Kuandika wosia "Last Will"

Grand Canyon

JF-Expert Member
Jan 2, 2020
327
1,000
Ninataka kuandika wosia ili familia yangu isije kupata matatizo huko mbeleni.

Nimeshuhudia familia zilizosambaratika na watu kuuana kisa mzee hakuandika wosia, nataka kuepusha familia matatizo hayo, ila nahisi nikiandika wosia kifo kitapiga hodi.

Kwa nini kuandika wosia kunaleta hofu ya kwamba uko karibu kufa?
 
adden

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
6,211
2,000
kama unayo mali basi igawanye kwa haki.hakikisha ufanyi upendeleo wowote pia usisahau watoto wa nje nao ni watoto wana haki sawa.msimamizi wa mirathi yako awe mtu unaemuamini sana.

Mimi babaangu alikuwa meli kwa kiwango cha pesa alikuwa nacho!lakin sisi waislam kidogo sheria za mirathi zinatubana hasa ukiwa mtoto wa nje..bila ndoa.

Nashkuru kipindi akiwa hai aliniachia elim kuliko wengine hata ilipotokea nikakosa urithi sikujali sababu ya elimu alinipa na kila kitu nilihitaji akiwa hai
 
Auz

JF-Expert Member
Apr 6, 2016
9,431
2,000
Ninataka kuandika wosia ili familia yangu isije kupata matatizo huko mbeleni.

Nimeshuhudia familia zilizosambaratika na watu kuuana kisa mzee hakuandika wosia, nataka kuepusha familia matatizo hayo, ila nahisi nikiandika wosia kifo kitapiga hodi.

Kwa nini kuandika wosia kunaleta hofu ya kwamba uko karibu kufa?
Kifo hupiga hodi wakati wowote, uandike wosia au la. Fanya unaloona litakuwa msaada kwa familia yako.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom