa factors of production (Nyenzo za uzalishaji mali). Theory of distribution/Price Indices.

Kila nyezo ya uzalishaji mali ina ujira(reward)wake.

-Labour-(Salary/Wage)
-Land-(Rent)
-Capital-(Interest)
-Entrepreneur-(Profit/Loss)

Sasa kwa mtiririko huo tofauti ya riba na faida tutaibaini kwamba, huyo mjasiliamali(enterpreneur) sio mara zote anapata profit/faida, kuna muda ana incur loss/hasara, lakini kwa anaeweka Capital/mtaji ili apate interest (riba)yeye lazima apate faida yeye hanaga hasara, ila wa profit anaweza pata mara dufu ya kile alichoweka na wa interest yeye iko fixed kwa muda maalumu, kama ni 5000 kwa mwezi au kwa mwaka kiasi ni kilekile hakipungui wala kuzidi(fixed percentage over time).
So Mungu hataki fixed income au sio..😂
 
We mtu Akiwa shoga nini kinabadilika katika maisha yako, same as betting, hawavunji sheria, hii sio Afghanistan sio kila mtu anamuamini Mungu wako wa kiarabu... heshimu mipaka ya watu
unadhani mashoga hawamwamini Mungu?
 
Kwa kukosa maarifa 🤣🤣🤣 marifa yakowapi?tupe eleza dhambi inatoka wapi ?Wewe hapo usipobeti huwezi ukakizi mahitaji yako ya kila siku.
unaona sasa jinsi unavyotafuta uhalali wa kubeti kama ni haki yako na sio dhambi?
Jamii imegawanyika kwenye hilo. Wapo wanaoamini ni dhambi na mpo nyinyi mnaoamini ni haki na sio dhambi....

sasa kuna tofauti gani na hizo jamii zingine nilizotaja ambazo nazo zinatafuta uhalali kwamba wanacho kifanya ni haki ni halali na si dhambi?

Katika Jamii kuna mgawanyiko mkubwa kama ilivyo dini. Watu wametofautiana kwamba dini yao ndio haki ni bora kuliko nyingine...

Maarifa ni Muhimu sana katika kuishi ndani ya Jamii hizi
 
proof ya nini tena?

Mashoga wanatafuta uhalali kwamba wanachofanya ni haki yao na ni halali haina shida kabisa....

Wabetiji nao ni hivyo hivyo...

Ndio maana kuna wanaoona ni sawa na kuna wanao ona si sawa...

Akili za kuambiwa changanya na zako...
Ushoga kwenye vitabu vya dini umekatazwa. Kubet kumekatazwa wapi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom