Kosa la mkwe ni lipi?

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
27,900
Reaction score
29,431
Kuna jamaa yangu mmoja ametembelewa na mama mkwe wake kutoka 'mkoani'. Jamaa amebahatika kupata mtoto wa kike ambaye kwa sasa ana umri wa mwaka mmoja.

Siku moja jamaa alikuwa anatoka kuoga bafuni akiwa amejifunga taulo lake, mtoto wake aliyekuwa amebebwa na mkwewe akashuka na kutambaa kwa furaha kuelekea kwa baba yake. Jamaa akaona sio vizuri kumpita mtoto hivi hivi, akamnyanyua kutoka chini akawa anamrusha juu na kumdaka.

Alipomrusha mtoto kwenda juu wakati bado akiwa hewani, taulo alilokuwa amejifunga likawa linakaribia kudondoka chini. Akapiga hesabu za haraka akaona afadhali amdake mtoto na kuacha taulo lidondoke. Akabaki mtupu mbele ya mkwewe. Baada ya kumdaka mtoto ndipo akajifunga taulo lake na kusepa kwa aibu.

Cha ajabu, badala ya mama mkwe kumpongeza mkwewe kwa ujasiri wake wa kuchagua kumdaka mtoto na kuacha taulo, akabaki anamlaumu kwa kumkalia uchi huku akiapa kumuadhibu na kumtoza faini ya kimila kwa 'kosa' hilo.

Hili ni sawa kweli wandugu? Mimi naona jamaa anaonewa. Kosa lake ni lipi hasa?
 
Hii kitu niliisoma zamani sana enzi za vijarida vya Sani...
 
mi nadhani angeenda tu ndani kwa ushujaa na kushangilia kwa kumuokoa mwanae!

mwambie mama mkwe nae apange ratiba mapema ya kurudi mkoani (dar es salaam).
 
Hii kitu niliisoma zamani sana enzi za vijarida vya Sani...

Huyu jamaa atakuwa kachelewa kukua. hata binti yangu wa std six anaijua hii hadithi ya Abunuwas
 
Huyu jamaa atakuwa kachelewa kukua. hata binti yangu wa std six anaijua hii hadithi ya Abunuwas

Mpwa halafu njemba imekomalia kuwa ni true story na picha zipo...

Hebu ngoja tusubiri huenda ni zile alikuwa akichora Ibra Radi Washokera au Marco Tibasima...
 
dah, umenikumbusha mbali, hivi marko tibasima yupo jamani!
Mpwa halafu njemba imekomalia kuwa ni true story na picha zipo...

Hebu ngoja tusibiri huenda ni zile alikuwa akichora Ibra Radi Washokera au Marko Tibasima...
 

Hii hadithi niisoma kwenye kitabu cha Bulicheka mfalme wa wagagagigikoko
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…