Kosa langu li-wapi?

Kosa langu li-wapi?

King''asti asante kwa ushauri. Lakini kumbuka yule yule binti ndiye alikuwa karibu sana na mimi kiasi kwamba nilimueleza mahusiano yangu. na nilipopita kwenda Bagamoyo nilikuwa nakwenda likizo na mchumba wangu na wote walilitambua hilo. Je hiyo haikutosha wao kuelewa kuwa hakukuwa na uhusiano kati yangu na yule baba?
 
Last edited by a moderator:
Labda kitendo cha kufungia safari msiba ndo kilimstua kuwa sasa umemuwin mumewe, na wanae. Na unatafuta umaarufu kwa ndugu wa mumewe.

Kumbuka ameishi miaka mingi kwenye hiyo familia, na atakuwa ameshagongana na baadhi ya ndugu wa mumewe. Labda alihisi unajiuza ukubalike.

Honestly, kama ni mie nafadhiliwa hapo ningeweka kadistance flani kati yangu na baba mlezi

Nashukuru kwa ushauri wako
 
Kuwa makini ukiendelea kujifanya mzungu na kumpuuzia huyo mama unaweza pigwa kipapai
 
::
Kwa maelezo yako huna kosa lolote.
Na kama dhamira yako inakupongeza kwa uaminifu huo zidisha uaminifu huo zaidi.
::
Ombi langu kwako,,usithubutu kumtafuta huyo Mzee umpe zawadi ya mwili wako kama shukrani yako ya juu kabisa kwa wema aliokutendea.Ukifanya hivyo uaminifu wenu uliopita utakuwa hauna thawabu.Kama utakosa zawadi ni heri utafute mtoto asiyejiweza umtendee ulivyotendewa!
=
 
Ndugu yangu Mbu, Unataka kusema tunapotaka kuwasaidia watu tuangalie jinsia? Yule mama kama alikuwa ana doubt na mie angelifanya uchunguzi ili kupata ukweli na sio kukurupuka.

🙂 haya, nijibu haya kwanza;...Huyo mama Hajakurupuka kama unavyotaka mdhania, "amekuvumilia" muda gani vile? ....anayajua mapungufu ya mumewe ndio maana akachukua hatua...

Kwanini unahisi kwamba malipo ya fadhila yangeishia kwenye mapenzi?

1. ....alipata kukwambia Anakusaidia ili iweje?

2......ushawahi jiuliza kwanini anakufadhili na kukukaribisha kwa familia?

3......unayalindaje mahusiano yako sasa na huyo baba mlezi bila kumkwaza huyo mama?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu ndio dunia yetu ilivyo siku hizi. Ubinadamu wa kusaidiana umepotea kabisa. Huyo Baba baada ya kusikia historia ya maisha ikawa imemgusa na kwa kuona alikuwa ana uwezo wa kukusaidia ili kunyanyua kiwango chako cha maisha basi hakusita kufanya hivyo. Akaamua na kukutambulisha nyumbani kwa mkewe na watoto ili kuhakikisha kwamba hakuna lolote atakalolifanya kwako kwa kifichokificho, lakini kwa kuwa dunia yetu siku hizi ni tambara bovu basi hitimisho la kwanza la Mama mwenye nyumba ni kwamba kulikuwa na mahusiano ya kimapenzi kati yako na yule Baba kitu ambacho hakikuwa na ukweli kama ulivyoelezea.

Mama angeweza kabisa kufanya uchunguzi kufikia hitimisho la kweli na kwa kuwa wakati mwingine ulikuwa ukisafiri na mchumba wako kwenye familia ya huyo Baba hiyo ingesaidia pia kuonyesha hakukuwa na mahusiano ya kimapenzi lakini ndiyo hivyo tena. Si ajabu hata ungekuwa Mwanaume yule mama bado hitimisho lake lingekuwa ni negative kwamba Mumewe amejiingiza katika mahusiano ya jinsia moja vinginevyo haiwezekani kumpa msaada mtu ambaye hauna nasaba naye hata ya kuunga na gundi. Pole sana.

Ndugu yangu Mbu, Unataka kusema tunapotaka kuwasaidia watu tuangalie jinsia? Yule mama kama alikuwa ana doubt na mie angelifanya uchunguzi ili kupata ukweli na sio kukurupuka.

Kwanini unahisi kwamba malipo ya fadhila yangeishia kwenye mapenzi?
 
