Kuajiriwa na mafanikio tunayotaka

Kuajiriwa na mafanikio tunayotaka

Kuajiriwa ni sawa na kuolewa lazma umsikilize mumeo ukiambiwa leo lala bila chupi itabidi ukubali, ukiambiwa rudi kinyume nyume lazma utii, kifupi ni kwamba ukipata mtaji sepa watumishi wa umma ambao hawapigi deal wanaotugemea salary wengi akili zao zimedumaa na wanateketea kama mshumaa kwa fultration na pia wanazeeka kwa haraka kupitia maelezo.
 
Hapa umeongea point! mkuu je wale wa sector binafsi itakuaje na je ukisepa life likienda kubana hapo si lazma ukubali kuolewa kwa mara ya pili bila mahari!
 
japo ni chache sana,zipo ajira(vyeo) zinazoweza kukufanya uwe bilionea.....katika nchi zilizoendelea,hususani marekani...
sidhani kama hili linawezekana, unamfahamu bilionea yeyote aliyeajiriwa? yaani kawa bilionea kwa mshahara tu.
 
nachelea kusema mtoa mada hujui unalolisema.

kujiari mtu si maamuzi yake mwenyewe tu bali inategemea ubinifu wa mtu katika mazingira yaliyopo.

nani anatengeneza mazingira ni serikali, kama serikali haijatengeneza mazingira ya wananchi wake kujiajiri hakuna wananchi wenyewe wanaloweza kufanya.

usije hapa na mifano ya marekani kutaja matajiri wa huko bila kujua serikali ya marekani ilichangia vipi katika utajiri wao.

wewe kama akili yako iko sawa utatuambia utajiri wako kupitia kujiajiri ukoje? lakini mbali na wewe binafsi familia yako, ndugu zako umewasaidiaje kujiajiri kujiletea utajiri.

kama wewe tu ndio umejiajiri na una watoto hawana ajira, una ndugu hawana ajira basi yawezekana kujiajiri kwako ni kwa kubahatisha kama kuokota fedha njiani huwezi kujisifu au kumdharau ambaye hajaokota.

serikali ndiyo inatengeneza ajira.

angalia sekita yoyote uangalie jinsi ambavyo mtu ambaye ana mawazo na anaweza kujikusanya kuanza anavyoweza kuanzia chini na kutoka utaona ni ngumu, riski ni kubwa kiasi ambacho hakishawishi au wajasiriamali wengi mitaji inapotea. wasiojua biashara wanasema kuogopa kupoteza mitaji ndio kikwazo cha ujasiriamali lakini nakuambia hakuna mfanyabiashara anayependa kucheza kamali. wanaweka mitaji yao katika biashara zinazoonyesha matumaini.

mfano sekita ya nguo inao uwezo wa kutengeneza wajasiriamali wengi lakini kutokana na kutokuwa na kiongozi mwenye dhamana anayejua majukumu ya serikali asilimia kubwa ya nguo tunazovaa zinatoka asia.

nenda kamchukue mtoto wako au ndugu yako mnunulie cherehani, mnunulie vitambaa atengeneze nguo utagundua bei ni ghali na ubora uko chini kuliko nguo za asia. lakini katika kujenga uchumi serikali inatakiwa sekita ambazo wananchi wake wanaweza kufanya shughuli hizo inatumia kodi kuzui bidhaa za nje. weka kodi kubwa kwenye mitumba, weka kodi kubwa kwenye nguo za nje, ondoa kodi kwenye vyerehani na mashine nyingine za ushoaji utaona jinsi ambavyo nguo za hapa nchini zitakavyoteka soko.

lakini haya ni mpango wa serikali, ambapo kama nchi haina wachumi, nchi haina mfumo wa kudhibiti uchumi kila mwanasiasa anachokifikiri yeye na wapambe wake ndicho wanatekeleza mnabaki kuwalaumu wananchi bila kujua mnachokifanya.

nenda sekita ya kandarasi.

leo hii kumejaa makampuni ya kigeni, utakuta ukienda kuchukua mkopo nje nchi zenye wachumi zinakuwekea masharti makampuni yao ndiyo yaje kufanya kazi ili fedha hiyo ikarudishwe kwao. leo hii kwetu fedha yetu ya ndani ya kodi asilimia kubwa ya kandarasi tunawapa wageni. lakini ni wapi nchi hii mtu anaweza kuanzisha kampuni akapata kandarasi bila kunyoosha mkono? wazalendo wanapokuwa wanapambana na makampuni makubwa ya nje unategemea nini katika mazingira ya kutoa chochote ili upate kazi?

