Lowassa alishtakiwa na kuhukumiwa kwa makosa ya ufisadi katika mahakama tatu tofauti
Kwanza bungeni ambapo wabunge kwa kauli moja walimtia hatiani na kumfukuza Uwaziri mkuu (kwa kumhurumia wakamwambia aandike barua ya kujiuzulu ili apate mafao). Mahakama ya pili ni ya kamati ya maadili ya CCM ambayo ilimwona hafai kugombea urais. Na mahakama ya mwisho ambayo ni funga kazi ni ya Watanzania wote ambapo wengi wao walimtosa kwenye urais baada ya kuwalaghai sana kiusanii ikiwa ni pamoja na kuwaahidi kuwafungulia kutoka gerezani watu waliohukumiwa kihalali. Kwa mtu mwenye uelewa mfupi atasema hao waliomhukumu sio mahakama. Kwa hao niseme tu wabaki kama walivyo ila sasa anatumikia adhabu