Kuacha mke mwenye watoto

UWOGA=UMASKINI

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2013
Posts
2,400
Reaction score
1,019
Kuna madhara gani ambayo anayoweza kumbana nayo mwanaume kumwacha mke mwenye watoto anayoweza kuyapata kiuchumi na kijamii inshort madhara kwa ujumla kisaikologia nk.
 
kiuchumi nakupeleka ustawi tunakata mshahara juu kwa juu ... kingne kutesa watoto, kingine kuwa na matumizi yasiyoyalazima kama kuhonga wapenzi
 
kiuchumi nakupeleka ustawi tunakata mshahara juu kwa juu ... kingne kutesa watoto, kingine kuwa na matumizi yasiyoyalazima kama kuhonga wapenzi
Natamani kukuacha leo hii...!
 
Kuna madhara gani ambayo anayoweza kumbana nayo mwanaume kumwacha mke mwenye watoto anayoweza kuyapata kiuchumi na kijamii inshort madhara kwa ujumla.

Pole kwa yaliyokufika.

Kuacha mke ilihali mnawatoto mara nyingi kunaongeza shida.

Hata mkiachana itabidi uendelee kukea watoto wenu.

Ukiishi na mwanamke mwingine naye anawezakuwa na hisia kwamba kwakuwa unalea watoto na mke wa zamani yamkini mkawa mnajikumbushia mambo fulani.

Watoto wako wakiumwa hata kama ni usiku menene ukijushwa basi utakayekuwa unaishi naye jiandae kwa maneno.

Baadhi matumizi yanaongezeka kwa wanawake wa nje.

Kwa watu wa bara familia itakudharau.

Kama ni muumini wa kanisa kuna namna utakuwa unatengwa.

Fanya maamuzi upya. Tafakari tena.
 
Mmh,hapa nadhani inategemea wewe unawaza nini kutokana na huyo mtalaka wako. Athari zote ziwe za kiuchumi,kisaikolojia na kimapenzi,itategemea sana kile ulichonacho kichwani. Kuna ndoa zingine mkibaki pamoja kwa kisingizio cha watoto,watoto wataathirika zaidi kuliko mngeachana. Mfano familia yenye magomvi,kupigana na kutukanana hadharani watoto hawatabaki salama! Hawa wanaojiita mbwa mwitu au panya road,ukifuatilia familia zao wengi wao wamelelewa na wazazi wote 2 lkn wazazi hawakutimiza wajibu wao.
 
Dhara kubwa la kuacha mke (yeyote hata asie na mtoto) Ni kukosa guarantee mbunye kitendo kitakachokufanya udise hovyo hovyo na possibility kubwa ya kudondokea pua.
 
Ya nini umuache mkeo,wakato uliapa hamtotengana mpaka kifo?Tena ana watoto....HAPO HESHIMA ITASHUKA kwa mke au mume inategeana na sababu
 
Hivi bado kuna wanaume wanaotelekeza familia zao??
 
Hivi bado kuna wanaume wanaotelekeza familia zao??

Bulldog;
Haya ni mapya kwako?? Tatizo ni ahadi hewa za wana siasa wetu. 2005 tuliambiwa tutapata maisha boraaa mpaka tujisahau. Tukawaamini, we acha tu. Wanaume wakachangamkia dili hilo, wakawazalisha wenzi wao kinyama atiii. Piga mahesabu, kila mwaka mtoto leo una wangapi?
Maisha yamekuwa tight ile mbaya. Suluhisho, ni kuomba ushauri humu jf ka huyu jamaa. Maisha yesha mshinda huyu. Badala ya maisha bora akapata bora kuishi tuuu. Mpe ushauri acha kumnyanyasa mwenzio yamemfika shingo maji.
Amengojea yale mabilioni ya JK mpaka leo hakuyaona wala hajui yalikopelekwa, 2010 akaambiwa wazi, afunge mkanda. Duh! too late. keshazalisha viumbe 5 na mke ni 6. hesabu ngumu hii. Dawa kuwaacha tu. JK atajua mwenyewe kwani kawaahidi ahadi hewa wanaume
 
Kuna madhara gani ambayo anayoweza kumbana nayo mwanaume kumwacha mke mwenye watoto anayoweza kuyapata kiuchumi na kijamii inshort madhara kwa ujumla.

Sababu za kufanya hivyo ni zipi? Je, ni watoto wake wa kuzaa - proven by DNA?
 
Inategemea sababu za kumuacha na mtu mwenyewe uliemwacha. Kuna wakati hasara hakuna bali faida. Kiuchumi ;mara nyingi matumizi au gharama za maisha huongezeka. Kina mama wanaweza kubajeti vzr. Kijamii ;suala hili hua halieleweki vzr kiasi kwamba utakumbana na maswali yenye kukukosesha "furaha ya moyo."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…