Kisutu: Wafanyakazi 18 wa TRL wapandishwa kizimbani, wasomewa Mashitaka 15

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,807
11,969
Wafanyakazi 18 wa Shirika la reli Tanzania, wapandishwa kizimbani na kusomewa Nashitaka 15 ya matumizi mabaya ya madaraka.

Ni wale waliotoa zabuni ya uaguzaji wa mabehewa ya mizigo na mabehewa ya mafuta.

Washitakiwa wote wamekana mashitaka hayo. Kesi imeahirishwa hadi 18Januari 2019.

Washitakiwa wapo nje kwa dhamana ya mtu mmoja na bondi ya milioni 20 na hawatakiwi kusafiri nje ya Dar Es Salaam bila dhamana
IMG_20181212_133221_5.jpg
IMG_20181212_121052_3.jpg
IMG_20181212_121114_0.jpg


Mabosi 18 wa Kampuni ya Reli Tanzania wamefikishwa mahakamani wakikabiliwa na mashtaka 15 yakiwemo ya matumizi mabaya ya madaraka.

Washtakiwa hao walifikishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Maghela Ndimbo.

Wakili Ndimbo alidai shtaka la kwanza linamkabili, Mkurugenzi Mkuu wa TRL, Kipallo Kisamfu ambaye anadaiwa Machi 21 mwaka 2013 Makao Makuu ya kampuni hiyo, akiwa mwajiriwa alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa zabuni kwa Kampuni ya Hindusthan Engeering and Industries Limited bila kuhakiki kwamba mkataba huo utatekelezeka kwa kuzingatia masharti ya mkataba.
Alidai Kaimu Mhandisi Mkuu wa Ufundi, Paschal Mafikiri, anadaiwa kati ya Februari 21 na Agosti 15 mwaka 2013 alishindwa kutoa taarifa ya mkataba wa zabuni wa kampuni hiyo na kusababisha Kampuni ijipatie manufaa.

katika shtaka la tatu, anadaiwa Julai 18,2013 TRL aliidhinisha michoro 274 ya mabehewa ya mizigo kwa Kampuni ya Hindusthan kinyume na mkataba wa zabuni.
Mshtakiwa huyo pia anadaiwa katika shtaka la nne, kwamba kinyume na mkataba aliidhinisha michoro ya mabehewa iliyoandaliwa na Kampuni ya Hindusthan.
Mshtakiwa wa nane, Muungano Kaupunda akiwa Kaimu Mhandisi wa Ufundi na Mkuu wa Idara aliidhinisha mchoro wa mabehewa na mafuta iliyoandaliwa na kampuni hiyo.
Wakili Ndimbo alidai shtaka la sita linamkabili, Kaupunda, Joseph Syaizyagi, Kedmond Mapunda na Lowland Simtengu ambao wanadaiwa kati ya Januari 10 na Februari 20 wakiwa waajiriwa wa TRL kwa nafasi zao za Mhandisi Mkuu wa Ufundi, Mchoraji Mkuu na Msaidizi Mkuu wa Meneja wa Usafirishaji wa Reli na wote wajumbe Kamati ya uthamini walitumia madaraka vibaya kwa kushindwa kufanya uchambuzi za zabuni.

Shtaka la saba kwa mshtakiwa Anthony Munishi , Meneja Mkuu wa Usambazaji, anadaiwa kuidhinisha usambazaji wa mabehewa 274 Febriaro11,2013 bila kuwasilisha ripoti hiyo kwenye bodi ya zabuni .
Gilbert Minja, Mafikiri, Mathias Massae, Munishi, Charles Ndenge, wanadaiwa Februari 20,2013 kwa kutumia madaraka yao vibaya waliidhinisha mapendekezo ya kamati ya uthamini katika mkataba wa Kampuni ya Hindusthan kusambaza mabehewa 274 .

Ngoso Ngosomwiles, anadaiwa Aprili 10 mwaka 2014 maeneo ya karakana ya Tiljala India akiwa Kaimu Mhandisi Mkuu wa Ufundi alitumia madaraka vibaya kwa kuidhinisha uzalishaji wa mabehewa 50 bila kufuata masharti
Ndimbo alidai Yonah Shija na Malumbo Malumbo, wanashtakiwa kwamba Julai 16,2014 waliidhinisha Kampuni ya Hindusthan kuzalisha mabehewa 174 ya mizigo na shtaka la 11 linamkabili Stephen Kavombwe na Donatus Bandebe wanadaiwa Septemba 4,2014 maeneo ya Santragachi India waliidhinisha kampuni hiyo kuzalisha mabehewa 50 ya matanki ya mafuta Shija na Malumbo wanadaiwa Julai 17,2014 waliidhinisha kusafirishwa kwa mabehewa 50, shtaka la 13 kwa mshtakiwa Kavombwe na Bandebe wanadaiwa kuidhinisha kusafirishwa kwa mabehewa 174 kuingia nchini bila kufuata masharti ya mkataba .

mshtakiwa Charles na Ally Mwangila wanadaiwa kati ya Aprili 26 na 27 mwaka 2015 kwa matumizi mabaya ya madaraka waliidhinisha Kampuni ya Hindusthan kuingiza nchini mabehewa 50 ya mafuta na 27 ya mizigo bila kuwa na uhakika kwamba mkataba utatekelezeka .
Wote walikana mashtaka wako nje kwa dhamana hadi Januari 18 kesi itakapotajwa.
 
Wafanyakazi 18 wa Shirika la reli Tanzania, wapandishwa kizimbani na kusomewa Nashitaka 15 ya matumizi mabaya ya madaraka.

Ni wale waliotoa zabuni ya uaguzaji wa mabehewa ya mizigo na mabehewa ya mafuta.

Washitakiwa wote wamekana mashitaka hayo. Kesi imeahirishwa hadi 18Januari 2019.

Washitakiwa wapo nje kwa dhamana ya mtu mmoja na bondi ya milioni 20.
Watashinda magakama ya rufaa, huku kwa mahakimu wa kujikomba kazi kweli kweli
 
Vipi kuhusu mkurugenzi wa trl,yeye hahusiki? Kama hahusiki aliyeithinisha matumizi ni nani??
Wafanyakazi 18 wa Shirika la reli Tanzania, wapandishwa kizimbani na kusomewa Nashitaka 15 ya matumizi mabaya ya madaraka.

Ni wale waliotoa zabuni ya uaguzaji wa mabehewa ya mizigo na mabehewa ya mafuta.

Washitakiwa wote wamekana mashitaka hayo. Kesi imeahirishwa hadi 18Januari 2019.

Washitakiwa wapo nje kwa dhamana ya mtu mmoja na bondi ya milioni 20 na hawatakiwi kusafiri nje ya Dar Es Salaam bila dhamana
View attachment 965797View attachment 965794View attachment 965792
 
Majizi Hayana Nafasi Awamu Hii Ya Tano
Kundi Kubwa Sana Hili Lilikuwa Kupe Kwenye Shirika Linanyonya Damu Taratibu
 
Back
Top Bottom