ili uweze kupata wajasiriamali wazalendo katika sekita hii ni kuweka sera za fedha ya ndani ya miradi ya maendeleo kufanywa na wazalendo kwa asilimia kubwa si chini ya 80%.

mfano mzuri ni china, nenda china leo gari ya japani kwa china ni kubwa kuliko gari ya japani kwa tanzania wakati china na japani ni majirani ambavyo katika hali ya kawaida kutokana na japani na tanzania kuwa mbali gari za japani zingekuwa ghali kwa tanzania kuliko china. je unajua sababu? siku zote mnunuzi si mzalendo yeye anaangalia ana shilingi ngapi na kuangalia thamani ya kitu alicho nacho na daima atanunua kilicho bora. hivyo nchi hutumia kodi kuzuia bidhaa za nje kuua soko la bidhaa za ndani. magari yanayotengenezwa china pale pale si mazuri kama ya japani hivyo china inalinda viwanda vyake kwa kuweka kodi kubwa kwa bidhaa za nje.

hivyo ndivyo nchi inavyotengeneza uchumi wake, ndivyo nchi inavyotengeneza ajira, ndivyo nchi inavyoondoa umasikini. lakini kukiwa na viongozi wenye fikra kama za mtoa mada kila siku wanasimama kwenye majukwaa kusema kutengeneza ajira na matokeo yake ni kuongeza nafasi za utumishi wa umma, kukaakwenye majukwaa kuhamasisha wakandarasi wazalendo bila kujua kuwa unatengeza mazingira kwanza, kulalamika uchumi unakua lakini wananchi wanabaki masikini bila kujua kuwa ili kuondoa umasikini ni nchi kujitahidi kupunguza kutemea wazalishaji wa nje.

nchi isiyo na wachumi ndiyo ushuru wa bidhaa uko chini wakati ushuru wa mashine za kuzalishia uko juu kwa lengo la kukataza uzalishaji wa ndani na nchi kutegemea bidhaa za nje. angalia ushuru wa kuagiza mashine za kuzalisha tanzania ni shilingi ngapi alafu angalia ushuru wa bidhaa mbalimbali ni shilingi ngapi ujiulize hivi sisi ni matahira au kama vile tumewaleta wakoloni wakatutengezea mfumo wa kodi ili tuendelee kutegemea viwanda vyao.

au tukisema kujiajiri tuna maanisha nini? maana kila sekita utakayoigusa utagundua kuna mazingira magumu na serikali inayo mambo ya kufanya.

mimi nadhani ili kutengeneza uchumi kila sekita tuunde mamlaka za kuendesha ya kuiendesha ambayo daima inajikita katika kutafiti sekita hiyo na kutafuta mbinu za kuboresha, lakini sekita zote lazima ziwe na chombo cha kuziunganisha na kuzisimamia na chombo hicho ni kuwa na mamlaka ya kusimamia na kudhibiti uchumi. na mawaziri wabaki katika kazi ndogo tu za kusimamia na kuhakikisha watendaji wanafanya kazi zao na kutengeneza dira za mwelekeo wa nchi.

Mkuu umetoa uchambuzi mzuri sana, lakini Watanzania tuendelee kupambana ili tujiajiri. Mkuu ukiangalia nchi yetu, uoni kama serikali ine mission ya kufanya wananchi wake wajiajiri. Mimi nilishangaa pale ambapo Kikwete alipokwenda Brazil, aliwaambia Wabrazil waje Tanzania ili wawekeze kwenye kilimo, aliwaambia kuna ardhi kubwa. Kikwete aliyasema hayo wakati anajua kabisa ukiwezesha Watanzania hasa vijana wanaweza kukaa katika vikundi na kukopeshwa vifaa kazi na Ardhi wakafanya uzalishaji, kuna vitu vya kufanyiwa na wageni lakini siyo hadi kulimiwa chakula. Hivyo nchi hii haina mipango mizuri ya kiuchumi, kazi iliyobaki ni ku copy slogan za nchi zingine kama BIG RESULTS NOW
 
sidhani kama hili linawezekana, unamfahamu bilionea yeyote aliyeajiriwa? yaani kawa bilionea kwa mshahara tu.

