Kuajiriwa ama kujiajiri

marandu2010

JF-Expert Member
Aug 7, 2010
1,199
435
Hello wakuu,

Naomba mnichambulie kwa kina katika hili, kati ya kujiajiri na kuajiriwa katika mazingira yetu ya kitanzania bora lipi??

Natanguliza shukurani zangu wakubwa.
 
Ni vizuri umesema katika mazingiora yetu ya Tanzania, kwani majibu yatakua ya uhakika kidogo. Kwa yule mtoto wa mkulima anayetoka kule Mpwapwa ambako hata mvua za mikataba, ukimwambia kujiajiri utampa mtihani utakaomuua kwa BP[blood pressure] lakini ni test rahisi sana kwa mtoto wa kishua kufaulu haka kajaribio.Mbaya zaidi hapa Tz hao watoto wa kishua ni "watoto wao" ambao wachache tu.Labda tu,tuangalie kinachomfanya mwenye nacho kufaniksha mtihani... Jibu ni simple-AMEWEZESHWA kimtaji,kimazingira,bila kusahau network inayoeleweka.So kwa hapa Tz ambako tunaanza na moja, kujiajiri ni mtihani wa form six kwa mtoto wa darasa la kwanza.HAKUNA MAZINGIRA YA KUJIAJIRI,labda haka kautaratibu ka nchi kabadilishwe-yaan mwanafunzi afundshwe kujiajiri na kuwezeshwa atakapomaliza[achana na mikopo benki-huko hawawezeshi wasiokuwa nacho kabisa]
 
Ahsante kwa swali lako zuri.
Ni kweli kuwa kwa mtu wa kawaida kujiajiri Tanzania ni ndoto. Maana mfumo wetu wa uchumi na siasa bado vimejaa umangimeza, Na adui mkubwa ni rushwa amabyo utakwama hata kuapata leaseni ya biashara. Mtaji ni ngoma mbichi maana security itakuwa kazi kwani hata kama una nyumba nyingi hazina Hati yaani title deeds!! Hivyo kujiajiri kama ni kutoa huduma sahau labda mtaji mdogo.
Ila kama wewe unjiajiri na una utalaam basi hiyo yawezekana. Tatizo letu watanzania ni uwoga wa ku take risk. we are not agressive in business. Inabidi na mind set za watu zibadilike yaani tuwe kama Obama ' yes we can'
 
Mkuu nashukuru,,,ila uminitachi zaidi pale ulivyogusia kipengele cha watanzania wengi ni waoga wa kutake risk,,hii na mimi ninaiona,,,kwa sababu japo kuna wanaoanza from top na kuendelea kuwa top au kupanda,,,lakini wengi huanza kutoka 0,1,2,3,4,5.........100,.......mpaka 1000000000000000000000000000000000000.

Lakini mazingira haya yangerekebishwa ingekuwa vyema zaidi....

Asante sana mkuu kwa mchango wako wenye akili..
 
Ajira zenyewe ziko wapi Bongo? Na ukiajiriwa ukawa mtu wa kutegemea mshahara usitegemee kutoka kabisa, labda uwe unapiga dili kidogo kidogo urefu wa kamba yako. Hata walioajiriwa bado wanajiajiri ili hesabu zitimie, watoto waende shule nk.
 
Hili swali limekaa kizushi! Nalifananisha na swali hili enzi za dibeti: Nini bora, Elimu au Pesa?
 
ikiwa hivyo ndivyo debate ni uzushi???? maana nakumbuka tulikuwa tunasafiri masafa marefu na kukutana katika shule fulani moja tukiwa wanafunzi kutoka shule zaidi ya 70 kwa ajili ya debate,ilikuwa kipindi kile niko kidato cha pili,,swali linakuja,tulikuwa tuna fanya mambo ya kizushi??? kuliweka hili katika ratiba na kuahirisha mambo mengine kwa ajili ya hili,,je tulikuwa tunapiga ngumi hewani?? mimi ninaamini debate au mjadala ni njia nzuri sana ya kuruhusu watu kutoa mawazo kuhusu maada husika na hivyo kuleta mafunzo na maarifa ya jambo husika kwa marefu na mapana zaidi..