Nashuku sana kwa ushauri ndugu BAK, Ningelikuwa na uwezo wa kumfanya yule mama aamini kuwa hakukuwa na kitu chochote nyuma ya pazia ningelifurahi sana. Lakini uwezo huo sina.
Hii issue imekuwa ikinisumbua sana kichwani.

hapo kwenye Red Nashauri ungeachana naye kwani yeye Mzee kala hasara kwa pesa alizokusomesha ni bora angejenga kibanda hapa Dodoma, au huko Moro au Tabora kwani huwezi kulipa fadhila kwa gharama km hizo. Na Mama aliona mapenzi yanashuka toka kwa Mumewe na huko Tabora ndio kwa wakwe huwa kuna Vikao vya SIRI sana vya Unyumba na watoto hata kugawana mali za Urithi na kukabidhiwa watoto wasio rasmi

Unajua kwa Story za km (fiction) za CHAI CHUNGU ni nzuri sana ingeendelea hasa leo Week-end jE MLIPOKUTANA AU KUWASILIANA inaedelea...........................................
 
Last edited by a moderator:
kazi ipo.

Ngumu kumesa, kama anakufadhili badi akuadopt uje uishi kwetu mazima.
 
Dada yangu sijui wala siwezi kujua kama kulikuwa na tatizo katika familia yake. Lakini kumbuka kuwa mie nilikuwa naishi mbali sana (nimetumia miji isiyohalisi ili kuwaelewesha) kiasi kwamba baada ya yule baba kupata uhamisho ilinichukua takribani mwaka mzima ndipo nikafunga safari kwenda kumsalimia.

Unampa huyo mama big up kwa kukurupuka au? Je ningemwambia anipe ushahidi wa mahusiano yangu na mumewe je angeweza?

Mydia ... take it easy, na kama unaweza kusoma alama za nyakati muda huu ndio wa kujiweka mbali na watu hao.

mshukuru Mungu kwa fadhila ulizopewa na mwombee huyo Baba, huyo mama alijitahidi sana kuvumilia mahusiano ya mumewe na binti mbichi asiyekuwa na undugu naye hata chembe na bado kipato cha familia kinahusika kukugaramia elimu, kisa usamaria wema lol.

But ... kikubwa kinachomtesa sio hata hizo garama ni WIVU wa mapenzi .. huenda that day hata kuna majibizano yali raise baina yao na chanzo ukiwa ni wewe na ndo sababu mawasiliano yakaharibika dk za mwisho. Take it easy n move on with ya life.
kingasti pia amejaribu kuelezea na kutoa mfano on the other side of the coin... SI RAHISI KAMA UNAVYOFIKIRI.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu ndio dunia yetu ilivyo siku hizi. Ubinadamu wa kusaidiana umepotea kabisa. Huyo Baba baada ya kusikia historia ya maisha ikawa imemgusa na kwa kuona alikuwa ana uwezo wa kukusaidia ili kunyanyua kiwango chako cha maisha basi hakusita kufanya hivyo. Akaamua na kukutambulisha nyumbani kwa mkewe na watoto ili kuhakikisha kwamba hakuna lolote atakalolifanya kwako kwa kifichokificho, lakini kwa kuwa dunia yetu siku hizi ni tambara bovu basi hitimisho la kwanza la Mama mwenye nyumba ni kwamba kulikuwa na mahusiano ya kimapenzi kati yako na yule Baba kitu ambacho hakikuwa na ukweli kama ulivyoelezea.

Mama angeweza kabisa kufanya uchunguzi kufikia hitimisho la kweli na kwa kuwa wakati mwingine ulikuwa ukisafiri na mchumba wako kwenye familia ya huyo Baba hiyo ingesaidia pia kuonyesha hakukuwa na mahusiano ya kimapenzi lakini ndiyo hivyo tena. Si ajabu hata ungekuwa Mwanaume yule mama bado hitimisho lake lingekuwa ni negative kwamba Mumewe amejiingiza katika mahusiano ya jinsia moja vinginevyo haiwezekani kumpa msaada mtu ambaye hauna nasaba naye hata ya kuunga na gundi. Pole sana.

.....lol, kaka .....sarcasm zimezidi nawee, kha?

Swali la The Boss umeliona? Mimi nimezisoma alama za nyakati....