soma kwa makini,sijasema mshahara tu,nimesema ajira na mabano nikaweka vyeo...msome Steve Ballmer,(mwajiriwa na. 30 wa Microsoft....kuna benefit nyingine alizopata kama vile employee's shares....(kwa sasa amejiajiri,lakini alishakuwa bilionea before)

Among billionaires who did not acquire their wealth entrepreneurially, many acquired their wealth through bequests, or many are CEOs who, though hired by entrepreneurial start-ups, are not themselves entrepreneurs.
http://icc.oxfordjournals.org/content/22/1/313.full

bonus:Want to be a billionaire? Work for Microsoft, Google, Facebook, or Wal-Mart but not Apple | Computerworld article yote)
[h=3]What Are the People Who Became Billionaires Through the ...[/h]http://www.businessinsider.com/non-greedy-startup-ceos-who-turned-employees-into-millionaires-2014-9

my point is. wapo ila kwa uchache sana...
 
soma kwa makini,sijasema mshahara tu,nimesema ajira na mabano nikaweka vyeo...msome Steve Ballmer,(mwajiriwa na. 30 wa Microsoft....kuna benefit nyingine alizopata kama vile employee's shares....(kwa sasa amejiajiri,lakini alishakuwa bilionea before)

Billionaires

bonus:Want to be a billionaire? Work for Microsoft, Google, Facebook, or Wal-Mart but not Apple | Computerworld article yote)
What Are the People Who Became Billionaires Through the ...

Non-greedy startup CEOs who turned employees into millionaires - Business Insider

my point is. wapo ila kwa uchache sana...
ukishapewa fursa ya kumiliki stocks sidhani kama utakuwa unafit vizuri kwenye maudhui ya uzi huu.
 
ukishapewa fursa ya kumiliki stocks sidhani kama utakuwa unafit vizuri kwenye maudhui ya uzi huu.

THATS AN EMPLOYEE PACKAGE THAT COMES UP WITH BENEFICIARIES BASED ON YOUR PERFORMANCE...MAUDHUI YA UZI NI KUTOKUWEPO MABILIONAIRE WALIOAJIRIWA...NIMEKUBALI NA KUELEZEA FEW EXCEPTIONALS...STOCKS BASED ON THAT HAIMAANISHI ''UMESHAJIAJIRI'' ....I INSIST NI SEHEMU YA ''PACKAGE'' WEWE KAMA ''MUAJIRIWA'' UNAFAIDIKA NAYO...Je unafahamu hata Tz kuna makampuni yanamega sehemu ya shares kwa ''wafanyakazi'' wake?..Sasa mtu akifaidika na hilo hutamuita muajiriwa tena...?
...
Among billionaires who did not acquire their wealth entrepreneurially, many acquired their wealth through bequests, or many are CEOs who, though hired by entrepreneurial start-ups, are not themselves entrepreneurs.
sijui hapo umeelewaje mwenzangu...
 
Hapana! Mi nadhani watu tunazaliwa tukiwa na hurka tofauti na tunakulia kwenye fursa tofauti pia, na ndiyo maana unakuta kuna watu wana mawazo mazuri(Ideas and Creativity) ya kujiajiri ila hawana uthubutu (daring) au mitaji, au pengine ana kila kitu kwao na mtaji pia upo lakini hana uono wa fursa. Mi nadhani mtando (network) ni kitu muhimu sana pengine kwa wale wenye azma ya kujiajiri.

Suala la kuajiriwa pia linategemeana na nature ya kazi au taaluma mtu aliyonayo, kuna aina ya watu tunawahitaji sana kwenye jamii zetu lakini kuwepo kwao ni lazima waajiriwe m.f. Askari, madaktari kwenye public sector, na hata Bill Gates mwenyewe anategemea waajiriwa ili awe na mapato ya kutosha, na pengine kuna baadhi ya wataalamu lazima wapewe maslahi makubwa ili waendelee kuwa kwenye sekta ya kuajiriwa, mtu mwengine pato analoingiza kwenye ajira na mazingira ya kazi ni zaidi ya idea ambayo anaweza kudevelop akaingiza faida. Kwa hiyo cha muhimu unajiajiri kwa maslahi ya nani?
zurich06.jpg

Google Offices.