kwa kusema hivyo,,swali haliko kizushi labda macho yako ndivyo yanavyoona hivyo,,kwa sababu japo karatasi ni nyeupe,,ukimwambia kipofu hii karatasi ina rangi gani atakwambia ina rangi ya giza..mwenye macho atakwambia rangi yake halisi,,lakini haijalishi macho yanaona au hayaoni,,rangi ya karatasi inabaki palepale kuwa ni nyeupe..

huoni vijana wanatoa mchango hapo ulienda shule,,ikiwezekana fuata nyayo zao basi ili tuendeleze mkakati wa kupeana mianga na nuru ili jamii iliyo katika giza zito ikombolewe isitumbukie kwenye mashimo..

asante sana amoeba kwa kadokezo!!

peace love
 
Marandu una hasira sana mkuu, nimecheka ile mbaya!
Unakumbuka enzi za dibeti shule ya sekondARI, Lengo lilikuwa ni kujenga wanafunzi kuweza kujieleza kwa Lugha ya kiingereza!
Hapa wewe naona unaanzisha mjadala tu ambao majibu yako unayo, na unajua kabisa kuwa yanatofautiana kwa mtu na mtu!!
Binafsi sikumbuki mara ya mwisho kufanya kibarua ilikuwa lini!! nina mwanangu, yeye mtazamo wake ni kuendeleza kazi za familia tu, hapendi kumtumikia mtu (mwajiri). Kifupi ni kwamba, aliyekuajiri UNAMZALISHIA anakulipa ujira!! ukijiajiri unazalisha kwa ajili yako,FAMILIA,UKOO na WENYEKUHITAJI!
 
Kujiajiri ni kuzuri kuliko kuajiriwa kama umejiandaa kikamilifu kwa maana kwanza uwe umeajiriwa, ukajikusanyia uzoefu pamoja na mtaji hapo unaweza kufanya kitu.

Hata hivyo bado unatakiwa angalau uwe na akiba ya kukutosha kuishi miaka si chini ya miwili bila kutegemea biashara yako. Mimi niliacha kuajiriwa nikiwa na Mshahara was Shs. 1,500,000 nikaanza biashara yangu (Ya kitaalam siyo Buy and Sell), kwa mwaka wa kwaza, biashara hii iliweza kunilipa Shs, 200,000 tuu kwa mwezi baada ya kodi, mishahara na gharama nyinginezo. Kwa mwenye moyo mwepesi si raisi uache 1,500,000 ukaumize kichwa kwa TShs 200,000. Leo hii ni tofauti kidogo, ofisi imeajiri graduate watano (full time), Part time wawili lakini baada ya kusota miaka mitatu
 
Kujiajiri ni kuzuri kuliko kuajiriwa kama umejiandaa kikamilifu kwa maana kwanza uwe umeajiriwa, ukajikusanyia uzoefu pamoja na mtaji hapo unaweza kufanya kitu.

Hata hivyo bado unatakiwa angalau uwe na akiba ya kukutosha kuishi miaka si chini ya miwili bila kutegemea biashara yako. Mimi niliacha kuajiriwa nikiwa na Mshahara was Shs. 1,500,000 nikaanza biashara yangu (Ya kitaalam siyo Buy and Sell), kwa mwaka wa kwaza, biashara hii iliweza kunilipa Shs, 200,000 tuu kwa mwezi baada ya kodi, mishahara na gharama nyinginezo. Kwa mwenye moyo mwepesi si raisi uache 1,500,000 ukaumize kichwa kwa TShs 200,000. Leo hii ni tofauti kidogo, ofisi imeajiri graduate watano (full time), Part time wawili lakini baada ya kusota miaka mitatu

najua vyovyote vile,,lazima kwa sasa unapata zaidi ya mil 1,500,000 shs kwa mwezi,,lakini bila shaka inahitaji uvumilivu na commitment ya hali ya juu katika hili,pia inahitaji muda kufikia hatua hii.

