DaveSave
JF-Expert Member
- Nov 20, 2010
- 440
- 637
Kwa kawaida mambo yanayotuharibia "direction ya maisha" ni yale yanayotupa raha kwa muda mfupi lakini huwa yana madhara mengi kwa baadae.
Kwa mfano; kuangalia "movies" kwa masaa inakupa raha ya muda mfupi lakini ungetumia muda huo kujiendeleza katika ujuzi kwa kusoma au kufanya biashara kungekupa matokeo mazuri na ya muda mrefu.
Kwa kawaida tunapenda kujiachia na kufanya mambo yanayotupa raha ya muda mfupi bila kujali matokeo yake hadi baaada ya miaka mingi sana ndipo tunakuja kujutia. Mwanzoni unaweza kuona kama hakuna madhara yoyote unayopata kwa sasa.
Hujawahi kukaa na wazee wakaanza kukupa story zao walivyokula bata zamani? Watakuambia mahali fulani viwanja vilikua bei Rahisi sana lakini cha ajabu hawakukunua. Kwa wale wazee walioishi Dar enzi hizo ukimkuta atakwambia Segerea ilikua pori, ulikua ukienda na senti 50 ukimpa Mjumbe unajipimia eneo mwenyewe. Lakini yeye bado anaishi nyumba ya kupanga. Unajiuliza mbona yeye alishindwa kujipimia.??
Au anakwambia Mbezi Beach viwanja vilikua vinalingana bei na kreti moja ya bia. Lakini unashangaa yeye hakununua. It means "aliopt" kreti ya bia instead of kiwanja. Maana yake ni kuwa alichagua jambo la kumpa raha muda mfupi lakini akateseka badae muda mrefu.
Uwezo wako wa kujizuia kutonunua nguo za gharama kwa sasa ili kuwekeza ndio utakaokufanya uwe na maisha mazuri kesho. Uwezo wako wa kujizuia kutonunua simu ya gharama kubwa leo ili usave pesa yako kwa badae ndio kiini cha mafanikio yako.
Uwezo wako wa kujizuia kutoishi kwenye nyumba ya gharama kubwa ili utunze pesa ununue kiwanja chako ndio utakaokufanya ujenge kwako na uondokane na nyumba za kupanga.
Kila wakati jitahidi kuwa mtu unayeweza kujizuia kufanya vitu vinavyokupa raha ya muda mfupi ili uweze kujenga msingi wa kupata mafanikio ya muda mrefu maishani mwako.
Leo jiulize ni vitu gani maishani mwako ambavyo vinakupa furaha ya muda mfupi lakini vinakuharibia malengo yako ya muda mrefu? Ukiweza kuvitambua, mara moja dhamiria na anza kuviepuka ili kujenga msingi imara wa mafanikio yako ya muda mrefu.
Kumbuka, kama hautakuwa tayari kuumia kidogo leo ili upate raha ya muda mrefu, utajikuta unapata raha kidogo leo na unaumia maisha yako yote.
kuwa kuna falsafa mbili za maisha katika maendeleo "either uteseke sasa ufurahi baadae, au ufurahi sasa uteseke badae"
Akina Bakhresa, Mengi, Dewji walikubali kuteseka kwa muda fulani ili waje wapate raha ya muda mrefu.
Bakhersa aliwahi kusema kuwa alianza biashara yake kama "baba lishe" kwa kuuza mgahawa huko Z'bar. Alikubali kuteseka kwa muda mfupi ili atengeneze kesho yake. Leo Bakhresa ni bilionea. Angeamua "kula bata" kipindi hicho bila shaka asingekuwa hapa alipo leo. Pengine angekua bado anasugua sufuria kule Zanzibar akipikia watu.
Mabilionea wakubwa kama Mark Zukerberg, au Bill Gates leo wana maisha mazuri kwa sababu walikubali kuteseka kwenye "jana yao".
Sasa wewe umeanza kazi leo unataka "udrive" wakati huna hata mwaka kazini. Unadhani kesho yako itafanikiwa?
Unalipwa "milioni moja" lakini umepanga nyumba ya laki 5 kwa mwezi. Unafurahia watu wakija kwako wanasifia geti la gharama kubwa na kukupamba "unakaa nyumba kali". Unalewa sifa na kusahau kwamba hilo geti ni la mwenye nyumba na wewe ni mpangaji tu. Aisee my friend Sahau kitu kinachoitwa mafanikio kwako. Utaishia kukaa nyumba za kupanga hadi uzeeni.
Kubali uteseke muda mfupi leo ili ufurahi muda mrefu kesho, au amua kufurahi muda mfupi leo na uteseke muda mrefu kesho. Uamuzi ni wako.!NDO NIMEMALIZA HIVYO WE ENDELEA TU KUZUBAA.