Kubali kukosolewa pale unapokosea

Jayspeed

Senior Member
Feb 23, 2014
156
168
KUBALI KUKOSOLEWA NA SAHIHISHA ULIPOKOSEA
Ili kujua ulipokosea kubali kukosolewa siku zote. Unapokosolewa lazima usahihishe makosa yako hautakuwa tayari kuonekana mtu wa makosa kila mara.

Watu wengi hawapendi kukosolewa na hii ni kwasababu mtu haamini kuwa anaweza kukosea katika jambo lake analolifanya anaona kila jambo analofanya yeye yupo sahihi hapa ni kujidanganya sababu mara nyingi mtu hawezi kujitathimimi peke yake na hata akijitathimini hawez kujikosoa kwa alichokosea ....

Kama ilivyo kwenye mpira wa miguu timu inapofungwa huwa imefanya makosa na goli kutokea wanapotoka uwanjani wakiwa wamepoteza jambo lile huwatafuna mioyo yao hvyo wanaenda kutafuta walipokosea na wana sahihisaha wanaporudi tena uwanjani hiubuka na ushindi na maisha ndivo yalivyo siku zote unapokosea kwenye maisha yanakupiga lakini unapolijua kosa lako na kurekebisha unafanikiwa.....

Hebu fikiria Mafanikio makubwa anayoyapata Jack Ma ndani ya kampuni yake ya Alibaba mpaka sasa yote hayo ni kufanyia kazi makosa yake aliyokosolewa kwenye kazi 30 alizoomba na kukataliwa kote..alijiuliza kwanini na ni wapi hasa anakosea mpaka mashirika 30 yanamkataa kwenye kazi hizo? alijua alipokosea na akafanyia kazi makosa yake sasa hivi ni moja ya matajiri wakubwa duniani na tajiri zaidi ndani ya China....

Kukubali kuwa umekosa haimaanishi wewe ni mjinga au huna akili la hasha! Inamaanisha wewe ni shujaa... Shujaa ambae umekiri kweli umefanya kosa hilo na sasa umejifunza kupitia kosa hilo..

Jifunze kupitia makosa yako rekebisha ikiwezekana uanaposhindwa omba ushauri kwa watu wa karibu ...kumbuka kukumbatia kosa lako moyoni ni ugonjwa, ugonjwa ambao unakuangamiza taratibu na mwishoni kufa kwa aibu
.

By Jay Speed
 
mimi ni mtu ninayejiamini.. ninajua nini kikae wapi na kipi kisikae.. mi sishauriki tena ukinishauri ndo umeharibu kabisa!!
 
mimi ni mtu ninayejiamini.. ninajua nini kikae wapi na kipi kisikae.. mi sishauriki tena ukinishauri ndo umeharibu kabisa!!
Kuna watu wa aina hiyo na mara nyingi wanakosea na watu kama hao wakikosea hawashughuliki nacho bali huanza kipya tofauti na kile kama upo hivyo utajikuta husogei lakini unapokubali kukosolewa huenda ni kitu kidogo tu ukishauriwa unajikuta umefanikisha jambo lako siku zote mafanikio kufanikiwa kwako kunatokana na makosa mengi uliyosahihisha na makosa hayo ni baada ya kukosolewa unapata morale zaid ya kurekebisha na kulifanya jambo hilo ndugu @theend
 
amini nakwambia ukipata rafiki anayekubari kukosolewa mshike huyo ni mwema lakini yule ......ambaye hataki na hayupo teyari kukosolewa na yupo teyari kutumia gharama zozote ili tuu kupindisha asikosolewe huyo muogope hafai kabisa.
 
Kamahukubali kukosolewa, huwezi kujifunza kutoka kwa wengine wanaokukosoa.

Ujumbe huu unatufaa wote.

Ujumbe huu unamfaa zaidi Baba J.
 
Kuna watu wa aina hiyo na mara nyingi wanakosea na watu kama hao wakikosea hawashughuliki nacho bali huanza kipya tofauti na kile kama upo hivyo utajikuta husogei lakini unapokubali kukosolewa huenda ni kitu kidogo tu ukishauriwa unajikuta umefanikisha jambo lako siku zote mafanikio kufanikiwa kwako kunatokana na makosa mengi uliyosahihisha na makosa hayo ni baada ya kukosolewa unapata morale zaid ya kurekebisha na kulifanya jambo hilo ndugu @theend
T a and sxAa
 
Back
Top Bottom