sasa hivi unaweza kuniambia umepata kitu gani cha zaidi ukiachana na ongezeko la kipato kwa kuacha mshahara huo mnono na kuamua kujiajiri mwenyewe???

vinginevyo nakushukuru sana kwa ushirikiano wako mzuri ulioambatana na mfano halisi wako mwenyewe,,shukurani sana mkuu,,

tuko pamoja..
 
Kaka binafsi nakushauri ujiajiri,suala la kuajiriwa kwa nchi hii ni pasua kichwa,maana hata kama umesoma hakuna anayejali professional,haiingii akilini nchi ina uhaba wa madaktari halafu unamlipa daktari sh, 600,000 kwa mwezi mbuge ambaye pengine kabahatika kupata elimu ya msingi analipwa M 6-12 kwa mwezi kweli hii ni nchi inayothamini professional?huo ni mfano mmojawapo.Mimi kama huyo jamaa aliyetoa mfano hapo juu nilikuwa nimeajiriwa nikifanya kazi na consulting firm ya makaburu fulani hapa town mshahara wangu ulikuwa 1,100,000 take home ukiweka gross ni kama 1.6 million hivi ila mwajiri wangu alikuwa anacharge USD 50 kwa saa kwa uwepo wangu site (nina maana ninapokuwa nasimamia kazi yoyote ya site)You can imagine for a day of 8hrs uwepo wangu site unamtengenezea mwajiri USD 400 na muda mwingi wa kazi zangu ilikuwa site naweza kuwa ofisini kwa wiki moja tu katika mwezi mzima.Nikaanza ndogo ndogo ikiwepo kufungua kampuni,nilipoweza kufungua kampuni japo ilikuwa ya mfukoni sikuwa na ofisi,ofisi ilikuwa nyumbani kwangu nikatoa notice ya miezi miwili huku sijui nitafanyafanyaje mambo yasipokwenda vizuri lakini niliamua na mawazo yangu hayakuwahi kufikiri kufanya kazi za kuajiriwa siku zote nilijipa muda wa miaka mitatu baada ya kutoka chuo lakini haikuwezekana ilipofika mwaka wa nne nikaamua liwalo na liwe nikajitoa muhanga.Mwezi wa november 2009 ndo ilikuwa mwisho wa notice ya ajira yangu,baada ya hapo nikaanza kutafuna akiba huku nikipambana kupata mpenyo wa kazi kwa ajili ya kampuni yangu,sikuweza kufanikiwa mpaka April 2010 nilipopata kazi ya Million 6 ilinipa faida ya milion 2,nikapata tena dili la M 38,kuanzia hapo ikawa ni kazi juu ya kazi to date naongea na kazi ya M 158 mkononi mambo hayakuwa rahisi kwa kipindi ambacho sikuwa na kazi na sikuwa na akiba ya kutosha maana kwa mshahara wangu wa M 1.6 ulikuwa na majukumu mengi hasa familia tegemezi ilikuwa kubwa,lakini nilijitoa muhanga nikaamua kwa ajili ya maisha ya baadae na Mungu akanisimamia,kama una wazo la kujiajiri ni suala la kupongezwa maana najua ipo siku utachukua hatua japo itakuwa ya kuumiza kichwa ila itakusaidia,pia nakushauri usifanye biashara ya kuiga tafuta biashara ambayo hata kama ni ndogo lakini si yenye watu wengi kama profesional yako inaruhusu kujiajiri kupitia hiyo fanya hivyo,maana kwa nchi yetu utakuta PROFESSOR na LAYMAN hawana tofauti hata katika kufanya biashara,maana utakuta layman ana daladala na profesor ana daladala why akawa profesor?kuwa profesor ina maana hata namna ya kufikiri kwako lazima kuwe tofauti na watu wengine profesor anatakiwa kutumia elimu yake aandike maandiko watu wampe pesa aanzishe kiwanda,au ufugaji mkubwa au kilimo chenye tija lakini utakuta hatuna wasomi wa aina hiyo. Jiyoe muhanga kiongozi utaona mafanikio,hata kama utaanza kwa kununua jiko mahali ukaange chipsi lakini ni biashara yako usikaange chipsi kama wengine we ongeza manjonjo kidogo ili uibe wateja toka kwa jirani yako hivyo ndo tunatakiwa kuwa watanzania,ubunifu kidogo tu unakuuza. Nitakupa mfano mwimgime **** juice ngapi zinatengenezwa hapa Tanzania na za bei rahisi tu?lakini angalia DELMONTE ilivyoteka soko la juice hapa Tanzania japo ni juice ghali lakini packaging yake inaiuza bila mgogoro.Anza sasa kuchukua hatua.
 
