Mla Bata
JF-Expert Member
- Jan 24, 2013
- 8,164
- 18,676
Wasalam,
Kumekuwa na wimbi kubwa la wadau hapa JF kutaka kujua taarifa mbalimbali za jinsi watakavyoweza kutoka nje ya mipaka ya nchi hii aidha afrika ama nje ya bara hili, Wapo wenye lengo la kutoka kimasomo, kutafuta kazi, kuzamia n.k.
Wadau mbalimbali wamekuwa wakija na nyuzi mbali mbali kwaajili ya kuuliza maswali ama taarifa juu ya fursa mbalimbali zinazopatikana nje ya mipaka hii, Shukrani kwa baadhi ya wadau wenye kujitoa kwa kushare taarifa mbalimbali za jinsi ya kutoka nje ya mipaka ya bongo , baadhi yao ni Jon Stephano lusungo Isanga family Kiranga The Icebreaker na wengineo.
Lengo la uzi huu ni kuwaomba wakuu Maxence Melo Moderator Farida
Kwa mamlaka mliyonayo muweze kutufungulia forum maalumu itakayohusu mambo na taarifa mbali mbali za safari aidha nje ama ndani ya bara hili, mnaweza mkaliita Safari forum, travel forum n.k
Kwa watumiaji wa forum maarufu ya nairaland mtakuwa mashahidi hawa jamaa wapo vizuri sana kwenye hili, wana forum yao ya travel ambayo wamekuwa wakipashana taarifa mbalimbali za huko duniani na jinsi gani ya kufika kwa namna tofauti tofauti, chungulia hapa Nairaland Travel - Nigeria - Nairaland jamaa hawapo nyuma wamekuwa wakichangamkia fursa kibao za kutoka.
Kuwepo kwa forum hiyo kutasaidia kurahisisha upatikanaji wa taarifa mbalimbali za jinsi ya kutoka na kupashana habari za fursa huko nje.
Ni imani yangu ombi hili litafanyiwa kazi wakuu.
Natanguliza shukrani zangu.
Wasalam.