Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,191
- 677
TUME ya Utangazaji Zanzibar, imesema kituo cha kwanza cha televisheni cha binafsi kitaanza kazi ya kurusha matangazo yake kwa majaribio Januari mwakani.
Katibu Mtendaji wa Tume hiyo, Ali Saleh Mwinyikai, alisema jana kuwa, wawekezaji wazalendo wa kituo hicho kitakachoitwa 'Zanzibar One Televisheni' wameshakamilisha taratibu zote muhimu.
Tumeshawapatia leseni ya matangazo, baada ya kuridhika na uanzishwaji waoÖkwa hivyo hiki kitakuwa kituo cha kwanza cha binafsi kwa hapa Zanzibar kurusha matangazo kwenye televisheni, alisema Katibu huyo Mtendaji.
Katibu Mtendaji Mwinyikai, alisema kuwa kuanzishwa kwa kituo hicho kikubwa kutasaidia sana kupunguza tatizo la ajira miongoni mwa wananchi wa hapa, hivyo alitoa wito kwa wazalendo wengine kuwekeza katika sekta ya utangazaji. Sheria yetu hairuhusu wawekezaji ambao si wazalendo kuwekeza kwenye utangazaji, inaelekeza mtu awe Mtanzania, kwa hivyo hii ni fursa kwa wananchi wenye uwezo kujitokeza na kuwekeza, alisema Mwinyikai na kuongeza kwamba yapo maombi machache ya uwekezaji katika sekta hiyo.
Alisema pamoja na kituo hicho kufunguliwa mwezi ujao, lakini pia kuna kituo kingine kitafunguliwa, ambacho kitaitwa Island Televisheni, ambacho kimsingi nao tayari wamekamilisha taratibu za kisheria.
Katibu huyo Mtendaji alisema kianzishwa kwa vituo hivyo ni mafanikio kwa Zanzibar, ambako Serikali imefungua milango kwa wananchi kuwekeza katika sekta hiyo ambako pia ni kukuza uwazi na demokrasia.
Tume ya Utangazaji hapa Zanzibar haikuanza muda mrefu, lakini katika kipindi kifupi kumekuwa na mafanikio makubwa kwa upande wa Radio na sasa pia hata kwa vituo vya Televisheni, alisema Mwinyikai.
mtanzania