Kuanguka kwa soko la hisa Marekani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuanguka kwa soko la hisa Marekani

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by NGAUTI, Sep 22, 2008.

 1. N

  NGAUTI Member

  #1
  Sep 22, 2008
  Joined: Jun 6, 2008
  Messages: 21
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 3
  Wanajamii kuna habari hii ambayo imetawala kwenye vyombo vingi vya habari kuhusiana na kuanguka kwa soko la hisa la marekani.Nimejaribu kufuatilia lakini sijaweza elewa vizuri.Naomba kwa wanaofahamu wanieleweshe.je hali kama hii inaweza pia kutokea katika soko letu la hisa hapa Tanzania.Asante
   
 2. Sita Sita

  Sita Sita JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2008
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 1,196
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Wachumi mko wapi????

  MI nadhani haitawezaq kutokea hapa Tanzania kwa kua wakuna watu walioweza kukopa fedha kutoka kwenye taasisi za fedha za Marekani. Hii itawadhuru sana Uingereza kwa kuwa wao ndio washirika wa Wamarekani katika soko la hisa.

  Ila Tanzania itaathirika kama wakileta morgage za nyumba. Hii ndio chanzo cha kuporomoka kwa soko la hisa marekani. Maporomoko yalisababishwa na hasara ambazo kampuni za nyumba (Estate dealers) walipata. Kampuni hizi zinajenga nyumba na kuuza kwa mfumo wa morgage. Hasa baada ya kupanda kwa bei ya mafuta, viwanda vingi vilikua vinapunguza wafanyakazi ili kupunguza gharama za uzalishaji. Kupungua kwa ajira kumeathiri consumption ya watu wenye kipato cha chini. Hivyo wakashindwa kulipia gharama za morgage.

  Wananchi wengi walijikuta wakipoteza makazi yao (kwa kuchukuliwa na kuuzwa kwa mnada). Hata hivyo kwa kuwa kipato kilikua kimeshuka, kampuni zilijikuta zikiuza nyumba kwa bei ndogo.

  Iliwapasa wananchi kuuza hisa zao ili kujikimu na gharama za maisha zilizopanda. Soko la hisa likakosa wateja.

  Taarifa hizi si Rasmi, Mimi nipo Tanzania. Naomba waliopo US, watuelezee kinaga ubaga.
   
 3. D

  David Nkulu Member

  #3
  Sep 22, 2008
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuanguka kwa soko la hisa kwa Tz ni possible lakini ni less probable. Kushuka kwa bei ya hisa zenyewe kunawezekana kutokana na ugumu wa uchumi unaotokea dunia nzima kwa sasa. Japo hatuna uhusiano mkubwa sana na USA na UK ki-uchumi, lakini vitu kama bei za mafuta zinatuathiri. Na ukishakorofisha mafuta, vilivyobaki vinafuata njia!
   
 4. N

  NGAUTI Member

  #4
  Sep 23, 2008
  Joined: Jun 6, 2008
  Messages: 21
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 3
  Sita Sita na David Nkulu, nawashukuru sana kwa kunielemisha.waliopo US, naona wamekaa kimya.
  kwa kiasi kikubwa nimeelewa nini kimetokea huko na nafurahi kusikia kuwa hapa kwetu si rahisi kwa sasa hali hiyo kutukuta.
  Thanks and stay blessed
   
 5. H

  Haika JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Je hii issue inakujaje?
  Ina uhusiano na Ubepari?
  Je haya ni mapungufu ya ubepari ambayo hayakuonekana au wanajaribu kuyadownplay?
   
 6. D

  David Nkulu Member

  #6
  Sep 25, 2008
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ngaita,

  Hiyo issue (nadhani una maana huko UK, USA) inatokana na wahusika (wall street financial broakers) wa hisa kuwa na uchu mkubwa wa kutengeneza pesa nyingi haraka haraka hivyo kubuni namna tofauti tofauti za bonds / shares (zikaitwa derivatives) ambazo walikuwa wakiziuza kwenye masoko hayo ya hisa kwa wawekezaki zaidi ya zile bonds original ambazo zilikuwa zina represent real life materials mfano mafuta, shaba, dhahabu n.k. . Bonds / shares hizo zikawa zinawazalishia pesa nyingi sana ktk muda mfupi. Wapambe hao walikuwa wakibuni namna hizo kwa kutumia mathematical formulas an vigezo vinginevyo. Bonus zao kwa mwaka ilikuwa ni mamilioni ya USD!!
   
Loading...