Samahani wakuu, kwani MpendaZoe ipi mpya tena? sijaingia humu ndani all th day :msela:
Nape nilikutahadharisha mapema, Acha kung'ang'ania kutaka kuvaa koti la Dr. Slaa hukunielewa. Oh Dr.slaa ni fisadi, Dr Slaa akakataa kukuvalisha Koti lake akaamua kukupatia koti jepesi kabisa kutoka kwa Mpendazoe. Looooh, unahema nalo karibia kuzimia, Je Docta wa Ukweli angekuvalisha la kwake si ungekufa?
Docta wa Ukweli alishawavalisha baba zako mpaka leo wanashindwa kulivua na ndilo lililosaidia hata wewe kupata nafasi uliyonayo. Sasa ndugu yangu, ukiweza kulivua la Mpendazoe, utapewa lingine na si la Dr. Slaa usije ukatufia bure.
Hili shairi, mnanda, twist ama taarab ??
mpendazoe kaua kabisa,kasambaratisha chama!
Yaani ingawa wengi walimlaum kwamba hayo sio mambo ya msingi
ya kuongelea saivi (na kweli sio),ila ni mazuri sana kwa magamba kujikuna day n night!
HADI MUWASHO UKIISHA,2015 hawajaleta hata mtumbwi ziwa victoria,kigoma itakua kama wapi sijui
Yote majibu mkuu, chagua lililosahihi zaidi.:smow:
Kwa mtazamo wangu nahisi huyo ni mtu mmoja anatumia majina tofauti. Wote walianza kuandika kwenye magazeti husika wakati wa uchaguzi mkuu huyu wa kwa Mwanahalisi alikuwa anajiita mwandishi maalum. Huwa sikosi kuwasoma hawa jamaa kwa sababu huwa nahisi kama anayeandika ni Salim Ahmed Salim, Joseph Butiku, Warioba au Fredrick Sumaye. Ni watu wanoonekana wako karibu sana na wenye "nji hii"Kwenye gazeti la Raia Mwema kuna jamaa anajitambulisha kama "Msomaji Raia"
Kwenye gazeti la MwanaHalisi kuna jamaa anajitambulisha kama "Kondo Tutindaga"
Sifa kuu ya hawa waandishi wawili wa magazeti hayo tofauti, ni kuwa wote wanaijua sana CCM.
Sanasana wanamjua sana mwenyekiti wa CHAMA.
Katika wiki hii wote wamezungumzia umuhimu wa "wahaini" wa chama kutemwa,
HApo kwa mbali nikaanza kuona hatima Blaza Nape, nikacheka tu!
Hivi koti likikushinda linakudhuru vipi, linakuangusha? Misemo ya kibongo mingi kwangu hai make sense.
Anyhow, bomu la Mpendazoe halijawa na devastating, lasting impact kwa Nape, labda amejisikia aibu mbele ya kina Kikwete siku mbili tatu, lakini hakuna atakae dai, kwa mfano, ajiuzulu kwa sababu alitaka kuhama chama. Scandle hazimuangushi mtu Tanzania.
Lakini kikubwa zaidi kuhusu udhaifu wa Nape ni kwamba kwa kweli toka aingie kumekuwa na chaos rather than calmness kwenye chama, kutokana na motormouth yake magazetini, mitandaoni, majukwaani, na mabarabarani. Kazi inamshinda.
hilo ni neno moja au mawili ??