Duuuu! Hii nimeipata vizuri sana,,hizi mimi ninaziita dhahabu,,wakati mwingi mimi hupendelea ideas nzuri kama hizi kuliko hata pesa,,kwa staili hii matumaini na imani inazidi kupanda na hakuna shaka nitafanikiwa tu..

Asante sana mkuu MANYUSI
 
Kujiajiri ni kuzuri kuliko kuajiriwa kama umejiandaa kikamilifu kwa maana kwanza uwe umeajiriwa, ukajikusanyia uzoefu pamoja na mtaji hapo unaweza kufanya kitu.

Hata hivyo bado unatakiwa angalau uwe na akiba ya kukutosha kuishi miaka si chini ya miwili bila kutegemea biashara yako. Mimi niliacha kuajiriwa nikiwa na Mshahara was Shs. 1,500,000 nikaanza biashara yangu (Ya kitaalam siyo Buy and Sell), kwa mwaka wa kwaza, biashara hii iliweza kunilipa Shs, 200,000 tuu kwa mwezi baada ya kodi, mishahara na gharama nyinginezo. Kwa mwenye moyo mwepesi si raisi uache 1,500,000 ukaumize kichwa kwa TShs 200,000. Leo hii ni tofauti kidogo, ofisi imeajiri graduate watano (full time), Part time wawili lakini baada ya kusota miaka mitatu
Niliwahi kusoma kitabu kimoja cha mambo ya ujasiriamali ameandika mfilipino mmoja (sikikukmbuki title, nitajaribu kukitafuta nishee) anasema kama umeajiriwa si vema kuacha kazi kwenda kujiajiri. Unatakiwa ujiajiri wakati unaendelea na kazi mpaka huo mradi wako utakapoweza kukupatia mara mbili ya mshahara wako ndo uache kazi ukasimamie mwenyewe mradi wako ili kuongeza kipato zaidi.
 
wazo zuri,tunakisubiri kwa hamu sana kitabu hicho ili tupate mawazo zaidi,,asante sana mkuu balozi
 
ubunifu mdogo sana Tanzania,wafanyabiashara wengi sio wasomi na wasomi wengi hawapendi kufanya biashara.
Jiulize serikali inafanya nini kuimprove bizness startup enviroment!
 
ubunifu mdogo sana Tanzania,wafanyabiashara wengi sio wasomi na wasomi wengi hawapendi kufanya biashara.
Jiulize serikali inafanya nini kuimprove bizness startup enviroment!
hilo pia neno, fikiria mimi ni msomi,unanishauri nikimbilie wapi kati ya haya mawili???? na ikiwa nitachagua A au B,nifanye vipi ili nifanikiwe zaidi???

asante sana mkuu kwa kidokezo hicho halisi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom