Kuasili mtoto


Mwenye Enzi Mungu, Muumba wa Mbingu na vijazavyo akujaalie Maisha marefu yenye hekma na moyo wa kusaidia kama ulivyodhamiria...akuinue na kuwa viongozi wa wengine ambao hawana maono kama haya ili kupitia wewe na wao wimbi la watoto wanaoishi kwenye mazingira yasiyo rafiki kwa sababu mbali mbali lipungue na hatimaye liishe kabisa!
 
Fanya ambalo utaona namna ya kumlinda huyo kiumbe nina ushuhuda wa jambo kama hili ila kila la kheri tujiweke katika kuamini mambo yatakwenda vizuri.

Kwa yale machache niliyojifunza ni kwamba hadithi za mazuri na yale yasiyo mazuri zipo.

Hivyo la msingi ni kuamua tu.

Ni kama vile ndoa. Kila siku watu walio kwenye ndoa wanaumizana lakini wapo pia ambao hawaumizani.

Lakini ukweli huo hauwafanyi watu waache kuchumbiana na kuoana.

Ukitaka kufanya jambo jema kwa kuangalia na kukazia mabaya yake basi pengine unaweza kushindwa kufanya lolote lile maishani.
 
Ninamjua kijana aliyeasiliwa na familia moja miaka ya 90's na hua haogopi kusema alipochukuliwa

sasa yupo mwaka wa pili anasomea elimu ya utabibu
amekua msaada mkubwa sana kwenye familia ile naimani atawasaidia pia sana baadaye

Kila la kheri!
 
Ninamjua kijana aliyeasiliwa na familia moja miaka ya 90's.

sasa yupo muhimbili mwaka wa pili anasomea elimu ya utabibu

amekua msaada mkubwa sana kwenye familia ile naimani atawasaidia pia sana baadaye

ni jambo lenye Baraka sana

Kila la kheri!

Safi sana na mifano kama hiyo ipo mingi tu.
 
Ni nzuri hii idea ht mimi mambo yakiwa sawa nitafanya hivyo sema watafutie mama yao mkuu utalea matom boys lol..

Kama nikiasili basi atakuwa wa kiume ili nilete uwiano kwenye ka familia kangu😀.
 
Dah..hiyo nayo ngumu aisee. Siwezi kutokuwa mkweli kwenye hilo.
Sio wanawake wote akili ya panzi kuweni makini tu na umpendaye ambaye unataka awe life partner, mother of your kids, your best friend and the only one. Ni kuhakikisha anaroho nzuri hata kama sura Sio kama ile ya matangazo tatizo kinakaka wote wanataka kuoa appearance.
 
Kweli kwa kila jambo lina pande mbili kama ulivyotoa mfano wa ndoa huwezi kuishi kwa kuangalia wengine huwezi kupata jibu. Kama wasemavyo wahenga mlima haupandwi kwa kuutizama na huwezi kukatiza daraja kabla hujafika kila la kheri NN.
 
"Your best friend and the only one" nimependa hapo zaidi teh
 
Kweli kwa kila jambo lina pande mbili kama ulivyotoa mfano wa ndoa huwezi kuishi kwa kuangalia wengine huwezi kupata jibu. Kama wasemavyo wahenga mlima haupandwi kwa kuutizama na huwezi kukatiza daraja kabla hujafika kila la kheri NN.

Shukrani saana!
 
Shukrani saana!

Tanzania process ni ndefu inaweza kuchukua miezi mitano mpaka sita.

Na huwezi kumuasili moja kwa moja mpaka uwe umekaa nae miezi mitatu chini ya uangalizi wa hao waliokupa, baada ya hapo ndio utafuata utaratibu wa kumuasili!
 
Nimeipenda sbb yako kua unapenda sana watoto na hupendi kuona wakiteseka kwa namna yoyote.

Na hiyo ndio sbb kubwa ya watu walioasili au wanaotaka kuasili,
UPENDO na HURUMA kwa watoto,

Nikutoe khofu, kuasili mtoto hakuna tabu yoyote, tena akiwa mdogo sana ni vzr maana utamkuza vile unavyotaka wewe,

Akikua kama utapenda kumwambia ni sawa kama utanyamaza ni sawa pia, japo ni vizuri ajue kabla wanafki hawajaleta mambo yao na kumjaza mtoto ujinga.

Kila la kheir,
Nami nipo mbioni kuasili.
 
Tanzania process ni ndefu inaweza kuchukua miezi mitano mpaka sita.

Na huwezi kumuasili moja kwa moja mpaka uwe umekaa nae miezi mitatu chini ya uangalizi wa hao waliokupa, baada ya hapo ndio utafuata utaratibu wa kumuasili!

Duh! Kweli mchakato ni mrefu lakini acha tu iwe hivyo maana jambo lenyewe si dogo.

Maisha ya mtu si ya kuchukuliwa kirahisi rahisi tu.
 

Ahsante sana na kila la kheri na wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…