Kubenea apandishwa Mahakamani leo

Kubenea apandishwa Mahakamani leo

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,278
Reaction score
8,868
Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea anafikishwa mahakamani Kisutu muda huu.

Huku ni kuiongezea mahakama mrundikano wa kesi zisizo na kichwa wala miguu.

Kwa mtindo huu lazima Makonda ajitafakari mara mbili mbili

=============

UPDATES;

Mbunge wa jimbo Ubungo kupitia Chadema, Saed Kubenea amepandishwa kizimbani kortini Kisutu, jijini Dar es Salaam leo na kusomewa shtaka la kutoa lugha chafu dhidi ya Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.Hata hivyo, Kubenea amekana kufanya kitendo hicho na kesi yake kuahirishwa hadi Desema 29, mwaka huu.

Aachiwa kwa dhamana.
 
Niseme tu kuwa sasa nimeanza kumchukia Magufuli.
Magu wala hana tatizo. Tatizo hapa ni kila kiongozi kutaka kuonekana mtendaji, kesho utasikia naye mwenyekiti wa kitongoji kaamurisha flani atiwe ndani, kesho kutwa napo utasikia balozi wa nyumba kumi, yaani bora tu nao waonekane watendaji.
 
Makonda aangalie, Kubenea yupo vizuri ooh! Na kama kweli wamepelekana mahakamani ningependa haki itendeke na mkosefu awajibike ikiwa ni pamoja na mahakama kutoa fudisho.
 
Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea anafikishwa mahakamani Kisutu muda huu.
Huku ni kuiongezea mahakama mrundikano wa kesi zisizo na kichwa wala miguu
Kwa mtindo huu lazima Makonda ajitafakari mara mbili mbili
Natabiri kuwa uchaguzi wa mameya dar utafanyika wakati kube hayupo
 
Garama za uendeshaji wa hiyo kesi nani atabeba..ni huyo DC ama serikali?
 
huyu makonda hafai kabisa saa zake zinahesabika
 
Serikali itashindwa hii naona hakuna kutumia elimu zaidi ya nguvu.inaweza haribu nchi yetu nzuri
 
Back
Top Bottom