~~Rejea andiko lako na ufanye utafiti wa kina katika fikra na uhalisia wa kimazingira uone mapungufu ya ulicho kiandika.
JE:
1.Nikweli kwamba mfumo wa elimu ya Tanzania hauna faida yoyote na humuandaa mwanafunzi kuajiriwa kwa 100%?Thibitisha hoja yako kwa ushahidi wa kimfumo.
2.Umhimu wa Elimu ni kumfanya msomi kutajirika tu.?
3.Wewe upo namba ngapi katika orodha ya matajiri wasiokuwa na Elimu duniani.?
4.Wajua biashara nyingi za matajiri uliowataja zinaendeshwa na mifumo iliyobuniwa na wasomi.?
5.Kwakuwa kigezo cha kujiajiri ni kutoelimika (yaani kuwa na kiwango duni cha elimu mfano.darasa la saba)kwanini watanzania wengi wenye akili (walio ishia darasa la saba na kujiajiri) ni maskini kuliko wachache wenye elimu walioajiriwa?
~~~~
Baada ya kujibiwa hayo maswali ntarudi kutoa mchango wangu.
jibu la 1.ni kweli mfumo wa elimu haumuandai vya kutosha mwanafunzi kujiajiri tofauti na technical schools. mfumo uliopo sehemu nyingi duniani unabase na kumpa mwanafunzi technical skills za kufanya kazi na zikipromote ajira tu.ubaya tena kila unavyozidi soma sana ndio unazidi specialize sehemu fulani tu.hii ni kinyume na ujasiliamali halisi.
kutokana na mfumo huu ni vigumu kumpa mwanafunzi softskills za what to do with my education?. wengi waliofanikiwa sana duniani utakuta kilichomsaidia sana ni background ya kwao .elimu anayopewa na wazazi kuhusu biashara huu ndio msingi mkuu .mfano warren buffet,bill gates, mark zuckerberg wote hawa fuatilia utagundua nyumbani kwao wazazi wao waliwapa kitu cha ziada.ndio maana hata walipodrop out lakini walikuwa na kitu cha ziada baada ya kupata elimu ya darasani kidogo tu. vilevile aliko dangote babu yake na mjomba wake walimpa elimu ya ziada ya kiujasiliamali so sio elimu ya darasani pekee(elimu ya ziada inahitajika kuwekwa mashuleni japokuwa ni vigumu sana kuiweka,vivyo ni muhimu wazaazi pia kuwa na mchango) nashangaza sana baba ni mfanya biashara baada ya kumfundisha mtoto japo kwa saa tu kuhusu biashara utakuta akimfokea "kafanye assignment ,au nenda kalale hayawahusu watoto nyie"
2.umuhimu wa elimu unamchango mkubwa kumfanya mtu kuajirika sababu jinsi unavyoongea elimu ndio zaidi ndivyo unazidi kuspecialize kwenye kitu kimoja ,mfano PHD holder wengi zaidi kuwa mkufunzi au researcher ndio wanapoishia.unakuta mtu ana phd ya entrepreneurship lakini hata duka hana .(hapa wengi wao waliofanikiwa wanakuwa na elimu ya ziada walioipata mtaani au sehemu tofauti kwa kutumia ujuzi wao kawa njia ya kuanzisha huduma au biashara fulani mfano consultation,financial services agency na zinginezo)
3. wewe upo namba ngapi kwa matajiri wasiokuwa na elimu? Mtoa maada hajamaanisha kwamba mtu asiwe na elimu hapana.bali alikuwa anamaanisha utofauti kati ya elimu rasmi na elimu ya ziada ambayo isio rasmi. kuna ambao hawana elimu rasmi kiwango kikubwa lakini wanaelimu isiyo rasmi ambayo imewasaidia .
4. ni kweli biashara nyingi za matajiri zilizokubwa zime kuwa designed na watu wenye elimu rasmi kubwa. hapa kuna utofauti kati ya intrapreneurship v entrepreneurship ,wewe ukiajiriwa na kampuni ni muhmu kama una idea ukampa bosi wako au mkurugenzi akaimplement na kuleta matunda na wewe ukapewa commission kubwa kabisa sababu huna fedha au uwezo wa kulitumia binafsi. lakini muhimu aidi ni mjasiliamali kuwa na kitu chake alichobuni halafu baadae akaanza kununua makampuni au uvumbuzi wa wengine aautumia kama wake(merger and acquisition mfano facebook founder alinunua whatsapp)."Most of richest people employ the people who are more intelligent that they are"
5.mwisho si kila mtu ataweza kujiajiri.bali kila mtu na wakati wake. watu wengi ambao wamejiajiri walikuwa waajiliwa wazuri sana.mfano wengi nawafahamu waliokuwa wahasibu wazuri ,Human resourses wamefungua makampuni ya auditing na consultation makubwa kabisa BAADA YA KUPATA EXPERIENCE KUBWA KABISA(huu pia ni ujasiriamali bora kabisa )
NOTE; si kila aliefanikiwa duniani ni kutokana na elimu,wengine wamerithi utajiri ,pia wengine wanabahati tu.wengine ni wezi tu. na wengine ni mafisadi. kujiajiri moja kwa moja after school si kitu rahisi inabidi uwe vizuri kweli na KILA UNAPOKUWA DARASANI USOME KWA MELENGO NA KILA KITU UJUE KWANINI UNASOMA NA NINI NI MATUMIZI AU UMUHIMU WA UNACHOSOMA UKIRINGANISHA NA MALENGO YAKO. MDA MWINGINE NI PERCEPTION TU ,JINSI UNAVYO PERCEIVE UNAPOSOMA KITU. pia waalimu wenyewe wnapomfundisha mwanafunzi ni muhimu kumfundisha mwanafunzi kama anampa maarifa sio ilimradi afaulu mtihani tu.
lazima watu waajiriwe ili kazi zifanyike.kosa kubwa ni kuajiriwa miaka mingi au almost maisha yote umekaa kuajiriwa tu.
WORK TO LEARN ,DONT WORK FOR MONEY .
Samahani na naomba kurekebishwa kama nimekosea sehemu kimaandishi na nilichoandika.hayo ni maoni tu.