Tanzania fursa ni nyingi sana, walioziona ni wengi mno na vikwazo vimejaa tele. Kujiajiri ni vita binafsi inahitaji kujituma, kujijima kwa kipato(Saving) au hata usingizi, kukubali kupoteza(failure) na pengine kukabiliana na changamoto kibao zikiwemo alizonazo mtu binafsi zinazoathiri kufikia malengo ("Usifikirie kubadili ulimwengu kama haufikirii kubadili nafsi yako"). Kuwa mjasiriamali si suala la jana haukuwa halafu leo umekuwa mjasiriamali ghafla, bali mjasiriamali ni hatua (daily process) hata kabla ya kuwa mjasiriamali, anglia muda wako wa kulala na kuamka, simu yako unaitumia zaidi kwenye mambo gani, muda gani unoutumia kwenye mtandao na TV, na ni aina gani ya vitu upo interested navyo kwenye mtandao n.k. Inahitaji kujituma kiukweli na siyo kidogo, na siku zote tufikirie ni namna gani tutavusha aidha huduma au bidhaa mipakani ili kuongeza (exportation) pindi mtaji unapokuwa. Ahsanteni.

Imeandikwa na Muakilishi wa (Learnintz.com)
 
cha msingi pesa unazopata zinakutosheleza kwa kila kitu , aliyejiajiri na aliyeajiriwa wote wanataka pesa za kuendeleza maisha yao vizuri, hakuna anayealipwa almasi wote yale yale yale tu,
 
THATS AN EMPLOYEE PACKAGE THAT COMES UP WITH BENEFICIARIES BASED ON YOUR PERFORMANCE...MAUDHUI YA UZI NI KUTOKUWEPO MABILIONAIRE WALIOAJIRIWA...NIMEKUBALI NA KUELEZEA FEW EXCEPTIONALS...STOCKS BASED ON THAT HAIMAANISHI ''UMESHAJIAJIRI'' ....I INSIST NI SEHEMU YA ''PACKAGE'' WEWE KAMA ''MUAJIRIWA'' UNAFAIDIKA NAYO...Je unafahamu hata Tz kuna makampuni yanamega sehemu ya shares kwa ''wafanyakazi'' wake?..Sasa mtu akifaidika na hilo hutamuita muajiriwa tena...?
...

sijui hapo umeelewaje mwenzangu...
nafikiri hao ndiyo wanafaa kuitwa INTRAPRENEURS
 
Kuajiriwa ni sawa na kuolewa lazma umsikilize mumeo ukiambiwa leo lala bila chupi itabidi ukubali, ukiambiwa rudi kinyume nyume lazma utii, kifupi ni kwamba ukipata mtaji sepa watumishi wa umma ambao hawapigi deal wanaotugemea salary wengi akili zao zimedumaa na wanateketea kama mshumaa kwa fultration na pia wanazeeka kwa haraka kupitia maelezo.

ha ha mpaka masharti ya kurudi kinyumenyume?
 
Mfumo wa elimu ya Tanzania hauna faida yoyote katika karne hii kwa sababu haiwezekani kumfundisha mtoto utaratibu wa kutegemea kuajiriwa kwa 100%. Kwani mfumo huo humfanya mtu anapomaliza masomo yake na asipoajiriwa huwa hana plan B Katika ubongo wake wakujua kipi afanye.Na watu wenye akili zetu tuliishia darasa la saba.

Hawa ndio matajiri kumi duniani walioripotiwa na mtandao wa FORBES hivi karibuni hakuna hata moja ambaye ameajiriwa.

1,BILL GATES ($79.2bn) microsoft

2,CARLOS SLIM HALU
($77.1bn) mfanyabiashara mexico

3,WARREN BUFFET
($72.7bn) mfanyabiashara

4,AMANCIO ORTEGA
($64.5bn)maduka ya nguo ya zara

5, LARRY ELLSION
($54.3bn) tekinolojia ya oracle

6, CHARLES KOCH
($42.9bn) mfanyabiashara

7, DAVID KOCH
($45.7bn) mfanyabiashara

8, CHRISTY WALTON
($41.7bn)mumiliki wa mauka ya walmart

9, JIM WALTON
($40.6bn) maduka ya walmart
10, JIM BETTENCOURT
($40.1bn)mfanyabiasha ya vipondozi vya L'oreal

Forbes:Bill Gates ni tajiri zaidi duniani - BBC Swahili

Hawa matajiri wa pesa ni asilimia ngapi ya watu wote duniani?

Ingekuwa vipi kama kila mmoja angejiajiri, nani angesimamia mifumo inayoongoza na kusimamia biashara zao? nani angeshiriki kupeana huduma za jamii kama elimu, afya, ulinzi na usalama? Mbona wanaojiri na walioajiriwa wote wanategemeana sana? Kwa nini tuwatie simanzi wanaoajiriwa?

FaizaFox njoo huku uulize tena lile swali lako la endapo watu huenda shule kujifunza ujinga linajirejea tena hapa.
 
FaizaFoxy
 
Last edited by a moderator:

Huyo Shy land msamehe bure tu, kwa sasa yupo safarini Dar.: https://www.jamiiforums.com/jamii-photos/813353-@shy-land-ndani-ya-dar-es-salaam.html
 
Last edited by a moderator:
Mimi naamini kujiajiri na kuajiriwa vyote vinategemeana. Tukiwekeza kwenye kujiajiri, nani atafanya kazi kwa mwenzie, maana hakuna mwajiri anayekosa mwajiriwa.
 
Mimi naamini kujiajiri na kuajiriwa vyote vinategemeana. Tukiwekeza kwenye kujiajiri, nani atafanya kazi kwa mwenzie, maana hakuna mwajiri anayekosa mwajiriwa.

hakuna aliyekataa kwamba watu wasiajiriwe, lakn kuajiriwa kwako kuwe na kikomo ili uachie watu wengine nao watafute mtaji wakajiajiri.
 
Mfumo wa elimu ya Tanzania hauna faida yoyote katika karne hii kwa sababu haiwezekani kumfundisha mtoto utaratibu wa kutegemea kuajiriwa kwa 100%. Kwani mfumo huo humfanya mtu anapomaliza masomo yake na asipoajiriwa huwa hana plan B Katika ubongo wake wakujua kipi afanye.Na watu wenye akili zetu tuliishia darasa la saba.

Hawa ndio matajiri kumi duniani walioripotiwa na mtandao wa FORBES hivi karibuni hakuna hata moja ambaye ameajiriwa.

1,BILL GATES ($79.2bn) microsoft

2,CARLOS SLIM HALU
($77.1bn) mfanyabiashara mexico

3,WARREN BUFFET
($72.7bn) mfanyabiashara

4,AMANCIO ORTEGA
($64.5bn)maduka ya nguo ya zara

5, LARRY ELLSION
($54.3bn) tekinolojia ya oracle

6, CHARLES KOCH
($42.9bn) mfanyabiashara

7, DAVID KOCH
($45.7bn) mfanyabiashara

8, CHRISTY WALTON
($41.7bn)mumiliki wa mauka ya walmart

9, JIM WALTON
($40.6bn) maduka ya walmart
10, JIM BETTENCOURT
($40.1bn)mfanyabiasha ya vipondozi vya L'oreal

Forbes:Bill Gates ni tajiri zaidi duniani - BBC Swahili

~~Rejea andiko lako na ufanye utafiti wa kina katika fikra na uhalisia wa kimazingira uone mapungufu ya ulicho kiandika.
JE:
1.Nikweli kwamba mfumo wa elimu ya Tanzania hauna faida yoyote na humuandaa mwanafunzi kuajiriwa kwa 100%?Thibitisha hoja yako kwa ushahidi wa kimfumo.
2.Umhimu wa Elimu ni kumfanya msomi kutajirika tu.?
3.Wewe upo namba ngapi katika orodha ya matajiri wasiokuwa na Elimu duniani.?
4.Wajua biashara nyingi za matajiri uliowataja zinaendeshwa na mifumo iliyobuniwa na wasomi.?
5.Kwakuwa kigezo cha kujiajiri ni kutoelimika (yaani kuwa na kiwango duni cha elimu mfano.darasa la saba)kwanini watanzania wengi wenye akili (walio ishia darasa la saba na kujiajiri) ni maskini kuliko wachache wenye elimu walioajiriwa?
~~~~
Baada ya kujibiwa hayo maswali ntarudi kutoa mchango wangu.
 
ego;

Asante kwa maneno mazuri! mfano mimi nafuga kuku wa asili nazalisha mayai. soko limekuwa shida! mtu anaona bora anunue mayai toka Kenya kwa 4000 au 5000, nakuacha mayai ya asili kwa sababu yanauzwa ghali! lakini kama waagizaji wangetozwa kodi kubwa wasinge agiza.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom