Kuajiriwa na mafanikio tunayotaka

Kuajiriwa na mafanikio tunayotaka

Shy land

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2013
Posts
6,245
Reaction score
2,856
Mfumo wa elimu ya Tanzania hauna faida yoyote katika karne hii kwa sababu haiwezekani kumfundisha mtoto utaratibu wa kutegemea kuajiriwa kwa 100%. Kwani mfumo huo humfanya mtu anapomaliza masomo yake na asipoajiriwa huwa hana plan B Katika ubongo wake wakujua kipi afanye.Na watu wenye akili zetu tuliishia darasa la saba.

Hawa ndio matajiri kumi duniani walioripotiwa na mtandao wa FORBES hivi karibuni hakuna hata moja ambaye ameajiriwa.

1,BILL GATES ($79.2bn) microsoft

2,CARLOS SLIM HALU
($77.1bn) mfanyabiashara mexico

3,WARREN BUFFET
($72.7bn) mfanyabiashara

4,AMANCIO ORTEGA
($64.5bn)maduka ya nguo ya zara

5, LARRY ELLSION
($54.3bn) tekinolojia ya oracle

6, CHARLES KOCH
($42.9bn) mfanyabiashara

7, DAVID KOCH
($45.7bn) mfanyabiashara

8, CHRISTY WALTON
($41.7bn)mumiliki wa mauka ya walmart

9, JIM WALTON
($40.6bn) maduka ya walmart
10, JIM BETTENCOURT
($40.1bn)mfanyabiasha ya vipondozi vya L'oreal

Forbes:Bill Gates ni tajiri zaidi duniani - BBC Swahili
 
Kumbuka hata Bill Gates alianza kuajiriwa....hata wewe usiogope tafuta mtaji kwa kuajiriwa halafu jitegemee
 
kuajiriwa sio tatizo endapo utaitumia kama source ya kupata capital then baadae uimplement mawazo yako ya kibiashara...Ila kama utazeeka ukiwa umeajiriwa bika kua na biashara yyte,bas hilo ni tatizo kubwa..
 
We imewahi kujiuliza walianzaje, ama hali, za famila zao zikoje, ki kifedha,!!!!!, by the way unajua behind ze secret of their succsess kuna nini... Mambo mengine ni neema ya mtu tu mwenyewe...
 
japo ni chache sana,zipo ajira(vyeo) zinazoweza kukufanya uwe bilionea.....katika nchi zilizoendelea,hususani marekani...
 
usikute hata inerviewe hujawahi itwa na hata BRELA pia hupafahamu
 
Hilo ndilo tatizo linaloongeza kiwango cha watu wasio na ajira Tz
 
Hujasema kiwango chao cha elimu ili tulinganishe thamani ya kutokusoma na utajiri wao. Ingawa kuajiriwa ni kweli kunsleta umasikini maana mshahara unakuwa umepimwa kuwa unakutosha wakati kiuhalisia unakuwa haukutoshi. Kila siku mikopo na bills.
 
Wote wakiajiriwa nani atafanya biashara?
 
We imewahi kujiuliza walianzaje, ama hali, za famila zao zikoje, ki kifedha,!!!!!, by the way unajua behind ze secret of their succsess kuna nini... Mambo mengine ni neema ya mtu tu mwenyewe...

Mambo ya "kusema neema ya mtu" ni dalili moja wapo ya uchovu wa akili.
 
ungeweka na maisha ya wazazi wao ingekuwa poa,

mfano; bill gates baba yake mzazi alikuwa mwanasheria maarufu marekani, na mama yake alikuwa kwenye bord ya wakurugenzi wa first interstate bank system na babu yake alikuwa ni raisi wa national bank(first bank of the USA),

carlos slim baba yake mzazi alikuwa ni mfanyanbiashara maarufu sana hasa kwenye kununua hisa za mabenki, na alianza kuwafundisha hao kina carlos slim wakiwa na miaka 12 tu yeye na ndugu zake,

warren buffet baba yakje mzazi ndio alikuwa mfanyabiashara na alikuwa pia yumo kwenye US congress!! unafananisha hizo background na mazingira ya kitanzania kwa mtoto wa mkulima wa nanjilinji ambae kasoma shule ya kata hadi university ya kata?

tolea mfano kwa billionea wa kitanzania then tuwe inspired
 
Kuna tunaopenda kujiajiri ,tazito ni upatikanaji wa mitaji .Hapo ndo kwenye utata.
 
japo ni chache sana,zipo ajira(vyeo) zinazoweza kukufanya uwe bilionea.....katika nchi zilizoendelea,hususani marekani...

Hata hapa bongo mkuu! Kikubwa uwe mpiga dili kazini,usiogope kuwa na ujasiri wa kupiga dili kubwa afu unatema mzigo. Ila kama umeajiriwa sehemu ya kipuuzi bora ujiajiri.
 
Countrywide

don't determine your life from the experience of others! worry is the success's biggest enemy
 
Last edited by a moderator:
nachelea kusema mtoa mada hujui unalolisema.

kujiari mtu si maamuzi yake mwenyewe tu bali inategemea ubinifu wa mtu katika mazingira yaliyopo.

nani anatengeneza mazingira ni serikali, kama serikali haijatengeneza mazingira ya wananchi wake kujiajiri hakuna wananchi wenyewe wanaloweza kufanya.

usije hapa na mifano ya marekani kutaja matajiri wa huko bila kujua serikali ya marekani ilichangia vipi katika utajiri wao.

wewe kama akili yako iko sawa utatuambia utajiri wako kupitia kujiajiri ukoje? lakini mbali na wewe binafsi familia yako, ndugu zako umewasaidiaje kujiajiri kujiletea utajiri.

kama wewe tu ndio umejiajiri na una watoto hawana ajira, una ndugu hawana ajira basi yawezekana kujiajiri kwako ni kwa kubahatisha kama kuokota fedha njiani huwezi kujisifu au kumdharau ambaye hajaokota.

serikali ndiyo inatengeneza ajira.

angalia sekita yoyote uangalie jinsi ambavyo mtu ambaye ana mawazo na anaweza kujikusanya kuanza anavyoweza kuanzia chini na kutoka utaona ni ngumu, riski ni kubwa kiasi ambacho hakishawishi au wajasiriamali wengi mitaji inapotea. wasiojua biashara wanasema kuogopa kupoteza mitaji ndio kikwazo cha ujasiriamali lakini nakuambia hakuna mfanyabiashara anayependa kucheza kamali. wanaweka mitaji yao katika biashara zinazoonyesha matumaini.

mfano sekita ya nguo inao uwezo wa kutengeneza wajasiriamali wengi lakini kutokana na kutokuwa na kiongozi mwenye dhamana anayejua majukumu ya serikali asilimia kubwa ya nguo tunazovaa zinatoka asia.

nenda kamchukue mtoto wako au ndugu yako mnunulie cherehani, mnunulie vitambaa atengeneze nguo utagundua bei ni ghali na ubora uko chini kuliko nguo za asia. lakini katika kujenga uchumi serikali inatakiwa sekita ambazo wananchi wake wanaweza kufanya shughuli hizo inatumia kodi kuzui bidhaa za nje. weka kodi kubwa kwenye mitumba, weka kodi kubwa kwenye nguo za nje, ondoa kodi kwenye vyerehani na mashine nyingine za ushoaji utaona jinsi ambavyo nguo za hapa nchini zitakavyoteka soko.

lakini haya ni mpango wa serikali, ambapo kama nchi haina wachumi, nchi haina mfumo wa kudhibiti uchumi kila mwanasiasa anachokifikiri yeye na wapambe wake ndicho wanatekeleza mnabaki kuwalaumu wananchi bila kujua mnachokifanya.

nenda sekita ya kandarasi.

