Kuanzisha ngo: Msaada tutani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuanzisha ngo: Msaada tutani

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MAKOLE, Jul 24, 2012.

 1. MAKOLE

  MAKOLE JF-Expert Member

  #1
  Jul 24, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 601
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Poleni na hongereni kwa kazi wana jf. Naomba kwa mtu anayefahamu hatua za kuanzisha NGO, Ushauri wa usajili na masuala mengine ya ki uzoefu wa namna ya kuendesha NGO anieleze kupitia jf. Tafadhalini naombeni msaada wenu waungwana. NGO yenyewe inahusika sana na mojawapo kati ya mambo yafuatayo; Msaada wa kisheria kwa wanawake, miradi ya utunzaji mazingira, misaada kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum na waishio katika mazingira maalum, elimu kwa waathirika wa HIV/AIDS.
   
 2. Rodcones

  Rodcones JF-Expert Member

  #2
  Jul 24, 2012
  Joined: Oct 16, 2007
  Messages: 403
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  wanakuja kutoa maelezo then na mimi ntafaidi

  kwasasa napita tu.
   
 3. prakatatumba

  prakatatumba JF-Expert Member

  #3
  Jul 24, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,337
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  NGO inadeal na mambo gani?
   
 4. galagaja mtoto

  galagaja mtoto Member

  #4
  Jul 25, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 84
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  napita tu ila n'tarudi
   
 5. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #5
  Jul 25, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Unachotakiwa kufanya ni kuandaa katiba, ambapo mtaonyesha na muundo wa NGO yenu, majina ya viongozi, waweka saini ambao lazima ionekane wamepitishwa na vikao halali vya wanachama wa hiyo NGO. Kwa sasa NGOs zote zinaratibiwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto na watkupa muongozo wa jinsi ya kuandaa katiba ni vyem ukajitahidi kutembelea website yao utapata muongozo na muundo wa katiba unaotakiwa. Katiba yenu lazima ipitishwe na wakili, mtaenda kuilipia then mtawasilisha katiba na risiti kwa mratibu wa NGO pale wizara ya jinsia ambapo mtapewa cheti cha usajili.

  Baada ya hapo kazi kwenu!
   
 6. Kijana leo

  Kijana leo JF-Expert Member

  #6
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 2,872
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  usisahau picha 2 kwa majina ya viongozi na c.v zao kwa kuongezea maelezo ya hapo juu.
   
 7. mozes

  mozes Senior Member

  #7
  Jul 25, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 115
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Fuata maelekezo ya bwana ndyoko bt kwenye kupitsha katba mtaandaa mhtasari wa kikao na kuonesha members na kuwapitsha viongoz accordng 2 muundo wa NGO yenu. Then mtaambnsha cv ya m/kit, mhazn na katbu thn mtapeleka na copy 3 za katba kwa usajil! Members msiwe ndugu wa damu
   
 8. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #8
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Uwe na katiba nakala 8 iliyopitishwa na wanachama. Cv za viongozi zilizobandikwa picha upande wa kulia. Barua ya kuomba Usajili kwa katibu tawala wilaya, barua ya utambulisho toka mtaani ilipo NGO pamoja na ya mtendaji wa kata, muhtasari wa kikao ulipoitisha katiba pamoja na saini zao, saini za waanzlishi wa NGO. Lazima uwe na ofisi na physical address. Nenda kwa afisa tarafa wa eneo husika, atakukagua na kukupa maelezo mengine.
   
 9. MAKOLE

  MAKOLE JF-Expert Member

  #9
  Jul 26, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 601
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Nawashukuru sana wadau kwa hili. Pamoja sana
   
 10. N

  Ngarenaro JF-Expert Member

  #10
  Jul 26, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 312
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33


  Ni nakala 3 sio 8, ufafanuzi wako mzuri pia
   
 11. h

  homeboyz Member

  #11
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ok mdau hapo juu umenisaidia safi sana
   
 12. Meljons

  Meljons JF-Expert Member

  #12
  Jul 29, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 2,591
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  nenda direct wizara husika, ukianzia huku ofc za tarafa na wilaya wana urasimu angali huko wizarani unapata huduma direct. Katiba ni nakala 2 tu.
   
 13. Mkaruka

  Mkaruka JF-Expert Member

  #13
  May 2, 2014
  Joined: Feb 5, 2013
  Messages: 8,613
  Likes Received: 4,759
  Trophy Points: 280
  Good advice!
   
Loading...