JACKLINE CELESTINE KITALE
Member
- Jul 29, 2021
- 81
- 158
- Thread starter
- #61
Duh...nilidhani humu ni sehemu ya watu wenye mtazamo chanya. Ila Kama wanavyosema, kwenye msafara wa mamba na kenge wamo.Kwanza wewe sio muoaji bali muolewaji,Hauna jeuri ya kuchagua mwanaume kana kwamba wewe ndiye muoaji.Pili anayeamua ndoa ni mwanaume sio wewe mwanamke,kama ni makosa anafanya mwanaume kwa kukuoa wewe sio kwa wewe kuolewa naye! Wewe kazi yako ni kusubiri kuolewa yaani kukaa kusubiri mwanaume atakapofanya maamuzi kuoa ndipo akuoe!
Ila sikiliza Ni kwambie kitu, maamuzi ya kuingia kwenye ndoa Ni ya watu wote wawili na sio ya mwanaume peke yake, na ndio maana uanweza kwenda kutoa posa na ikakataliwa na mwanamke mwenye kwasababu zake alizokuwa nazo.
Ila ukiendelea na huo mfumo wako dume hadi kwenye familia utaenda kuiharibu. Na hata Kama wewe Ni mwanaume hakuna mwanamke anaye taka mtu ambaye hawaelewani siku zote, na anyejiona hakosei eti kisa Ni mwanaume.