...akawa mteja wetu mzuri kiasi kwamba hawezi kumaliza siku mbili hajaja kufanya kazi zake. Hata kama hana kazi ya kufanya alipita kutusalimia. Yule baba alinipenda sana .....

"Grooming"....!!!

Huyo baba anajenga mazingira mazuri si kwa mlengwa pekee, bali hata kwa mpenzi wa mlengwa, na familia yake.
BAK, haya mambo yanatokea na yamezidi sana miaka hii. Wanaume wanahonga nyumba, gari na mengine mengi yenye thamani ya mamilioni ya fedha kupata wanachokikusudia.

Dada'ngu huyu is either too naive, au too smart penye "kula na kipofu." 😀
 
Last edited by a moderator:
Wewe ulipaswa kujua pa kuishia, na hauwezi kumlaumu yule binti. By the way, binti anaweza asiwe na tatizo, mama ndo amatatizika.

Usiongelee mchumba, siku hizi watu wana waume ana wake na still wanaenda kwa small house na kujikawaidisha. Kama haujawahi kualikwa na mwanaume anaekutolea macho kwenda hospitali kumuangalia mkewe akiwa mgonjwa, baso wewe bado ni binti!
King''asti asante kwa ushauri. Lakini kumbuka yule yule binti ndiye alikuwa karibu sana na mimi kiasi kwamba nilimueleza mahusiano yangu. na nilipopita kwenda Bagamoyo nilikuwa nakwenda likizo na mchumba wangu na wote walilitambua hilo. Je hiyo haikutosha wao kuelewa kuwa hakukuwa na uhusiano kati yangu na yule baba?
 
Last edited by a moderator:
Nitakuwa muwazi kabisa kwako. Ulijiingiza sana pua yako pasipohusika. Tungekuwa tunafahamiana ningekuonya hili toka mwanzo manake ningeliona ujio wake. Kulala kwa watu is deep!

Ni sawa kutambulishwa kwa familia nzima. Lakini habari ya wewe kuja kulala nyumbani kwangu wiki nzima. Na uje kulala kwangu tena! Ingekuwa sawa kwenda kusalimia na kula dinner ama lunch tu, lakini sio kulala. Na kilichomuumiza zaidi nadhani ni mwanae kuja na mjukuu kukaa kwako wiki.
Mbu, asante kwa kuwa honest. Viatu vya huyo mama vingem'bana mwanamke yeyote. Hata tuwaulize wanaume humu jf:

mkeo anamfadhili kijana muda wote, na hatimae unakutana nae na unaambiwa alilala kwako wiki wakati haupo. Japo na wanao walikuwepo. Ukimuangalia kijana ana six pack, na wewe kitambi kiko mahali pake!
Thank you... Baadhi yetu tunakua too naive nankusahau tuko duniani

kusema ukweli nimekereka sana na huyo mleta mada... She just cant know her limits
 
Naomba nimtetee kwa hili, angeweza kabisa kumnyima. Japo ingevunja ubaba. Mtu ukishaamua kuchora mstari kwenye moyo wako sidhani kama inakupa shida. Na hapo wanaume ndo mnapokoseaga na kuharibu urafikia. Unamsaidia mtu na kujihakikishia hapa hachomoki. Unakuja kichwa kichwa na kusababiaha mtu kutoka nduki.
Pole sana,
swali hapa ni je kama baba mlezi angeomba?
ungekuwa na ubavu wa kumnyima?
 
Hahaha, typical wife reply!

Kama ni mimi huyo mama, nahisi ningekuwa comfortable zaidi kama toka mwanzo hajaanza kumsaidia angeniambia. Na ningeshirikishwa waziwazi juu ya matumizi yake etc. Na ukiangalia mama aliuliza 'nani kakuambia kuhusu msiba?!'. Binti anaambiwa about msiba na hajampa pole maza house,(im a Leo, sijui ndo maana niko somehow controlling?)
huyo daughter nae (nna wivu na babangu kuliko Paw aisee. Babangu na kaka zangu, hehehe! Ntahamisha mtu mjini!). Ningekuwa mie ndo yeye nahisi ningeweka distance kiduchu pia.

Ila on a serious note, tabia ya kwenda kulala kwa watu siipendi! Uliwezaje.kwenda kukaa kwa huyo mama wiki, angekumwagia maji ya moto ukiwa umelala je?
kazi ipo.

Ngumu kumesa, kama anakufadhili badi akuadopt uje uishi kwetu mazima.
 
Back
Top Bottom