Kotoka Diamond Jubilee: Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa DCB, Wilson Kabwe Aliliwa!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,669
119,288
Wanabodi.

Niko kwenye mkutano mkuu wa wanahisa wa Benki ya Wananchi wa Dar es Salaam, DCB unaendelea hapa ukumbi wa Diamond Jubilee, Mkutano huo ilisimama kwa dakika moja, kumlilia/kumkumbuka aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji aliyetumbuliwa, Wilson Kabwe ambaye alikuwa ni mmoja wa wakurugenzi wa Benki hii.

Kwa vile sikualikwa kudisclose kinachoendelea kwenye mkutano huu, naomba kuishia hapa.

Asanteni.

Pasco
 
Kila mfanyakazi wa serikali ni mchafu ila nje ya system ni wasafi Sana. Rest in perfect and everlasting peace KABWE.
 
Pasco hii sasa inaonyesha jinsi ulivyokuwa mnufaika kwa kufanya propaganda kwa watuhumiwa.Ikumbukwe tu Kabwe alikuwa mjumbe wa bodi DCB kwa wadhifa wake wa Ukurugenzi wa jiji lakini sio kwa merit nyingine.
 
Apumzike kwa amani, ila hatuta msahau kwa jinsi alivyo shiriki kuikanyaga demokrasia jijini mwanza, na ktk hili bado hatuja msamehe!
 
Nani ana ile clip au maneno aliyoyatamka Ole sendeka kula kwenye mazishi ya Kabwe?
Alisema kabwe alituhumiwa tu.. Na akatolea mfano wa Mkapa. Kuwa mkapa alishawahi kusimamishwa na Nyerere
 
RiP Kabwe! DCB naona sasa ni muda kujitanua zaidi na kujipambanua zaidi na zaidi na product zaidi na mikopo kwa wajasiriamali w jijini!
 
Pasco heading yako haijakaa sawa!
Ungesema wanahisa wamlilia Kabwe, lakini kwa kusema aliliwa ni sawa na kuelewa kuwa alitapeliwa(kuliwa kete kimjini)
 
Back
Top Bottom