Kubenea apanda kizimbani, akana shtaka na kujidhamini

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
338
180
1457679931167.jpg

Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea pamoja na Manase John Mjema wamepandishwa kizimbani muda huu na kusomewa shtaka wakiunganishwa na Halima Mdee, Mwita Mwikwabe na wengine wawili.

Mbele ya Hakimu Cyprian Mkeha wa Mahakama ya Kisutu mbunge huyo na mwenzake wamesomewa shtaka la kumjeruhi Theresia Mbaga katika ukumbi wa Karimjee mnamo Februari 27 mwaka huu.

Wote wamekana shtaka nakujidhamini wenyewe baada ya kusaini bond ya Sh. Milioni mbili kila mmoja.
 
Attachments

  • 1457679865328.jpg
    1457679865328.jpg
    38.4 KB · Views: 30
  • 1457679904022.jpg
    1457679904022.jpg
    37.8 KB · Views: 51
Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea pamoja na Manase John Mjema wamepandishwa kizimbani muda huu na kusomewa shtaka wakiunganishwa na Halima Mdee, Mwita Mwikwabe na wengine wawili.
Mbele ya Hakimu Cyprian Mkeha wa Mahakama ya Kisutu mbunge huyo na mwenzake wamesomewa shtaka la kumjeruhi Theresia Mbaga katika ukumbi wa Karimjee mnamo Februari 27 mwaka huu.
Wote wamekana shtaka nakujidhamini wenyewe baada ya kusaini bond ya Sh. Milioni mbili kila mmoja.
Kuwa Mbunge halisi wa upinzani hapa kwetu lazima uwe na moyo wa simba maana ni mateso na manyanyaso matupu. Ila uzuri wananchi wanaona na kuelewa kwani maisha ya kubambikiwa kesi wao au ndugu na marafiki wanayajua sana
 
Baada ya figisufigisu hizi kwisha na uongozi wa jiji kuanza kazi tusubiri kugeuka kwa kibao, itakuwa zamu ya makada wa CCM kufikishwa mahakamani kwa makosa ya ubadhirifu na ufisadi.
 
Atamaliza korti zote akifikiri anapata umaarufu kumbe ndio anazidi kuonekana hafai, wananchi wa ubungo oneni mtu mliyetuletea....
 
Inategemea na uko chama gani.Kwa tukio na Utaifa kwanza tunaamini Mbunge anayenyanyaswa hii ni bila kuangalia chama basi ujue ameshika watu Fulani pabaya sana.So Kubenea ataendelea kuwa Mbunge mpaka aseme poo
 
Kuwa Mbunge halisi wa upinzani hapa kwetu lazima uwe na moyo wa simba maana ni mateso na manyanyaso matupu. Ila uzuri wananchi wanaona na kuelewa kwani maisha ya kubambikiwa kesi wao au ndugu na marafiki wanayajua sana
aliyesoma pingamizi la uongo yuko huru na anapumzika na mumewe nyumbani kwake , hii ni aibu sana kwa jeshi la polisi .
 
Atamaliza korti zote akifikiri anapata umaarufu kumbe ndio anazidi kuonekana hafai, wananchi wa ubungo oneni mtu mliyetuletea....
Kwani kajipeleka mwenyewe mahakamani!?
Kwani kajishtaki mwenyewe!? Watanzania vichwa vyetu ni vizito sana kuelewa hata mambo madogo madogo!
 
Atamaliza korti zote akifikiri anapata umaarufu kumbe ndio anazidi kuonekana hafai, wananchi wa ubungo oneni mtu mliyetuletea....
Kama CCM sasa wanafikia hadi kufoji saini ya Hakimu Mkazi Kisutu ya pingamizi la Mahakama na bado aliye wakilisha pingamizi hilo yupo HURU basi TZ ni ya hovyo hovyo kuliko hata watu wanavyo fikiri
 
Back
Top Bottom