Kuandika wosia au will sio uchuro, watanzania tusiogope

NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Jul 1, 2017
3,032
4,023
Nimekuja kugundua sisi waafrika na watanzania kuandika wosia au will tunaona ni kujichulia kifo, ukweli ni hakuna ambaye hatakufa.Tumeshuhudia mitafaruku mingi hasa mtu mwenye mali akifa huku nyuma anaacha matatizo makubwa kwa walio baki wakati mwingine watoto wa marehemu kudhulumiwa na ndugu wa kike au kiume.

Hili tatizo haliko kwa wazungu sisi bado tuko kwenye ujima. Pamoja na yote naomba niulize machache kwa wajuzi wa sheria za mirathi, na yeyote anayetaka kuuliza maswali apitie hapa uzi huu aulize tuelimishane.

1.Mara nyingi mali alizochuma mwanaume inahesabika wamechuma na mwanamke.Je mwanamke akijenga kwa siri au akafungua mradi kwa siri bila kumshirikisha mume, mali hiyo itahesabika wamechuma pamoja?

2.Wosia unatunzwa bank, RITA, kwa mwanasheria je kuna malipo maalum yanalipwa? Na je ni mara moja au kila mwaka?

3.Wanasema wosia ni siri inafichuka mtu akifa. Je ni vyema kumshirikisha mke ukiandika wosia? (wanawake ni pasua kichwa rejea hadithi ya Esau na Yakobo kwenye biblia)

4.Mara nyingi wosia tumezoea mtu akiugua karibia kufa. Je ukiandika wosia ukiwa huumwi mali zikiongezeka unaweza andika wosia current kubatilisha wa nyuma?

5.Watoto wa kike wana haki kurithi?

6.Watoto wa nje ya ndoa wana haki gani kwenye urithi? Maana ni damu yako watateseka.

7.Ni nani kisheria hakubaliki kurithi?

8.Mahakama ina mamlaka gani kutengua alichoandika mtoa wosia?

Karibuni wanasheria tusaidieni na karibuni maswali tuelimishane mambo haya yanagusa kila mtu.
 
Back
Top Bottom