Ku fake maisha ni chanzo cha maumivu katika mapenzi

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
26,792
58,674
Wengi huumizwa na mapenzi kwani hao wapenzi wao wamewapata kwa ku fake maisha.. mtu anajimwambafai kuwa hela zipo,burudani ndio kisima,shida hazijawahi kusumbua wakati kiuhalisia si sahihi!.

Ndugu kaa ukijua lazima pia utapata mpenzi fake!.. atakachofata kwako ni u fake wako ila atakapo gundua uhalisia wako ndio mwanzo wa kukengeuka! Nawe huachwa taabani na kuishia kulaumu jinsia husika.

Inaaminika jinsia ke ni wagumu kuwapata hasa usipo fake maisha,na huo ndio ukweli lakini nashauri njia ya kufake maisha itumike kumpata ambae si wa kuwa mke au mume!! Utaachwa tu siku uhalisia wako ukiwa bayana..

Jambo hili la ku fake maisha si tu litakupatia mpenzi fake bali hata marafiki fake.
Mke au mume halisi ni yule anaekupenda kwa uhalisi wako, hivyo hivyo marafiki halisi pia si wale wa ku fake nao maisha.
 
Ni kweli, hivi mtu unataka mwenza wa kudumu then unafake ili iweje? Ndio maana mimi kosa la kunidanganya huwa halisameheki maana najua wewe unapita njia tu umekatiza kwangu kuchimba dawa uendelee na safari... Maana haiwezekani udanganye jambo ambalo unajua kadri tunavyoendelea nitajua tu ukweli
 
Kwanini uigize....? Ishi maisha yako....
Mkuu haujui mapenzi yanaweza kukufanya uigize maisha.. unaazima nguo kwa masela,gari,gheto ili tu umpate kimwana anaezingua.. ukienda na makinyelamumo walahi msamiati kutoswa hauta kuepuka😂😂 ku fake,fake kwa asie mume au mke fake kwa yule wa kula then mbele.
 
Kwanini uigize....? Ishi maisha yako....
Kwanini uigize, ishi maisha yako/
Mimi usiniulize, kwani ni wajinga kazi yao/
Mpenzi mueleze, uhalisi wa maisha yako/
Kamwe usimbeze, onyesha hisia zako/

Watu hawajiamini, ndio maana wanafake
Mwenzio muamini, penzi halita feail
 
Kudanganya huwa kuna gharama zake.
Kipindi cha miaka kadhaa iliyopita nilidanganya jina kwa mwanaume ambaye nilikutana nae.

Siku zinavoenda akanipenda, na Mimi nikawa naanza kumpenda ila tatizo sasa hata jina lenyewe analoniita nilimdanganya. Kuanza kumwambia ukweli nashindwa. Maana alivokuwa analipenda jina langu la uongo , nikaona haifai.

Nilichofanya ni kulipa gharama za kumdanganya, nikamwambia kwamba simpendi na asinitafute. Nikamblock.

Siku akaja akajua jina langu la kweli akaja niuliza Paula mbona ulinidanganya? Nikamwambia kwani sababu hauijui? Nilikudanganya kwa sababu sikukupenda.

Akaanza kuni approach upya kwa kutumia jina langu la kweli, nikamkubali haraka haraka kwa kuwa na Mimi nilikuwa nimeshaanza kumpenda, lol
Nilihisi nimetua mzigo mzito sana nilikuwa nimeubeba.
 
Mkuu, naona unazuka sana m-buyu. Ebu ngoja wanaume wa huko Daslam waamke, watakushukia kama mwewe...teh
 
kudanganya nisehem yaku-aproach na kila mwanaume hufanya bt tumia uongo unao akisi uhalisia wa maisha yako....
usijifanye unacho akat huna hapo utasuffer tu one day
 
Back
Top Bottom