leo hii kumejaa makampuni ya kigeni, utakuta ukienda kuchukua mkopo nje nchi zenye wachumi zinakuwekea masharti makampuni yao ndiyo yaje kufanya kazi ili fedha hiyo ikarudishwe kwao. leo hii kwetu fedha yetu ya ndani ya kodi asilimia kubwa ya kandarasi tunawapa wageni. lakini ni wapi nchi hii mtu anaweza kuanzisha kampuni akapata kandarasi bila kunyoosha mkono? wazalendo wanapokuwa wanapambana na makampuni makubwa ya nje unategemea nini katika mazingira ya kutoa chochote ili upate kazi?

ili uweze kupata wajasiriamali wazalendo katika sekita hii ni kuweka sera za fedha ya ndani ya miradi ya maendeleo kufanywa na wazalendo kwa asilimia kubwa si chini ya 80%.

mfano mzuri ni china, nenda china leo gari ya japani kwa china ni kubwa kuliko gari ya japani kwa tanzania wakati china na japani ni majirani ambavyo katika hali ya kawaida kutokana na japani na tanzania kuwa mbali gari za japani zingekuwa ghali kwa tanzania kuliko china. je unajua sababu? siku zote mnunuzi si mzalendo yeye anaangalia ana shilingi ngapi na kuangalia thamani ya kitu alicho nacho na daima atanunua kilicho bora. hivyo nchi hutumia kodi kuzuia bidhaa za nje kuua soko la bidhaa za ndani. magari yanayotengenezwa china pale pale si mazuri kama ya japani hivyo china inalinda viwanda vyake kwa kuweka kodi kubwa kwa bidhaa za nje.

hivyo ndivyo nchi inavyotengeneza uchumi wake, ndivyo nchi inavyotengeneza ajira, ndivyo nchi inavyoondoa umasikini. lakini kukiwa na viongozi wenye fikra kama za mtoa mada kila siku wanasimama kwenye majukwaa kusema kutengeneza ajira na matokeo yake ni kuongeza nafasi za utumishi wa umma, kukaakwenye majukwaa kuhamasisha wakandarasi wazalendo bila kujua kuwa unatengeza mazingira kwanza, kulalamika uchumi unakua lakini wananchi wanabaki masikini bila kujua kuwa ili kuondoa umasikini ni nchi kujitahidi kupunguza kutemea wazalishaji wa nje.

nchi isiyo na wachumi ndiyo ushuru wa bidhaa uko chini wakati ushuru wa mashine za kuzalishia uko juu kwa lengo la kukataza uzalishaji wa ndani na nchi kutegemea bidhaa za nje. angalia ushuru wa kuagiza mashine za kuzalisha tanzania ni shilingi ngapi alafu angalia ushuru wa bidhaa mbalimbali ni shilingi ngapi ujiulize hivi sisi ni matahira au kama vile tumewaleta wakoloni wakatutengezea mfumo wa kodi ili tuendelee kutegemea viwanda vyao.

au tukisema kujiajiri tuna maanisha nini? maana kila sekita utakayoigusa utagundua kuna mazingira magumu na serikali inayo mambo ya kufanya.

mimi nadhani ili kutengeneza uchumi kila sekita tuunde mamlaka za kuendesha ya kuiendesha ambayo daima inajikita katika kutafiti sekita hiyo na kutafuta mbinu za kuboresha, lakini sekita zote lazima ziwe na chombo cha kuziunganisha na kuzisimamia na chombo hicho ni kuwa na mamlaka ya kusimamia na kudhibiti uchumi. na mawaziri wabaki katika kazi ndogo tu za kusimamia na kuhakikisha watendaji wanafanya kazi zao na kutengeneza dira za mwelekeo wa nchi.
 
ego mkuu umeongea mengi sana na yote uliyoongea yanaukweli asilimia 100%, na pia nakushukuru sana kwa mchango wango nimepata maarifa mengi na fursa nyingi mno ndani ya maelezo yako.
ubarikiwe sana mkuu ego
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom