Kwenye UJENZI, ni heri jengo liwe na Nondo(Reinforcement) Kidogo au hafifu ila kuliko zege (Concrete).
Kama umeshaangalia Crushing Test basi unajua ninaongelea nini na kama hujaona, basi angalia video chini.
Nondo zikizidiwa UZITO, basi huanza kuvutika hadi zipite ule uwezo wake wa kuvutika na kurudi kwenye umbo lake la mwanzo. Pia huendelea hadi zinaanza kuvutika kwa urefu wa milimita kadhaa kabla ya kuja kukatika (Young's Modulus of Elasticity - kwenye Hooke's Law).
Ila Zege, Elasticity yake (uwezo wa kuwa kama Spring) ni mdogo sana. Ndiyo maana huwa wanajenga na Nondo ili kuzipa uwezo wa mmoja anaweza kubeba uzito wa kukandamizwa (pressure on Concrete) na mwingine uwezo wa kuvutwa na kuvutika (Steel/Reinforcement tension).
Sasa basi, kama jengo likianza kuzidiwa uzito, ila Zege bado lipo imara, Nondo zitaanza kuvutika na kwenye jengo utaanza kuona MIANYA. Hapo ujuwe ni ONYO kuwa kimbia haraka sana ndani ya jengo hilo. Ila kama Nondo bado zipo IMARA ila Zege (Concrete) imeshaanza kuvutwa na ikazidiwa, uzito, basi linakuwa kama vile limegongwa na Kitu kizito kisicho na ncha kali. Linavunjika na kuanguka papo kwa papo (Crush).
Tafadhali muwe MAKINI sana na zege mnalotumia kwenye majengo yenu na si Nondo unazotumia. Hii pia ni kwa wale wanaosema hawakuona Nondo ila Kifusi. Kama Nondo zingeshindwa kazi, walau unapata taarifa mapema kama jengo lililoanza kupinda au unaona jengo linaanza kupata mipasuko, kimbia.
Kwa kuangalia kuwa jengo lilianguka GHAFLA, basi jibu siku zote ni kuwa CONCRETE (Zege) lilizidiwa uzito na kuvunjika ghafla. Angalia Video hii hapa chini:
Video ya Stress kwenye Steel. kwenye Video, unaona kabisa jinsi katikati panavyoanza kuvutika na mwisho chuma kinakatika. Huko kuvutika kwa chuma, kunaweza kukupa muda wa wewe kukimbia, kabla chuma hakijakatika.
Ila kwa jengo kama hilo, unaweza kukuta hata ndondo pia zilikuwa hazifai. Ila Zege ndiyo lilikuwa halifai zaidi.